Ndugu Murshid Hassan Byeyombo
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Maruk Vanilla Farming and Processing Ltd
Ndugu Wadau,
Kwa niaba ya Wakurugenzi wa Maruk Vanilla Farming and Processing (MVFP) Ltd nawatakia mwaka mpya wenye heri na mafanikio katika mipango yenu. Sisi kama MVFP Ltd tunawaahidi kuendeleza gurudumu la ukombozi wa Mkulima wa Vanilla na mazao mengine ya Biashara hasa viungo (spices).
Mwishoni mwa mwaka jana tulianzisha mpango maalumu wa kuongeza uzalishaji wa zao la vanilla kwa kugawa marando (vines) mapya. Pia tuliweza kuanza ushamirishaji wa mazao mbadala ya Biashara mkoani mwetu. Tumeweza kugawa zaidi ya miche 7500 ya vanilla na miche 800 ya pilipilimanga (black pepper) yote kwa wakulima wapya. Mpango huu umeonyesha kuitikiwa vema na wakulima hivyo mwaka 2014 tutazidisha jitihada.
Mwaka huu tayari tumezindua huduma ya MALIPO YA AWALI KWA WAKULIMA WENYE DHARURA. Huduma hii ni maalumu kuwakwamua wakulima wa vanilla kifedha wakati wakisubiri mavuno na mauzo ya mazao yao. Dharura zitakazo hudumiwa ni zile zinazohusiana na Elimu na Afya kwa wanafamilia wa mkulima wa vanilla. Tunatarajia kupanua mkondo mmoja wa huduma hii kufikia kuwa huduma kamili ya Bima ya Afya kwa Wakulima.
Kama ilivyo ada, msimu wa mwaka huu 2014 MVFP Ltd itaendeleza sera yake ya manunuzi ya vanilla kwa mkulima ambayo wakulima hulipwa papo kwa papo pesa taslimu mara tu wanapofikisha mazao yao kwenye kituo cha manunuzi. Tunaheshimu utaratibu huu kwani tunatambua kuwa mkulima anauza mazao yake ili kujikomboa na kukidhi mahitaji mbalimbali. Kwa kuwa mahitaji na shida zake hazisubiri baadae, hivyo malipo kufanyika muda kitambo baada ya mauzo ni kumfanya mkulima ashindwe kutimiza haja zake. Na hatma yake wakulima huacha kuhudumia mashamba, hung’oa miche na kulichukia zao.
Kuna kila dalili kwamba bei ya mapodo itapanda na hivyo kumfanya mkulima apate malipo mazuri. MVFP Ltd tunazidi kuwasisitiza wakulima kuongeza uzalishaji na kujali miche yao. Pia tunaishauri serikali na wadau wa maendeleo kumulika zao hili la vanilla. Tuna imani kwamba vanilla ina uwezo mkubwa wa kubadili maisha ya wakulima iwapo itapata msukumo stahili kutoka kwa wafanya maamuzi na watendaji wa vyombo vya umma.
Mwisho tunapenda kuwashukuru na kuwapongeza wamiliki na waendeshaji wa http://bukobawadau.blogspot.com/kwa kazi nzuri wanayoifanya kuuhabarisha umma juu ya nini kinaendelea nyumbani na duniani. Blog hii imetusaidia kwa njia ya “trickle-down effect”ambapo wale walioko mbali na nyumbani, baada ya kusoma habari zetu hapa, huamasisha walioko nyumbani kujiunga na kilimo cha vanilla. Tunaomba wadau muendelee na moyo huu kwa maendeleo ya watu wetu na Kagera yetu.
Omutwale Innocent Mushaijaki kutoka Ishozi Rutala lakini kwa sasa naishi jijini Dar es salaam na kufanya kazi katika kampuni ya SCANAD kama media monitoring meneger,nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu mpya wa 2014 na pia nasema kwamba TWETOHYE TULEKELE OLWANGO , OKUTENDELANA N'ENOBI.
Finally 2013 Came To An End. Happy New Year For All Of U.As the Year Goes on, You are also get old Before leaving let me Wish you All for You Good Future and full of success as the last year was very challenging but still we belive we can still make it with our life goals as i belive where theirs a will theirs a way,so just axcept the challanges and make sure your playing a right game to achive the success.And also thanks alot mc for updating us withl all the news around the world ,bukoba we are one.Rehena Gulam.