Na mwandishi wetu
Muleba
WATU wanne wamefariki dunia na majeruhi wengine 14 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Nundu-Katoke wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajiri T832 lililokuwa linaendeshwa na bwana Omar Twaha (40) kupinduka na kupotea njia.
Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoani Kagera Agustino Ollomi alisema kuwa tukio hilo lilitokea novemba 07 mwaka majira ya saa 1:10 jioni wakati watu hao walipokuwa wakitoka msibani ndipo walipofika eneo la Nundu katoke kutokana na mwendo kasi lililokuwa nalo gari hilo lilipasuka tail la nyuma la kulia na kuacha kupinduka.
Ollomi aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na Evodius ambaye amekufa papo hapo aliyetambulika kwa jina moja ambaye mwili wake umehifadhiwa katika kituo cha afya Kaigara, Diana Pius aliyefia katika hospitali ya Rubya, Edmundi Fidelis na Renatus Vedasto miili yao imetunzwa katika hospitali ya Kagondo.
Alisema majeruhi watatu hali zao ni mahututi ambao ni Thobias Titus (28) fundi wa vioo Rwamishenyi , Max Hanta (45) na Rweyemamu Frediricki wote wakazi wa Rwamishenyi ambao wamelazwa katika hospitali ya Kagondo na madakitari wanaendelea kuwahudumia ili kuokoa maisha yao na majeruhi wengine kumi na mmoja wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Kagondo.
Kamanda Ollomi aliongeza kuwa , chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na mwendo kasi wa huyo dreva na gari lilipata pancha taili ya nyuma mkono wa kulia na baada ya tukio dreva ametoroka na novemba 08 mwaka huu alikamatwa na atafikishwa mahakamani.
Hapo hapo, Perepetua Julius (32) amekutwa amekufa katika tarafa ya Rulenge wilayani Ngara baada ya kupigwa na kitu kizito kichani.
Aidha Kamanda huyo wa polisi mkoani Kagera Agustino Olomi alieza juu ya tukio hilo na kusema kuwa, marehemu amekutwa amekufa akiwa ametupwa kichakani umbali wa mita 100 kutoka anapoishi.
Aliongeza kuwa , mnamo novemba 04 mwaka huu majira ya saa nne usiku marehemu aliondoka nyumbani kwake hakuonekana tena hadi alipokutwa amepoteza maisha novemba 07 mwaka huu na uchunguzi umebaini kuwa alipigwa kitu kizito kichwani.
Amesema mtu mmoja ambaye ni mume wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Julius Saimon Sengiyunva anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na tukio hilo baada ya kuwepo ugomvi wa muda mrefu baina ya marehemu na mume wake.