Matukio ya picha yaliyojiri katika hafla fupi iliyo andaliwa na Familia ya Mwl.Philbert F. Byabato wa Kijijini Gera kwa ajili ya kumpongeza mwanafamilia wao Mwl. Pelagia Philbert ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma baada ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake na miaka 40 ya Utumishi.
Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Ibada iliyoongozwa na Fr. Godwin Rugambwa pichani imefanyika Nyumbani kwao Kijijini Kashambya -Gera mwanzoni Jumatatu ya Pasaka March 28,2016.
Wakati Ibada ikiendelea Baadhi ya waalikwa wakishiriki Ibada hiyo iliyofanyika Nyumbani kwa Familia ya Mwl.Philbert F. Byabato Kijijini Kashambya -Gera mwanzoni Jumatatu ya Pasaka March 28,2016.
Mara ya baada ya Ibada inafuata ratiba ya Waalikwa kupata chakula na Vinywaji
Baadhi ya wanafunzi waliopita mikononi mwa Mwl. Pelagia Philbert
Neno la shukrani kutoka kwa Mwl. Pelagia Philbert pichani ambaye amebahatika kustaafu utumishi wa Umma baada ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake na miaka 40 ya Utumishi.
Mwijilist akitoa Somo
Mdau Paul Rwechungura pichani kushoto ambaye ni rafiki wa familia akisalimia na Mwl.Philbert F. Byabato mwenyeji wa familia hii