Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati za Troika za Mabalozi wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kamati hizo zimekutana leo Brussels kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kulia kwa Balozi Kamala, ni Balozi Mhe. Dimitrious Touloupas Mwenyekiti wa Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya na Mwakilishi wa Ugiriki katika Kamati ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Ulaya.
↧