Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4222 articles
Browse latest View live

MKUTANO MAALUM WA WADAU WA FILAMU ZA MAADILI

$
0
0
WASANII,WATAYARISHAJI, WASAMBAZI,WATAZAMAJI NA WAANDISHI
                            WOTE   MNAKARIBISHWA

Asalaam Alaaikum Warhmatullah Wabarakatuhu
Tunapenda kuwajulisha wadau wa maadili movies nchini kutakuwa na mkutano wa mkubwa utakaofanyika tarehe 31 Mai 2015 kuanzia saa 2.00 asubuhi ukumbi wa Jaffar Complex uliopo  Mnazi mmoja jijini Dar es salaam  
AGENDA ZA MKUTANO
Kuandaa daftar la orodha ya wasanii na kuchagua rasmi aina ya mfumo wa filamu zetu na mengineyo
Kuchagua uongozi wa wa muda uliona mpangilio rasmi na kuupa majukumu likiwepo la
  1. Kuanzisha mtandao wenye hamasa na mwelekeo kwa wassii wote wa maadili Africa mashariki na Africa kwau ujumla
  2. Kushirikiana na kujenga na kuunga mkono kuimarisha soko la filamu
Tunapenda kuaalika waandishi wa habari watunzi waongozaji  wasambazaji na hata watazamaji wa filamu za maadili wasanii wote nchini tunawaalika ila stara ya mavazi kwa wanawake izingatie muhimu kwa wanawake  
"Maadili Movies Lengo ni kusimamia ulinzi wa maadili mema kupitia filamu za Kitanzania, kuazisha, kuendeleza na kuhamsisha uwepo na ukuwaji wa filamu zenye heshima, zinazozingatia maneno, matendo na mavazi yenye maadili."
Tuwe pamoja wana

  • BURUNDI
  • RWANDA 
  • KENYA
  • UGANDA
  • CONGO
  • TANZANIA na AFRICA KWA UJUMLA
Kwa mawasiliano ya simu kwa wale watakaoshiriki kutoka nchi tofauti tofauti pamoja na nchini ,Tafadhali tuwasiliane kwa simu kwa namba zifutazo:

WANAOUA ALBINO WAMUHOFIE MUNGU - IPTL

$
0
0
Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. [/caption] Na Mwandishi WetuKAMPENI maalumu za kupinga mauaji ya watu wenye u-albino nchini inayojulikana kama 'Imetosha' iliyoanzishwa na balozi wa kujitolea, Henry Mdimu, chini ya Imetosha Foundation zimezidi kushika asi baada ya makampuni ya IPTL na PAP kutoa shs milioni 10 kusaidia kampeni hizo. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege jana alimkabidhi balozi Mdimu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kama ishara ya kuunga mkono kampeni hizo za kutoa elimu kutokomeza imani potofu zilizojengeka kwa baadhi ya wanajamii juu ya watu wenye albino. Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Makandege alisema matukio ya mauaji au kukatwa viungo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino yamefika hatua ya kutisha nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu kila mmoja bila ubaguzi kushiriki kusaidia mapambano hayo. Alisema ulemavu wa ngozi waliyonao watu wenye albino ni mapungufu ya kibaiolojia ambayo ni mapenzi ya Mungu hivyo imani potofu zinazoendelea hazina budi kupigwa vita kwa nguvu zote. "...Kuna minongono mitaaani kwamba watu wanatenda matukio hayo wana imani potofu kwamba ukitumia kiungo cha mtu mwenye albinism, ndipo utafanikiwa. Kama kweli viungo vyao vingekuwa vinaleta utajiri, basi watu wenye albinism wangekuwa matajiri namba moja duniani," alisema Makandege akizungumza. "...Sisi IPTL na PAP tumeguswa sana na jambo hili. Kwa wote wanaofanya matendo haya, mnapaswa kuwa na hofu ya Mungu mkijua kuwa siku ya kihama, kila mtu atajibu na kuhukumiwa kwa matendo yake. Tunakubaliana kabisa na wenzetu IMETOSHA Foundation kwamba, imefika wakati kila Mtanzania, na hata wageni waishio Tanzania, kusema IMETOSHA na kusimama kidete kuwalinda hawa ndugu zetu," alisisitiza kiongozi huyo wa IPTL. Aidha kampuni za IPTL na PAP zimeyataka makampuni mengine nchini na watu binafsi kuungana kwa kuchangia harakati hizi za imetosha ili kusaidia kampeni ya imetosha kupita mikoa ya kanda ya ziwa kupaza sauti na kuielimisha jamii juu ya uwepo wa imani potofu zinazoendeleza mauaji ya watu wenye u-albino. Kwa upande wake Balozi wa Imetosha, Mdimu aliishukuru kampuni za IPTL na PAP kwa moyo wauliouonesha wa kusaidia harakati hizo na kumtaka kila Mtanzania kwa nafasi yake kusaidia kupaza sauti kwamba imetosha mauaji na unyanyasaji wanaoupata watu wenye ualbino. Alisema mauaji haya yanamgusa kila Mtanzania na kuendelea kuichafua nchi yetu hivyo kumtaka kila mmoja kupaza sauti yake kupinga vitendo hivyo. Machi 28, 2015 Imetosha Foundation inatarajia kufanya matembezi ya hisani kuchangisha fedha zaidi ili kusaidia kampeni za kukomesha mauaji ya watu wenye u-albino kabla ya kuanza rasmi safari za kuzunguka katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na wasanii waliojitolea kueneza elimu hiyo kwa jamii moja kwa moja.

KITCHEN PARTY (MJUBURO) WA BIBIE RUKIA NADHIR RAJABU KUFANYIKA TAR 19/4/2015 KATIKA YA UKUMBI WA LINAS

$
0
0
Mama Amina Sued Kagasheki wa Mtaa wa Twiga (Bilele ) Mjini hapa anapenda kuwafahamisha na kuwaalika ndugu , majirani na marafiki wa familia yake kushiriki katika Shughuli ya kumfunda,kumzawadia na kumuelimisha binti yake kitinda mimba (pichani) Omwana Rukia. Shughuli hiyo inatalajiwa kufanyika tarehe 19/4/2015 katika ukumbi wa Linas Night Club Nyote mnakaribishwa!!

KUUNGUA MOTO MABWENI YA MABIBO

$
0
0
 Baadhi ya Mabweni ya wasichana katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Campus ya Mabibo yameteketea kwa moto chanzo kikidhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Hata hivyo wanafunzi hao wameonekana wakililaumu jeshi la zimamoto kwa kuchelewa kuja kuzima moto hal;I iliyowachuukua muda wanafunzi hao kuzima moto huo wao wenyewe na hivyo gari la zimamoto lilivyofika kukuta tayari moto huo umeshapunguza makali yake.Endelea kufuatilia taarifa zetu kufaham zaidi

MASHINDANO YA NANI MKALI YAENDELEA KUCHUKUA KASI !

$
0
0
Msimu wa pili wa mashindano  ya 'NANI MKALI'  yanayo andaliwa na TESSO BOY Entertainment  yameendelea tena kufanyika mwishoni mwa juma hili katika fukwe za Kiroyera Mjini Bukoba..
 Mmoja wawasanii maarufu kwa jina la 'Kirokoroko'akiwajibika katika jukwaani katika mchuano wa 'NANI MKALI' unao endeea kuchukua kasi Mjini hapa kwa kuwakutanisha Vijana mbalimbali wenye vipaji tofauti kwa lengo la kutafuta nani Mkali wao

 Mkali  wa miondoko ya Ragga na Dancehall akifanya yake jukwaani
Ndivyo anavyo onekana pichani Jaji kiongozi wa mashindano hayo.
Wasanii wakiendelea kuwajibika
 Ni Wasanii na Vipaza...!
 Taswira mbalimbali kutoka viwanja vya fukwe za Kiroyera katika shindano lake la Nani Mkali lililofanyika jumapili ya jana March 15,2015
 Kushoto ni mshiriki wa  mashindano hayo akiwa jukwaani na Mzazi wake .
Sehemu ya Umati wa watu wakati mashindano yakiendelea kufanyika
Msanii anayefanya vyema katika michano Michano (The Mic King)  mara baada ya kushuka jukwaani kushiriki mashindano ya 'Nani Mkali' yaliyofanyika jumapili ya jana katika viwanja vya fukweni Kiroyera.
 Mmoja wa Mc Muongozaji wa mashindano hayo
 Umati mkubwa ukifuatilia mchuano wa wasanii wanaotikisa katika fani mbalimbali Mji hapa
Wachaa Kabisa....!

Meza ya Majaji wa Shindano la 'Nani Mkali' katika Uigizaji,kuimba na kucheza.

 Meza ya Wadau wakubwa katika tasnia ya burudani , Shangwe na Kadansee Mjini hapa.
TESSO BOY Entertainment ambao ndio Waratibu na waandaaji wa Mashindano ya 'Nani Mkali' katika tasnia ya kucheza muziki ,kuimba na Uigizaji mkoani Kagera wanasema fainali za  mashindano haya yanayo endelea kila siku za Jumapili  itafanyika siku ya Pasaka katika Viwanja vya fukweni Kiroyero Mjini hapa.
Mdau pichani kushoto akiwa na muandaji wa mashindano hayo Mpambanaji  Tesso Boy 
 Meza ya Majiji katika mashindano hayo.
 Mkali katika Miondoko ya Hip hop akiimba Accapella na freestyle kama vile Kendrick Lamar 
 Mmoja wa washiriki akiendelea kuonyesha uwezo wake jukwaani
 Mzee wa 'Kirokoroko' msanii aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia 'Nani Mkali'
 MWISHO wa Matukio ya picha yaliyojiri Jumapili hii katika Viwanja vya fukweni Kiroyera katika Shindano la Nani Mkali.

ATANGAZA NIA KUMRITHI MAMA TIBAIJUKA

$
0
0
Anaitwa Roderick Lutembeka. Ni mzaliwa wa kijiji cha Buganguzi kata Buganguzi wilayani Muleba mkoani Kagera.
Anatarajia kugombea ubunge wa jimbo la Muleba Kusini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mbunge wa sasa ni Prof. Anna Tibaujuka ambaye kimsingi hana tena 'credibility' ya kuwa mbunge wa Jimbo hili kwa kile kinachotajwa na wengi kuwa tangu awe mbunge hajawahi kuitisha mkutano wa wananchi wake kusikiliza kero zao, hajafanya lolote la maana la kukumbukwa na mbaya zaidi amechafuka kwelikweli kutokana na sakata la Escrow lililopelekea kung'olewa kwenye kiti chake cha uwaziri.
Aidha ile kauli yake aliyoitoa kwenye baraza la maadili lililopelekea kuvuliwa wadhifa wake wa UNEC- CCM, ya kutumia milioni kumi (10,000,000/=) kwa ajili ya mboga tu imechefua wengi na hivyo kutafsiriwa kama MTU anayejikweza, mwenye dharau, mwingi wa kiburi na majivuno kwa watanzania hususani wale wa Muleba Kusini anaowawakilisha bungeni.
Hivyo kwa kuwa habari ya mjini ni CHADEMA, basi kuna uwezekano mkubwa mbunge ajaye atatoka chama hiki na chaguo la wanachama na wana Muleba walio wengi ni huyu ndugu Roderick Lutembeka; mwenye hekima na busara za hali ya juu, mwanasiasa mzalendo, mwadilifu na msomi nguli na mahiri mwenye uwezo jadidi na uzoefu wa kutosha katika masuala ya Uchumi na Fedha pamoja na Uongozi.
Ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Lutembeka ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Taifa na hii inampa nafasi ya kuwa miongoni mwa 'mainjinia' wa Chama hiki kinachokua kwa kasi ya roketi!

ELIMU YAKE:
Shule ya Msingi: Mubango, Buganguzi
Shule ya Kati (middle school): Biirabo, Nshamba
Shule ya Sekondari (O-Level): Balimi Sekondary, Bukoba
(A- Level): Ndanda High School, Songea
Alijiunga na chuo kikuu cha Dar-es-Salaam kuchukua shahada ya Uchumi, BA(Economics) akahitimu mwaka 1987 na kuajiriwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi yaani National Board of Accountancy and Auditors (NBAA) kama Muhasibu Msaidizi hadi mwaka 1995 ingawa alihudumu pia kama Muhasibu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Arusha mwaka 1990.
Wakati akiwa Muhasibu Msaidizi wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA) alipata fursa ya kujiendeleza kielimu.
Mwaka 1993 alitunukiwa Certificate in Programming (UK) na akaongeza Diploma in System Analysis and Design (UK)
Mwaka 1994 alitunukiwa Stashahada ya juu katika masomo ya Kompyuta, yaani Advanced Diploma in Computer Studies (UK)
Mwaka 1995 alienda Chuo Kikuu cha Salford (UK) kusomea Shahada ya Uzamili MSc (Business Management and Information Technology)
Alirudi nchini Tanzania akafanya kazi kama Mshauri (Consultant) katika Kampuni ya Price Waterhouse Coopers hadi mwaka 2009 alipong'atuka rasmi na kuanzisha Kampuni binafsi ya masuala ya Ukaguzi ambapo alifanya kazi kama Auditor au Freelance Consultant hadi 2014 alipoombwa na Chadema kushiriki katika harakati za Ukombozi wa Taifa na kuchaguliwa kuwa Katibu wa Taifa wa Baraza la Wazee la Chama, nafasi anayoishikilia hadi sasa.
UZOEFU:
Akiwa Mshauri na Mkaguzi wa masuala ya Fedha na Uchumi, ndugu Lutembeka amesaidia mashirika ya umma na ya binafsi kuboresha utendaji wao wa kazi.
Ameshiriki katika ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwenye Halmashauri mbalimbali za wilaya, mikoa, manispaa, wizara na taasisi mbalimbali za umma na hivyo kupata uzoefu wa kutosha kuhusu utendaji wa Serikali na Usimamizi wa Fedha za Umma.
Aidha, ndugu Lutembeka ni mwanzilishi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali (N.G.O) ya Maendeleo Buganguzi yenye jina Buganguzi Development Association (BUGADEA). Ni taasisi inayojishughulisha na Uhamasishaji wa matumizi ya raslimali zilizopo kwa Maendeleo ya Wilaya ya Muleba.
Kwa sasa BUGADEA inafadhili ujenzi wa Kituo cha Afya kata Buganguzi, mradi unaokadiriwa kutumia kiasi cha shilingi milioni mia NNE (400,000,000/=)
Huyu ndiye Roderick Lutembeka, mrithi wa Prof. Anna Tibaijuka.
Muungeni mkono kwa Maendeleo na ustawi wa Jimbo la Muleba Kusini.
Wana wa Muleba Kwetu na wafuatao mnakaribishwa KUTOA MAONI yenu

AMAZING VIDEO:INCREDIBLE LEOPARD AND BABY BABOON INTERACTION!

AK 47 NDUGU YAKE CHAMELEONE AFARIKI DUNIA!!

$
0
0

 Taarifa kutoka nchini Uganda zinasema kuwa mwanamuziki wa Dancehall nchini Uganda anayefahamika kwa jina la AK47amefariki dunia usiku wa leo baada ya kuanguka akiwa bafuni anaoga. Taarifa zinadai kuwa AK47 amefariki saa 5.30 usiku ya tarehe 16, Machi, 2015 baada ya kukimbizwa katika hospitali ya Nsambya jijini Kampala ambapo taarifa za madaktari zinadai kuwa damu nyingi ilivujia ndani baada ya kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa chake. 
Kupitia ukurasa wake wafacebook  haya ndiyo maneno ya Msanii Jose Chameleone  kuhusu msiba huu:DEATH ANNOUNCEMENT!Death has robbed us off Emmanuel Mayanja also known as AK 47. To all our friends May God Give us All strength to stand in such a trying time.
My Brother you have Gone too soon.
RIP

KUTOKA MAGAZETINI LEO J'NNE MARCH 17,2015

$
0
0
BILIONI 8 ZIMETENGWA KUWAMALIZA WAJUMBE WA PAC - ZITTO
Takriban miezi mitatu tangu sakata la uchotwaji wa fedha zaidi ya Sh. bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow kutikisa nchi huku mawaziri wawili na mwanasheria mkuu wa serikali wakiondoka madarakani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amefichua kuwa wajumbe wote wa kamati hiyo wataadhibiwa vibaya kwenye majimbo yao kama njia ya kulipiza kisasi kutokana na kuwaumbua wote walionufaika na fedha hizo. Katika mahojiano na kituo cha ITV kwenye kipindi cha Dakika 45, kilichorushwa jana usiku, Zitto amesema kuwa wakati PAC wakiendelea kuchambua ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya Escrow, mjumbe mmoja wa kamati hiyo aliitwa na ‘wakubwa’na kuelezwa kwamba akifika bungeni awageuke wenzake na aseme kuwa mgogoro wa ripoti ya Escrow iliandikwa kwa shinikizo la mfanyabiashara mmoja.
Aliongeza kuwa mjumbe huyo alipokataa aliambiwa: “ Umekataa kutekeleza hili? Sasa tumetenga Sh. milioni 500 kwa kila jimbo kwa kila mjumbe wa PAC ili kuhakikisha hawarudi bungeni.”

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza katika tovuti yake majina 287 ya washtakiwa waliopatikana na hatia katika kesi za rushwa na miongoni mwa waliotajwa wamo wafanyabiashara, wanasiasa,waandishi wa habari, walimu, wauguzi, polisi, mwanafunzi na watumishi mbalimbali wa umma.
CHADEMA YAIGARAGAZA CCM MARUDIO UCHAGUZI SERIKALI MITAA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibuka na ushindi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa katika mtaa wa King'azi B, Kata ya Kwembe, jijini Dar es Salaam. Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo, George Lupia, alisema Chadema kimeshinda nafasi zote hizo dhidi ya wapinzani wake CCM na hivyo kuwa viongozi wa mtaa huo. Msimamizi huyo alisema kuwa mgombea wa Chadema, Donath Mtemekele, alishinda kwa kupata kura 585 huku wa CCM, Daud Ngaliba, akipata kura 376 na kwamba kura 18 ziliharibika.

Imetosha Movement Kufanya Matembezi Hisani Machi 28

$
0
0
Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni.[/caption] Na Mwandishi WetuASASI ya Harakati za Imetosha ilioanzishwa kupinga mauaji na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye u-albino inatarajiwa kufanya matembezi makubwa ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa uma juu ya imani potofu zinazoendelea za mauaji ya albino. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu amesema matembezi ya hisani kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015. Alisema matembezi hayo yataanzia katika Viwanja vya Leaders na kuzunguka maeneo yaliyopangwa kisha kurejea viwanjani hapo kwa ajili ya shughuli maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati maalumu za imetosha zitakazo kwenda kwa jamii ya kawaida na kueneza elimu ikiwa ni juhudi za kuhamasisha kila mwana jamii kupaza sauti na kusema 'Imetosha Mauaji ya Albino'. "...Baada ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo, karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu," alisema Mdimu katika taarifa yake. Aidha akizungumzia uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa kuna taratibu za kufuata kabla ya uandaliwa shughuli hizo. "...Hili suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu za kisheria ili upate kibali. Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu kuahirishwa. "Tulikuwa tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili wa Imetosha...sasa imetosha imekuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT. Napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu," Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi sa mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi. _________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

BALOZI KAMALA AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MAANDALIZI YA KONGAMANO LA BIASHARA LA AFRIKA NA UBELIGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na WAjumbe  wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Biashara la Afrika na Ubeligiji linalotarajiwa kufanyika Ubeligiji mwezi ujao. Wajumbe hao wamekutana na Balozi Kamala ofisini kwake Brussels. Tanzania ni nchi pekee kutoka nchi zinazozungumza kingereza iliyohalikwa kushiriki Kongamano hilo.

MAHOJIANO YA ZITTO KABWE KATIKA KIPINDI CHA DAKIKA ZA 45 ITV

$
0
0
Katika mahojiano haya, zitto anatoa maelezo yote juu ya tuhuma dhidi yake. Swali: Mwaka 2009, ulitaka kugombea uenyekiti wa Chadema, uamuzi huo ulikuwa ni wako mwenyewe ama kuna watu nyuma yako walikushawishi kufanya hivyo? Jibu: Chadema nilivyoingia kwenye uongozi Makao Makuu, kulikuwa na wabunge watano, wanne wa kuchaguliwa na mmoja wa viti maalumu. Nilivyoingia pale nilipewa nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na wa Mambo ya Nje kwa ajili ya kujenga mahusiano ya chama chetu na vyama vingine vya kimataifa, hiyo kazi niliifanya kwa ubora na mpaka sasa uhusiano wote ya Chadema na vyama vya nje, niliyajenga mimi. Mwaka 2005 niliandika mkakati wa uchaguzi tukapata majimbo mengi zaidi, tulipata asilimia nane ya kura hivyo tukapata wabunge sita wa viti maalumu. Kabla ya hapo Chadema ilikuwa ikizidiwa hata ya UDP, pamoja na kwamba kilikuwa na wabunge tangu 1995.

Wabunge wake hawakujitanabaisha kama wapambanaji wa misingi ya kitaifa, tulivyoingia (Bungeni) sisi na kina Ndesamburo (Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo), DK Slaa (Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa), tukaanza kubadilisha hali hiyo.

Tukaanza kupambana na ufisadi, kabla ya hapo Dk. Slaa alikuwa bungeni kwa miaka 10 lakini hakuwa machachari kama ilivyokuwa kuanzia 2005. Alivyoingia mwaka 2005 ndipo tukaanza na hoja kama zile za EPA na Buzwagi. Baada ya hapo mimi na kina Profesa Kitila Mkumbo tukaona kuna haja ya kubadilisha chama, mwaka 2009 nilivyotaka kugombea uenyekiti nilikuwa na nia ya dhati kabisa.

Ndani ya Chadema kuna watu wanaamini katika uliberari, kama biashara na mtaji, hawa ni watu kama kina Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), sisi tunaamini katika demokrasia ya jamii. Hapa kwenye kundi hili unatukuta mimi kina Profesa Mkumbo, Profesa Mwesiga Baregu, na wenginr, tulitaka kukitoa chama kwenyel mrego wa kihafidhina kwenda kwenye ujamaa. Hata hivyo wazee walinitaka niache kugombea nikaacha, ni kweli ukiangalia chanzo cha ugonzi ni mwaka 2009, ila mimi sikudahani kama kitu kile kingeleta chuki, nilidhani mambo yangeishia pale. Swali: Nini kilifanya iwe vigumu kumaliza tofauti zako na Chadema? Jibu: Mara zote nimekuwa nikiwaambia Chadema kwanza waniambie kosa langu ni nini, Ndesamburo aliwahi kunifuata ili tuyamalize, Wenje naye alinifuata na siku kutaka tuyamalize, lakini upande mwingine viongozi nao wanasema yao kwa hiyo ni undumilakuwili tu kila mahali. Swali: Kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa wewe na Mbowe mna ugomvi binafsi, tofauti na vile ambavyo watu wanadhani kuwa mnagombea uongozi. Wengine wanasema uliwahi kutoa siri zake, juu ya kuwa na nyumba Dubai, madai haya yana ukweli? Jibu: Kama Mbowe ana mali nje mimi kwa kweli sijui, mimi nilitoa hoja ikaundwa kamati ya uchunguzi, kama ilimkuta ana mali nje sijui. Hata hivyo kama ana nyumba, ama mali nyingine ni kwa nini auogope? Kama una nyumba Marekani, Afrika Kusini, Dubai ama wapi hiyo siyo tabu, ilimradi kwenye tamko la maadili (Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma) uwe umesema kuwa unazo na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wajue umepata wapi hizo fedha. Swali: Lakini inadaiwa kuwa ulikaa na Mbowe wewe akakueleza kama mtu wake wa karibu kuwa ana nyumba Dubai na wewe ukatoa hizo habari kwa umma na ndicho kilichomuudhi. Jibu: Mimi sijawahi kukaa na Mbowe kuzungumza hayo mambo. Sina ugomvi binafsi Mwenyekiti wa Chadema, siku zote nimekuwa nikimchukulia kama kaka, ndiyo maana hata akinishambulia nimekuwa nikijitahidi kukaa kimya. Mwanzoni kabisa yeye alikuja chuo kikuu kunifuata, mwanzoni mwa mwaka 2001, nikiwa mwanachama wa Chadema lakini siyo kiongozi, yeye akiwa Mbunge wa Hai, alikuja akaniambia naomba tuzungumze utusaidie kwenye chama. Alikuwa anataka kufanya mabadiliko ya katiba ya chama, nikatumia nafasi yangu ya uanaharakati wa wanafunzi na uwezo wangu wa uchambuzi tukafanya hivyo tulivyofanya. Tukabadilisha chama mimi na yeye, mabadiliko makubwa ambayo yanaonekana hivi sasa Chadema ni kazi ambayo tulifanya mimi na yeye, hata gumboe mwaka 2009 niliona ni jambo la kawaida. Kilichopo ni mitizamo tofauti ya namna ya kuendesha siasa, na tofauti hizo zimesababisha yatokee yaliyotokea. Wakati mwingine nikikaa peke yangu huwa yangu na kujiuliza, huwa sioni msingi wa ugomvi wangu na chadeama, naona ni ugomvi tu wa madaraka na juhudi za watu kutaka kuondoa wengine katika ulingo. Katika mazingira kama hayo ni rahisi kutoa tafsiri kwamba kuna ugomvi binafsi. Yeye (Mbowe) alikuja hapa Kigoma akafanya mkutano wa hadhara akanitukana, akasema alinisaidia sijui gari, sijui nini, yaani alikuja nyumbani kwetu kunisimanga. Nikasema huyu mtu ananisimanga, kwanza ni mambo ya kishamba, kwamba unamsaidia mtu halafu unakuja kumsema, kwanza kuna vitu ambavyo mimi mwenyewe nimemsaidia labda kifedha ama siyo fedha, na tunajua kati ya mimi na yeye. Siyo vitu naweza kuibuka nikasema nilimdharau sana kwa kweli, na juzi nimemsikia huko Shinyanga akisema kuwa hawezi kukaa na kuongea na mimi kwamba ni msaliti na mambo kama hayo. Huu ni undumilakuwili kwa kweli kwa sababu huku anatuma watu kwamba kina Ndesamburo (Philemon Ndesamburo), kwamba tuongee tuone namna ya kuyamaliza haya mambo alafu yeye huku nyuma akikaa anaongea yake. Kwa hiyo binafsi naamini sina ugomvi naye sanasana ni tofauti za kiitikadi. Mimi na yeye tumekaa Bungeni miaka 10, naomba tu watu watupime. Katika miaka yangu 10 ni hoja gani nimezisimamia na yeye ni zipi amezisimamia. Mimi siku zote siasa zangu ni hoja na issue za kusaidia wananchi na nafurahi ninavyosimamia vitu na kuona vikienda. Swali: Mara kadhaa viongozi wa chama chako wamekuwa wakikutuhumu kwa kusaliti chama, na kwamba kwa upande mmoja unatumiwa na CCM na upande mwingime usalama wa taifa, ni kwa nini ushutumiwe kwa tuhuma kama hizo? Jibu: Kwenye siasa ukitaka mwanasiasa amalizike ni kumpa hizo tuhuma. Lakini waulize (Chadema), ni taarifa zipi zinapelekwa kwenye usalama wa taifa, watu haohao walisema siendi kwenye vikao vya chama, wala ofisini, sasa hizo taarifa ninazozipeleka ni zipi wakati kwenye vikao wala ofisini siendi? Mtu anayepeleka taarifa ni yule asiyekosa kwenye vikao. Anahudhuria kila kikao ili apate taarifa za kupeleka. Lakini pia angalia, mwaka 2010 nilitoa taarifa ya kumuomboa Waziri Mkuu, hoja ile ikaungwa mkono kwa kusainiwa na wabunge wa pande zote, hivyo ikasaidia kuondoa baadhi ya mawaziri waliokuwa na shutuma. Mwaka 2013 kulikuwa na Operesheni Tokomeza. Ripoti ya Kamati ya Bunge iliyokuwa imewasilishwa ilikuwa inamtaja waziri mmoja tu, lakini nilisimama na kujenga hoja mawaziri wengi tu wakaondolewa. Mwaka 2014 nimepeleka hoja ya Escrow na nikaisimamia, mawaziri wameondoka, serikali imetikisika, sasa mtu anayetumika na Chama Cha Mapinduzi kwa nini aiangushe serikali ya chama hicho mara tatu ndani miaka mitano? Mtu ambaye anatumika inawezekanaje alete mjadala utakaoingusha serikali? Ndiyo maana sipotezi muda kujibizana na propaganda za aina hiyo, watuambie ni taarifa gani zilipelekwa huko zikawaathiri? Swali: Baada ya Mahakama kutoa uamuzi wake na Mwansheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu kutangaza kuwa umefukuzwa uanachama kwa kuwa kukishitaki chama ni kujifukuza katika chama moja kwa moja, tangu ukiwa kiongozi wa chama uliwahi kukitilia shaka kifungu hicho kwa kuwa hivi sasa umeonekana kukilalamikia. Jibu: Hiki kifungu kipo kwenye kanuni na wala siyo Katiba, kilitungwa mwaka 2013. Mwaka huo kuna mabadiliko fulani fulani yalifanywa. Mabadiliko yale yalikuwa na malengo fulanifulani ikiwamo kulenga watu fulanifulani. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, mamlaka ya kutoa haki iko kwenye chombo kimoja tu nacho ni Mahakama, kila raia ana haki ya kwenda mahakamani kudai haki, unaposema mwananchama wa Chadema akienda mahakamni amejivua uanachama ina maana wewe huitambui Katiba ya Jamuhuri. Hii ina maana kama mwanachama amekipangisha chama, na chama kikashindwa kulipa kodi, yule mwanachama akienda mahakamani amejivua mwenyewe uanachama kwa kuwa haruhusiwi kwenda mahakamani. Hicho ni kipengele ambacho hakikupaswa kuwap, Wanachama wa Chadema waende mahakamani kushtaki kipengele hicho ili kitangazwe kuwa siyo halali. Chama kinachopambana kushika dola hakipaswi kuwa na vipengele kama hivi. Ila yote kwa yote hiki kipengele kimewekwa mwaka 2013 na mwaka 2015 kikatumika kwangu, ni wazi kilitungwa kwa ajili yangu.

Swali: Baada ya kufukuzwa Chadema, ni nini hatma yako kisiasa? Jibu: Nina ziara ya kuzunguka na wananchi wa jimbo langu kuangalia jinsi ya kuwatumikia, leo (jana) nawaaga rasmi kwamba sintakuwa nao baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, lakini ni nini kinachokuja baadaye ya hapo tutakijua vizuri wiki ijayo (wiki hii). Hatujajua kama Chadema wameandika barua kwa Spika ili kunitangaza kuwa jimbo liko wazi, kama ndivyo tutakaa kujua ni nini cha kufanya. Ilipaswa baada ya kesi kwisha taratibu zifuatwe, mpaka sasa sijapata taarifa zozote za kufukuzwa ndiyo maana nasema mpaka wiki kesho iishe tutajua, nitakuwa na nia ya kuendelea kutumikia kwenye jimbo lolote Oktoba. Swali: Una mpango wa kujiunga na ACT? Jibu: Tusijaribu kuvuka mto kabla hatujafika pa kuvukia. Swali: Vipi hukumu ya Mahakama Kuu juu ya kesi yako na Chadema? Jibu: Kwenye kazi yangu kuna miguu ya watu wengi naikanyaga, taarifa yangu ya Escrow nimewakanyaga mpaka mahakama. Kwa hiyo yawezekana kabisa mahakama iliona hapa ndipo kwa kunikanyaga, ama yawezekana kabisa ni taratibu. Inaonekana kuna uhusiano wa karibu wa mahakama na wanasheria wa Chadema, sisi tulisikia kwenye vyombo vya habari kwamba hukumu ya kesi yetu imetolewa. Hata baada ya hukumu hiyo, tulijaribu kufuatilia ili kupata hukumu, kwa siku mbili tulizungushwa, siku ya tatu tukaambiwa kuwa jalada lipo kwa jaji kiongozi. Lakini mimi bado nina imani kwamba wakuu wa mahakama watachunguza jambo hili na kuona kama kuna cha kufanya. Sisi tulipaswa kuitwa mahakamani, lakini hatukuitwa, kuna taratibu za mahakama hazikufuatwa, tuna imani kuwa viongozi wa mahakama watachunguza kama kuna suala la rushwa katikati hapa ama kuna nini. Lakini pia hali hii imenifanya niwe na kiu zaidi ya kuhakikisha nikipata tena nafasi nitafanya operesheni kwenye mfumo wa mahakama kwa kuwa umekuwa na malalamiko sana ya kuwaumiza wananchi.

ZITTO KABWE BUNGENI LEO

$
0
0
Siku moja baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda kusema kuwa Zitto Kabwe ni mbunge halali wa jimbo la Kigoma Kaskazini kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa rasmi ya kutenguliwa ubunge wake, mbunge huyo leo amehudhuria mkutano wa bunge unaoendelea mkoani Dodoma.
Katika siku hiyo ya kwanza ya kuhudhuria bungeni hapo mara baada ya chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA ambacho alikuwa mbunge kupitia chama hicho kumfukuza uanachama Mhe.Zitto Kabwe amelalamikia hatua ya Serikali kutowatendea haki wakazi wa Kilwa kwa kutowanufaisha na gesi inayopatikana eneo hilo.
 
Katika kikao hicho Zitto Kabwe amesema kumekuwa na malimbikizo ya fedha ambazo kampuni inayohusika na kuchimba gesi katika eneo la Songosongo Wilayani Kilwa ilitakiwa kulipa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa lakini tangu kuanza kwa uchimbaji huo kampuini husika haijalipa fedha hizo.
 
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa nishati na madini Charles Kitwanga ameliambia bunge kuwa tayari Serikaliimegundua madhaifu hayo na kwamba kwa sasa ipo katika mchakato wa kutathmini halmashauri hiyo inadai shilingi ngapi na hatimaye iweze kulipwa.

NONDO KWA JUMATANO YA LEO MARCH 18,2015

$
0
0
Watoto kwenye ndoa sio chanzo cha furaha, na wala hawaji kuleta furaha bali wanakuja kuongeza na kuendeleza furaha iliyokuwepo baina yenu ninyi wapenzi. Ukiona mtu anasema watoto wameleta furaha maana yake haikuwepo awali. Watoto hawawezi hata sikumoja kuchukua "kureplace" nafasi ya furaha ya ndoa, ndoa inafuraha yake na watoto wanafuraha yao, vyote hivi vinaleta ukamilifu wa furaha ya kweli. Inauma sana pale furaha ya ndoa inapokufa na mtu anabaki tu kwa ajili ya watoto, inasumbua moyo sana pale mtu anapoona hapati tena furaha kutoka kwa mume au mke wake na anaamua kuhamishia mapenzi kwa watoto. Utamu wa asali ni wa asali na utamu wa sukari ni wa sukari ingawa vyote ni vitamu na vyote hutumika kwenye chai, kimoja kimetoka kwenye mmea na kingine kwenge mdudu. Jifunze kutofautisha na kuiheshimu tofauti iliyopo.
 Mara nyingine kwenye mahusiano mmoja anaweza kuamua kuanzisha mazingira ya ugomvi ili tu hali ya hewa ichafuke yeye apate upenyo wa kutoka na kwenda kwenye mchepuko au kwenye mishemishe nyingine. Kikawaida ni ngumu kuamua kuondoka kwenda kumsaliti unayempenda wakati anakuchekea na kila kitu baina yenu kiko sawa, hii inaitwa "guilty conscious" ingawa wako ambao hawana hiki kitu na wanaweza kukusaliti katikati ya kipidi cha amani na furaha tele. Sasa wengi hutumia mbinu inaitwa "chafua hewa utoke", yamkini hata haendi kwa mwanamke bali anaenda kwa marafiki zake au kwenye kinywaji na anajua wewe ni kipingamizi cha kutoka kwake basi anaamua kuchafua hali ya hewa ili asepe. Sasa basi maranyingine ukiona mwenzako anakuvuruga mivurugo isiyo na sababu kabla ya kumuuliza "kwanini unafanya hivi ?", muulize " unataka kwenda wapi?" - Chris Mauki

MCHAKATO MAJIMBONI 2015:KIJANA STEVEN THOMAS TUMAINI KUPITIA CCM ATANGAZA NIA KUGOMBEA JIMBO LA MULEBA KUSINI

$
0
0
Pichani ni Ndugu Steven Thomas Tumaini mzaliwa wa Muleba Nshamba Kijiji Bugarama ambaye ametangaza nia yake ya kugombea jimbo la Muleba Kusini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM



Kaka Mc Baraka pole na majukumu ya kuhabarisha Umma,Kwa jina Naitwa Steven Thomas Tumaini natangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Muleba Kusini kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi CCM 2015,Nia yangu nikuinua vijana kibiashara na kuwajali wazee. Shule ,kilimo na international business opportunity. Hatua za masomo ;Primary Kagondo B 1986-87na Burigi Ngote 1987-93 Wilaya ya Muleba. Secondary Nyakato Bukoba 1994-1998. High level Kishoju sec 1999-2001. Diploma in Business ADM Cambridge UK 2004-2005.Degree Enterprenuer 2007-2010 Birmingham Univercity UK. Masters degree in Marketing Manamegement Birmingham city university 2010-2011. Mali juice Muleba driver and sales man. Marketing Manager Tesco Uk, Transport Manager Ocean link , Regional Business Manager Kilimo Markets ltd.
NAAMBATANISHA CV: 

Steven Thomas Tumaini

P.o. Box 4 Muleba Kagera

Tanzania

Mobile: +255653754499 or +255759576433


Personal Statement

I have high impact on Business executive offering diverse track records and have managed to build brand recognition and sales momentum in business. I have managed to offer an exceptional customer service with my team. Excellent marketing and sales strategies plan in the industry with well known brand Virgin Media United Kingdom, Tesco and Kilimo Markets Tanzania.

Area of expertise

Brand strategy, Sales Logistic, Marketing products, global marketing strategy, strategic planning and execution, channel strategy, brand recognition, budget & cost control, forecasting and market research /customer insight and new products development.

Professional experience

September 2013-up to date

 Regional Business manager Kilimo Markets LTD

Sales and Marketing consultant, Quality control, brand strategy, marketing training & Development Quality control, branding, internal and external customer publicity, Management and coordinating KM activities within the Farmer Marketing Association (FMAs) target business.

January 2013-Augost 2013

Marketing manager Farm Africa Babati region

Core job description is to monitor and to control product quality, Value chain training, Market linkage trainee, and monitor and supervise small and large farm project, supervise seed branding, marketing and control supply chain to small and large Agro-dealers, transport management and logistic plan to support plans deployment on budget requirements. To develop logistic contingency plans while formulating standards operating procedure including materials and personnel.

Jun 2007 - 2012  Branch Brand manager TESCO PLC UK

Managing products and marketing strategies for services and product at this £1.3 million generated in five stores. Team leader in developing and implementing pricing strategy, I also conducted in-depth analysis on new and existing market trends.

Sample contribution

  • Launched Gorilla attack marketing campaign to combat competitive pressure and we generated income and new market channel obtained.
  • Assisting customers with enquiries, marketing plan, product trend
  • In the same period new sales strategy were introduced e.g. new product development
  • Contact with suppliers and managing inventory.



March 2003 – Nov 2006 Marketing & Sales Manager Muleba Agriculture and Local Industry (MALI)

Working with Muleba farmers in various value chains which created  brand identity that positioned the company (MALI) juice on the stage to breakeven point and strengthens the company on the position to compete with other competitors.   

Sample contribution

  • Dealing with suppliers chain and purchasing

·         Served as a leader in the developing of non-chemical juice and market research for Kagera region(value addition)

  • Launched trade show and conducted farmers day known as (Nane Nane) for the first time in Muleba district.
  • Launched campaign to encourage farmers to sale only organic fruits to the industry.

Additional professional background

Base line survey with Professor Kamanzi and Market research in Kagera and Mwanza region.

Education Affiliation

2010 to 2011      Masters (MSc) Marketing Management Birmingham City University

2009 to 2010      BA Enterprise (Hons) University of Birmingham

2007 to 2009      Businesses & Management (HND) South Birmingham College

2007 to 2009      Baccalaureate in Marketing Administration (BMA) Cambridge College

2005 to 2006     Diploma in Business Management Administration Cambridge College



Other Short Courses

Jan 2009               Prince’s Trust; Management in Business plan, Marketing, Sales &financial resources

Nov 2009              Advanced Business studies in presentation, Negotiation technique, Sales and Marketing

May 2007             Biohazard and Sewage Awareness

Jun 2007               Protection of Vulnerable adults

Jun 2007               Health and Safety

Jun 2007               Appointed Persons First Aid

Dec 2004               Base line survey



Hobbies and Interests:  Football, Cooking and Gym



References:



  1. Nelly Nicolas (HR)

Virgin Atlantic UK

Apartment 3, Harvest Fields

Harvest Road B65 AB United Kingdom

Mob-+447445831773



  1. Mr Edmond .J. Ringo (C.E.O)

Match Maker Associates Limited

Private Sector Development Consultants

PO Box 5172, Dar es Salaam, Tanzania

Mob-0754403204





  1. Mr Telesphory Gama (Director)

MALI Juice Industry Muleba

P.O.Box 4-Muleba

Mob-0754758818

TAFITI ZA KUFANYIWA TAFITI

$
0
0

NA PRUDENCE KARUGENDO
IMEKUWA  kawaida kujitokeza taassisi mbalimbali zinazojifanya kuendesha tafiti kuhusu hali ya kisiasa hapa nchini wakati wa uchaguzi mkuu. Mara nyingi,  kama sio mara zote,  tafiti zinazofanywa zinalenga kutoa mwelekeo wa uchaguzi utakavyokuwa kwa maana ya ni mtu gani au chama gani kilicho kwenye mwelekeo wa kushinda uchaguzi.
Jinsi inavyoonekana tafiti hizi zinalenga kushawishi, kwa namna ya kampeni, badala ya kutoa mwelekeo wa halihalisi ilivyo. Katika kufanya hivyo tafiti hizi zinaonekana kuwapigia “debe” baadhi ya watu au vyama vya siasa kwa kuonyesha kuwa ndio au ndivyo vinavyopendelewa na wananchi walio wengi ambao ndio watakaofanya uamuzi katika uchaguzi mkuu unaokuja.
Mimi nadhani ipo haja ya kuzifanyia tafiti hizi taasisi zinazojitokeza kila uchaguzi mkuu unapokaribia. Nazo zifanyiwe utafiti ili kujua malengo yake na walio nyuma ya hizi taasisi za utafiti kutokana na tafiti zake mara nyingi  kuwa za utata.
Mfano katika Tanzania hakuhitajiki sayansi kubwa ili kujua nani atashinda hasa katika ngazi ya urais kulingana na hali halisi tuliyoizoea inayotokana  na sababu zilizo wazi.
Mojawapo ya sababu hizo ni kwamba uchaguzi wenyewe kwa hapa Tanzania haujakaa kisayansi kiasi cha kuufanya utoe picha halisi ya matakwa ya wapiga kura. Katika mazingira hayo ni vigumu kujitokeza mtu na kudai ametumia mbinu za kisayansi na kujua ni mtu gani anaweza kushinda au chama kipi kinaweza kushinda kwa maana halisi ya matakwa ya wananchi.
Mfano Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi zinazoitwa za dunia ya tatu, ambako uchaguzi unafanywa tu kutimiza mazoea ili ionekane kwamba viongozi wa nchi husika wanatokana na matakwa ya wananchi, haijataka kuwa na vifaa vya kisasa vya kufanyia uchaguzi tangu kwenye ngazi ya uandikishaji wa wapiga kura. Na hilo sio jambo ambalo linaweza kuchukuliwa kama uduni wa nchi wa kutoweza kumudu vifaa vya aina hiyo, la hasha.
Tunayo mambo mengi ambayo wakati mwingine yanayazidi hata ya nchi zilizo na uwezo zaidi ya nchi yetu, japo mambo yenyewe si muhimu kama lilivyo suala hilo la vifaa vya kufanyia uchaguzi.
Mfano rais wetu anayo ndege ya kusafiria ya kisasa na ya gharama kubwa sana,  wakati waziri mkuu wa Uingereza anatumia ndege za abiria wa kawaida anapotaka kusafiri! Ikumbukwe nchi yetu inajiendesha kwa kutegemea zaidi hisani ya Uingereza na nchi za aina hiyo.
Lakini pamoja na kuonyesha ufahari wa namna ya kumtunza kiongozi wetu mkuu kuliko wanavyofanya Wangereza, bado nchi yetu inaona ugumu wa kumwezesha mwananchi kuonyesha matakwa yake halisi kwa kisingizio cha ufukara!
Tunabaki kufanya uchaguzi kwa njia za kubahatisha bila ya uhakika wa ni namna gani mtu anaweza kuthibitisha matakwa yake, kamchagua nani na kumuacha nani. Sababu vifaa vya kutupatia uhakika huo hatuna. Katika mazingira ya aina hiyo ambayo mpiga kura hawezi kuwa na uhakika kama alichokikubali ndicho kilichoonyeshwa mtu wa pembeni anawezaje kutafiti mpaka akajua mpiga kura atamtaka nani na kumuacha nani?
Fikiria katika mazingira ambayo idadi ya wanaojitokeza kupiga kura wakati mwingine haifiki nusu ya waliojiandikisha kupiga kura, inawezekanaje mtu atafiti na kutoa mwelekeo wa uchaguzi ulio sahihi?
Mara nyingi tumeshuhudia matokeo ya kura yakichezewa kadri ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wanavyotaka, kitu ambacho hakitoi taswira ya kweli ya uchaguzi husika. Tumeona aliyeshinda akionekana ameshindwa na aliyeshindwa akionekana ndiye kashinda! Hiyo ni  kutokana na kutokuwa na vifaa vya kuzuia uovu wa aina hiyo!
Hizo ni kura halisi za uchaguzi unaofanyika chini ya usimamizi na ulinzi, inawezekanaje sasa utafiti usio na usimamizi wala ulinzi ndio utoe matokeo yaliyo sahihi kiasi cha wananchi kukubaliana nayo kuwa ni ya kweli?
Kitu kingine kilicho kigumu katika kuzifanya tafiti hizi zisiaminike ni mazoea waliyo nayo Watanzania ya kutofanya tathimini kabla ya kufanya maamuzi. Kwahiyo ugumu unakuwa kwamba huwezi kujua mtu ambaye hafanyi tathimini ataamua nini kesho baada ya leo kuonyesha msimamo fulani. Watanzania walio wengi wamezoea kufanya maamuzi kwa kitu kilichowafurahisha kwa wakati huo na dakika hiyo, hata kama kitu chenyewe hakionyeshe mustakabali wa siku kumi zijazo!
Mfano mwaka 2005 Watanzania walitokea kumpenda Kikwete aliyeonyesha mvuto wa aina yake, naye kwa kuutumia mvuto huo aliokuwa nao kwa wananchi akawapa wananchi ahadi za ajabu akimalizia na maisha bora kwa kila mwananchi, hiyo ilikuwa zawadi aliyowapa wananchi waliotokea kumkubali kwa wingi. Na kweli,  kwenye uchaguzi mkuu akapata ushindi wa kishindo ambao wengine walisema ni wa kimbunga.
Lakini  baada ya miaka 5 hatukuyaona maisha bora kwa kila mwananchi. Kikwete akaongezewa miaka mingine mitano japo kwa kusuasua, yeye akazidi kuwapa matumaini wananchi kwa kuongeza ahadi, mpaka sasa anapoelekea kumaliza miaka 10 ya kipindi chake cha kukaa Ikulu ni mafanikio gani yanayoweza yakaakisi mvuto  aliokuwa nao kwa Watanzania? Je, ni kweli kila Mtanzania anayo maisha bora yaliyoahidiwa?
Baada ya kuangalia namna Watanzania walivyo wagumu kufanyiwa tafiti zinazoonyesha msimamo na mwelekeo wao kisiasa,  sasa tuangalie namna tafiti zenyewe zinavyofanyika.
Maranyingi tafiti hizi zinatoa takwimu ambazo zinaonekana ni za kubuni au kuhisi, sababu hazionyeshi zilikofanyikia. Kila mtu anaweza kujiuliza ni lini amewaona watafiti wakimuuliza kuhusu masuala ya uchaguzi kwamba ni chama gani au mtu gani anayetaka kumpigia kura. Kama hakuna aliyewaona tuseme hizo tafiti zao wanazifanyia wapi?
Hii inaweza kutuleta kwenye hitimisho la kwamba tafiti hizi zina malengo fulani kwa watu au vikundi fulani ikiwa ni njia mojawapo ya kuwashawishi wananchi wavifikirie vikundi hivyo au watu hao kwa maana kwamba ndivyo,  au ndio,  walio kwenye uwezekano wa kukubalika. Hizo ni kama njama tu kwa mtazamo wangu. Tafiti za kinjama.
Utafiti kuhusu matakwa na maamuzi ya Watanzania ni vigumu kufanyika katika hali ya sasa waliyomo Watanzania. Hii ni hali ya kubahatisha tu ambapo mambo hayawekwi wazi kwa makusudi mazima kwa hofu ya uwazi huo kuleta matokeo yasiyopendeza kwa baadhi ya watu. Kwa mantiki hiyo ni lazima matokeo yanayopatikana kwenye tafiti hizo yawe ya kubahatisha vilevile ambayo hayapaswi kutiliwa maanani.
Kinachoshadidia mawazo yangu haya ni kama hiki; niliamua kufanya utafiti binafsi katika maeneo ya vijijini ambako watu hawajali suala la kutathimini mambo, nikawapata watu kama 100 na kuwauliza ni chama gani wanakitaka kati ya CCM na Chadema,  wakanijibu tofauti na swali langu lilivyokuwa. Wao walisema wana kiu, kama nataka kuuliza maswali yangu kwanza niwapoze kiu. Nikajitutmua na kuwapa kinywaji.
Baada ya kupata kinywaji wakawa wanatafuta jibu la kunifurahisha, nao wakaniuliza, kwani wewe ni chama gani? Nikawajibu CCM, wakacheka na kusema sasa unawezaje kutuuliza habari ya Chadema wakati unaelewa kuwa hapa miaka nendarudi sisi tunaijua CCM tu? Nilipowambia kuwa huu ni wakati wa vyama vingi vya siasa na nimeishahamia Chadema papo hapo wote wakageuka wakawa Chadema, wakisema walikuwa wananipima tu!
Kwa mtindo huo umawezaje kusema umefanya utafiti na kujua ni chama gani au mtu gani anayekubalika kwa wananchi wa aina hiyo?
Tafiti za aina hiyo zinafanyika na kufanikiwa katika nchi ambazo chaguzi zinaakisi matakwa halisi ya wapiga kura. Kama tunataka kuziiga tafiti hizo basi tuanze kuiga namna ya kufanya kitu cha kweli, kwa maana ya kuhakikisha kwamba matakwa ya wananchi yanakuwa ya kweli bila kupindishwa.
Mfano wa wazi ni wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.  Katika mkoa wa Dar es salaam wananchi walikuwa wamedhihirisha kukikubali chama cha upinzani cha NCCR- Mageuzi. Ikaonekana kwamba majimbo yote ya Dar es salaam yangekwenda kwa chama hicho. Kilichofuatia ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuuvuruga kwa makusudi uchaguzi katika mkoa wa Dar es salaam na baadaye kutangaza kuwa utarudiwa baada ya muda fulani. Uliporudiwa mambo yakabadilika!
Sababu zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi hazikuwa na pahala pa mashiko. Sababu haiwezekani uchaguzi ukaenda vizuri sehemu za Karagwe, mpakani mwa Tanzania na Uganda na Rwanda, zaidi ya kilometa 1500 toka makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, halafu uchaguzi huohuo uvurugike kwa kutotimia vifaa vya uchaguzi maeneo ya Mtaa wa Shabani Robert, hatua chache toka ofisi za Tume ya Uchaguzi.
Nihitimishe kwa kusema kwamba tafiti hizi kuhusu uchaguzi zingekoma kuliko kuendelea kuwapotosha wananchi kwa kuwaelekeza na kuwashawishi namna ya kufanya uchaguzi. Wananchi waachwe wachague wanavyoona wao inafaa kwa sababu mambo yote ni ya kubahatisha tu.
0784 989 512



BALOZI KAMALA AWEKA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA JAMHURI YA VANUATU UBELGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka saini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Vanuatu. Vanuatu imekumbwa na kimbunga kilichosababish uharibifu wa miundombinu na mamia ya watu kupoteza maisha.

DIAMOND PLATNUMZ NI KIOO CHA WASANII KATIKA JAMII YETU

$
0
0
NA PRUDENCE KARUGENDO
MKOA  wa Kigoma ni hazina kubwa ya vipaji hapa nchini Tanzania. Tangu zamani kulishuhudiwa vipaji vingi toka mkoani humo hasa vya wanamichezo na wasanii. Mfano kwa upande wa kandanda tutaona kwamba mkoa huo ulitingisha sana kwa vipaji vya wanasoka.
Kina Manara, Kitwana Manara, Sunday Manara, Kassim Manara na ndugu zao wengine wanatoka Kigoma. Baadaye kikafuatia kizazi cha kina Edbili Lunyamilla, Nteze John, Omari Mavumbi, Itutu Kigi na wengineo wengi.
Kwa upande wa wasanii wa muziki Kigoma imetoa watu wengi wenye majina makubwa katika sanaa hiyo,  kama Shem Kalenga, Hassan Rehan Bitchuka, Marijani Rajabu, Zahir Ally Zorro, Banana Zorro, Wema Abdallah, Nyota Waziri na wengineo wengi.
Kwa upande wa muziki wa kizazi kipya Kigoma imefanya kufuru. Imetoa vijana wengi wa muziki huo wakiongozwa na mtaalamu wa muziki, kwa maana ya kutunga, kuimba, kucheza kila ala ya muziki na kutengeneza muziki, Emmanuel Bizimana Ntavyo, maarufu kimziki kama Bizman. Vilevile wapo wengine wengi wa muziki wa kizazi kipya, kama kina Ally Kiba, Banana Zorro, Jacqueline Ntuyabaliwe, maarufu kama K-Lynn na wengine wengi.
Lakini pamoja na wote hao makala hii ni mahususi kwa moja ya vipaji hivyo vya mkoa wa Kigoma ikiwa imemlenga chiriku wa muziki wa kizazi kipya kwa sasa hapa nchini, Nassibu Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz.
Diamond kadhihirisha kipaji cha sanaa ya muziki kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa kipindi cha muda mfupi alioutumia katika sanaa hiyo. Naweza kusema kwamba ni kipindi kisichozidi miaka mitatu. Hiyo ni tofauti na kipindi alichokitumia mfalme wa muzuki wa pop duniani, Michael Jackson, kuwa kileleni mwa mafanikio. Michael Jackson alitumia zaidi ya miaka kumi kufika kileleni, kati ya 1967 – 1979.
Lakini ndani ya miaka mitatu Diamond ameweza kuibeba Tanzania na kuiweka kwenye chati ya kimataifa kwenye fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya. Na ninaposema ngazi ya kimataifa sina maana ya kuvuka tu mipaka ya nchi na kuingia nchi za jirani kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi, Msumbiji wala Kongo, kama ambavyo wameweza kufanya wasanii wengine wa muziki huo wa hapa nchini, ninamaanisha kimataifa kwa maana halisi. Nalenga nchi za mbali na Tanzania.
Muziki wa Diamond kwa sasa unapigwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika kuanzia Afrika Kusini, Afrika ya Kati, Mashariki na Afrika Magharibi, ukiondoa nchi za Kiarabu kwa upande wa Afrika Kaskazini, ambako sina uhakika kama muziki wa kizazi kipya una mashabiki kulingana na utamaduni wa Kiarabu ulivyo.
Kwa maana hiyo Diamond kaiweka Tanzania kwenye chati ya kimataifa kwa maana halisi kimuziki. Kwa  sasa msanii huyo anakula sahani moja na wasanii wa kimataifa kama kina Peter Okoye na Paul Okoye, Wanigeria wanaounda kikundi cha P Square, ambao mara kadhaa wamemuomba watoe naye vibao vya pamoja. Pia yuko kwenye kiwango cha wanamuziki kama Youssou N’Ndour wa Senegal na wengine wa aina hiyo.
Kwa eneo hili la Afrika Mashariki, nashindwa kumtofautisha Diamond na mwanamuziki wa Uganda, Joseph Mayanja, maarufu kama Chameleone. Kwa sasa wanamuzi hao wanafanana kwa kwa mambo kadhaa nitakayoyajadili hapa chini.
Tanzania iliwahi kuvuma sana duniani miaka ya nyuma kupitia kwa wanamichezo, hususan wanariadha, kina Filbert Bayi, aliyewahi kuwa bingwa wa mbio za mita 1500 duniani, ambaye mpaka sasa anashikilia rekodi ya mbio hizo kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola aliyoiweka mjini Christchurch nchini New Zealand mwaka 1974. Wengine ni Seleman Nyambui, Adventina Mtakyawa, Juma Ikangaa, Gidmas Shahanga na wengine wengi.
Lakini kutokana na umri kuwatupa mkono nyota hao,  jina la Tanzania limefifia katika tasinia ya michezo na kuifanya nchi yetu isahaulike kabisa kana kwamba haipo kwenye nyanja ya michezo na burdani!
Hivyo Diamond ni kijana aliyedhamiria kulipandisha tena jina la nchi yake kupitia tasinia ya burdani. Na niseme kwa uhakika kabisa kwamba ameweza. Hilo linashadidiwa na tuzo mbalimbali za kimataifa anazozipata kwa sasa kwa upande huo wa burdani baada ya kushindanishwa na wasanii wengine wa kimataifa toka nchi mbalimbali.
Kitu cha kipekee nilichokigundua kwa Diamond na kuhisi kwamba pengine ndicho kinachochochea mafanikio yake ni tabia yake ya kusikiliza ushauri na kuufanyia kazi.
Wakati fulani nilimpa changamoto, ambayo vilevile niliwahi kuitoa kwa Joseph Mayanja (Chameleone) wa Uganda nilipokutana naye Jijini Mwanza, Mei mwaka jana, kwamba kwa kiwango alichopo hapaswi kuendelea kuimba muziki kwa kutumia mtindo wa “play back”, kwa maana ya kuimba kwa kufuatiza muziki uliorekeodiwa tayari,  kwamba anatakiwa kuwa na vyombo vyake na kupiga muziki wa moja kwamoja pasipo kutumia CD. Diamond kanielewa na kusema kwamba hilo analifanyia kazi kwa bidii kubwa.
Kitu kingine ni namna anavyoendesha mahusiano na jamii aliyomo. Kawaida kuna dhana ya kwamba wasanii ni watu wasioeleweka vizuri ndani ya jamii, wahuni, na huo kuwa mwanzo wa neno usanii, kwamba fulani kanifanyia usanii ikiwa na maana ya kanifanyia uhuni.
Lakini hilo ni tofauti kabisa kwa Diamond. Yeye anapenda sana kuwasaidia wenye mahitaji kulingana na hali halisi ilivyo. Kipindi fulani kwa mfano, kwa kuuthamini mchango wa Baba wa Muziki hapa nchini, Marehemu Muhidini Mwalimu Gurumo, aliamua kumpatia msaada wa gari jipya. Huo ni usanii kwa upande wa pili anaouonyesha Diamond tofauti na upande uliozoeleka kwa jamii.
Diamond anasema kwamba amejipangia kila mwezi kuwa anatembelea vituo vya watoto yatima na kutoa misaada mbalimbali kadri inavyowezekana. Huo ni mchango mwingine katika jamii anaoufanya kijana huyo.
Anawashauri vijana wenzake, hasa wasanii, wanaojiingiza kwenye ulevi uliopindukia pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya waache mambo hayo mara moja. Anasema kwamba mambo hayo yanaharibu vipaji na wakati mwingine kusababisha kupoteza maisha. Anasema ili kukilinda kipaji chake yeye anahakikisha anaepukana na mambo hayo yasiyo na maana na yaliyo hatari kwa maisha ya binadamu.
Diamond anasema kwamba alizaliwa Septemba 22, 1990, Kigoma, na kwamba kabila lake ni Mmanyema.
Anasema kwamba kilichomfanya aingie kwenye muziki ni kipaji chake kilichojitokeza tangu akiwa shule ya msingi. Eti alikuwa akipendelea kuimba kwenye kwaya ya shule na burdani nyingine za shuleni.
Huyo ndiye Nassibu Abdul, au ukipenda Diamond Platnumz, ambaye wasanii wengine vijana wanapaswa wamtumie kama kipimo ya mafanikio katika usanii huo wa muziki wa kizazi kipya wanaoufanya. Bilashaka watakaofuata mwenendo wake watafanikiwa kama yeye alivyo.
0784 989 512

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA BRUSSELS AIRLINE

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa kampuni ya Brussels Airline Mhe. David Lyssens (kulia) baada ya kumaliza kikao naye ofisini kwake Brussels. Kushoto ni Bwana Geoffrey Kabakaki Mchumi Mhandamizi Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. Balozi Kamala ameiomba kampuni hiyo kuingia kwenye biashara ya usafiri wa anga Tanzania.

SHUGHULI YA KITCHEN PARTY (MJUBURO) WA BIBIE RUKIA NADHIR RAJABU KUFANYIKA TAR 19/4/2015 KATIKA YA UKUMBI WA LINAS

$
0
0
Mama Amina Sued Kagasheki wa Mtaa wa Twiga (Bilele ) Mjini hapa anapenda kuwafahamisha na kuwaalika ndugu , majirani na marafiki wa familia yake kushiriki katika Shughuli ya kumfunda,kumzawadia na kumuelimisha binti yake kitinda mimba (pichani) Omwana Rukia. Shughuli hiyo inatalajiwa kufanyika tarehe 19/4/2015 katika ukumbi wa Linas Night Club Nyote mnakaribishwa!!
Viewing all 4222 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>