Mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA.
Hii ni kwa kujibu wa tweet ya East Africa Radio
Kupitia taarifa zilizosambaa kuhusu kufukuzwa kwa Zitto Kambwe uanachama CHADEMA, mwanasheria wake Albert Msando kaandika kupitia Instagram taarifa hii..
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA.
Hii ni kwa kujibu wa tweet ya East Africa Radio
Wakati tukiendelea kusubiri taarifa kamili, hiki ndicho alichokisema mwanasheria wa Zitto Kabwe.

Taarifa kuhusu maamuzi ya Mahakama Kuu leo tumezipata kupitia mitandao ya kijamii kwa sababu kesi awali ilikuwa imepangwa tarehe 12.03.2015 lakini inaonekana kwenye rekodi imerudishwa nyuma na maamuzi hayo kusomwa leo bila sisi kuwa na taarifa. Tunafanya utaratibu tupate nakala ya maamuzi hayo ili kujua nini cha kufanya. Hatuna taarifa rasmi ya kufukuzwa Mh. Zitto Kabwe uanachama. Taratibu zote zitafuatwa pindi tukipokea taarifa rasmi kutoka mahakamani na kwenye chama. Ni matumaini yetu jambo hili halitaendeleza chuki zisizokuwa na sababu au kujenga kati ya wahusika. #Demokrasia #Haki #UtawalaBora #Taratibu