Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4196

"NIMEMALIZA USAJILI" ASEMA MOURINHO

$
0
0
Boss wa Chelsea, Jose Mourinho amesema amemaliza kununua wachezaji msimu huu baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto Filipe Luis kutoka Atlètico Madrid.
Luis ni mchezaji wa nne mpya kusajiliwa na Mourinhomsimu huu baada ya Cesc Fabregas, Mario Pasalic na Diego Costa.
"Tumefunga biashara leo," amesema Mourinho. "Dirisha la usajili linafungwa Agosti 31, lakini sisi tumefunga Julai 19.
"Klabu yangu imefanya kazi nzuri, sio kwa wachezaji tulionunua tu, lakini pia kwa sababu tumemaliza biashara mapema kabisa."
Chelsea wamekuwa wakihusishwa na wachezaji kadhaa wa bei ghali msimu huu, akiwemo Sami Khedira wa Real Madrid na Radamel Falcao wa Monaco.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4196

Trending Articles