Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4177

PROF TIBAIJUKA ACHANGIA MIL 60 KUKUZA MITAJI YA WANAWAKE JIMBONI MWAKE

$
0
0
Zaidi ya vikundi 500 vya wajasiliamali kutoka kata 17 kati ya 25 zinazounda jimbo la Muleba Kusini Mkoani Kagera vimepokea mchango wa Sh 60 milioni kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo kwa lengo la kuboresha mitaji na kujipanua kiuchumi
Akihutubia  wawakilishi wa vikundi hivyo jana  katika ukumbi wa Kajumulo Foundation mjini Muleba mbunge wa jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka amesema vikundi alivyochangia fedha hizo ni vya wanawake , Vijana pamoja na  wazee
Profesa Tibaijuka amesema kuwa vikundi hivyo ni vile vilivyopata usajili kupitia idara ya ushirika wilayani humo na kutimiza masharti ya kuanzishwa vikundi vya ujasiliamali hivyo anaviongezea mitaji viweze kupanuka na kujipatia maendeleo.

Aidha amesema katika ziara yake ya Mwezi Machi hadi April  kuzungukia wapiga kura alikabidhiwa risala za vikundi hivyo kwa kutajiwa changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mitaji, elimu ya ujasiliamali  pamoja na kukosa masoko.
“Wananchama  wa vikundi hivyo hawana budi kuwa wabunifu katika kuendesha vikundi hivyo ambapo halmashauri ya wilaya iendelee kutafuta fedha kutoka vyanzo vya ndani kusaidia vikundi vya vijana na wanawake”Alisema Tibaijuka
Viongozi wa vikundi wamepongeza kuhusu juhudi za mbunge huyo ambaye hakubagua jografia ya jimbo hilo kwani kahusisha kuchangia vikundi hata vile vilivyoko  visiwani ambavyo wajumbe wake wanaishi mazingira magumu
Kwa upande wake diwani wa kata ya Gwanseli (CUF) Julius Rwakyendela amesema kuchangia vikundi hivyo ni wajibu wake na kwamba alichelewa kuwakumbuka wananchi labda ni  kwa nafasi aliyokuwa nayo ya uwaziri.
Amesema katika kata yake amechangia kikundi cha vijana wanaotengeneza barabara kwa mikono ambayo alipita na kushindwa kufikia baadhi ya vijiji kutokana na miundombinu hafifu ya  kuharakisha maendeleo ya kijamii.
Pamoja na hayo Mwenyekiti wa CCM wilayani Muleba Muhaji Bushako ambaye ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Muleba Kusini amebeza uchangiaji wa vikundi akidai ni takrima ya kutaka  kujisafisha kwa wapiga kura
Bushako amesema kinachofanyika ni kujinadi kwa kila kijiji kuendelea kuwatumikia wana jimbo lakini muda wake ameupoteza akiwa Waziri na kufanya zaidi shughuli za kitaifa akiwasahau  wapiga kura aliowawakilisha bungeni

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4177

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>