Kukamilika na kukabidhiwa kwa daraja la kimataifa la Rusumo mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda kutainua uchumi wa mkoa wa Kagera kwa kutoa fursa zaidi za kibiashara kati za Rwanda, Kongo DRC na Tanzania kwa kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Aidha John Mongella aliishukuru serikali ya Japani kupitia shirika lake la maendeleo JICA kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hasa miundombinu. Vile vile alisema kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kati yake na Nchi ya Japani ili kuleta maendelo ya kiuchumi na ya haraka.
Uzinduzi wa Daraja Rusumo Utepe Ukikatwa
Mara baada ya Kukata Utepe Daraja Likitembelewa
Daraja hilo la kimataifa la Rusumo lilikabidhiwa rasmi kwa serikali za Tanzania na Rwanda tarehe 10 Januari, 2015 na Rais wa shirika la maendeleo la Japani JICA Dk. Akihiko Tanaka katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mpakani mwa Tanzania na Rwanda Rusumo baada ya ya JICA kukamilisha daraja hilo.
Akikabidhi rasmi daraja hilo la Rusumo Dk. Tanaka alisema lengo la serikali ya Japani kupitia JICA kutoa takribani Dollar billion 6.5 za Kimarekani kujenga Daraja la Kimataifa la Rusumo na kituo cha umoja wa forodha ni kutaka kuunganisha nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa miundombinu iliyo imara itakayoziunganisha nchi za Afrika kwa maendeleo zaidi.
Dk. Tanaka alisema kuwa maendeleo ya Afrika yatakuwepo iwapo Afrika itakuwa na miundombinu imara inayoziunganisha nchi zote ili shughuli za kiuchumi ziweze kufanyika kwa wepesi zaidi na kuleta tija zaidi katika maendeleo ya nchi moja moja na bara zima kwa ujumla.
Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella akimwakilisha Waziri wa Ujenzi John Magufuli katika hafla hiyo aliishukuru Serikali ya Japani kupitia JICA kukamilisha ujenzi wa daraja la Kimataifa la Rusumo kuwa daraja hilo litatoa fursa zaidi za kufanya biashara kati ya nchi ya Tanzania, Rwanda na Kongo DRC.
Pichani muonekano wa Daraja la Zamani.Aidha John Mongella aliishukuru serikali ya Japani kupitia shirika lake la maendeleo JICA kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hasa miundombinu. Vile vile alisema kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kati yake na Nchi ya Japani ili kuleta maendelo ya kiuchumi na ya haraka.
Kwa upande wa nchi ya Rwanda iliyowakilishwa na Waziri wa Miundombinu Bw. James Musoni alisema kukamilika kwa daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha umoja wa forodha ni fursa kwa Wanyarwnda kufanya biashara zaidi na kukuza uchumi wa nchi yao kwa kupunguza muda wa kukaa mpakani kwa ajili ya kushughulikia masuala ya ushuru.
Pia Waziri Musoni alisema kuwa daraja la Rusumo ni tegemeo kubwa kwa nchi yao kwani Nchi ya Rwanda haina Bandari na wanategemea sana bandari ya Dar es Salaam katika kupitisha mizigo yao na kuisafirisha kupitia mpaka wa Rusumo.
Eneo la Mto Kagera na Daraja la RusumoUzinduzi wa Daraja Rusumo Utepe Ukikatwa
Mara baada ya Kukata Utepe Daraja Likitembelewa