Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live

JK AANDALIWA MAPOKEZI MAKUBWA BAGAMOYO

$
0
0
Na Richard Mwaikenda, Dodoma

MWENYEKITI mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jakaya Kikwete ameandaliwa mapokezi makubwa na wanaCCM wilayani Bagamoyo kesho baada ya kung'atuka wadhifa huo, kwenye Mkutano Mkuu Maalum Dodoma.

Akielezea kuhusu mapokezi hayo mjini Dodoma jana, Katibu Mwenezi wa CCM, Wilaya ya Bagamoyo,Kassim Gogo alisema kuwa mapokezi hayo yataanzia Chalinze hadi Bagamoyo.
Alisema kuwa wanaCCM wa wilaya hiyo wanajisikia furaha sana kuona Jakaya Kikwete ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Msoga, wilayani humo, ameng'atuka salama baada ya kukitumia chama na serikali kwa miaka kumi.
Alisema kuwa jambo lingine linalowapa faraja ya kuandaa mapokezi hayo ni kwamba Jakaya Kikwete ameng'atuka uongozi kwa kukiacha chama salama na nchi ikiwa salama pia.

Gogo, alisema kuwa katika mapokezi hayo watakuwepo madiwani wote wa wilaya hiyo, viongozi wa CCM, wabunge wote wa Mkoa wa Pwani na wananchi. 

Alisema kuwa wakati wa hafla hiyo pia Mwenyekiti mstaafu, Kikwete atakabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kumvisha gwanda ili awe mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani.

Katika sherehe za mapokezi zitakazofanyika mbele ya Makao Makuu ya Ofisi za CCM za wilaya hiyo zilizopo Bagamoyo Mjini, patakuwepo ngoma za asili ya makabila ya Wakwere, Wazaramo na Wazigua pamoja na wasanii mbalimbali pia watatumbuiza.
Alisema kuwa Kikwete akiwa amepumzika baada ya kung'atuka, watapata wasaa wa kuchota hekima na burasa zake ya jinsi ya kukiongoza chama hicho na serikali pia. 


SIMULIZI LETU LEO JUMAPILI JULY 24,2016

$
0
0
Miaka kadhaa iliyopita, hii ilikuwa nyumba ya hadhi ya juu kabisa katika jamii iliyopo hapo. Mmiliki wake alikuwa ni tajiri mno ambae kila mtu angependa kwenda kwake kuomba msaada. Hilo gari lilikuwa kivutio kwa kila mtu katika hiyo jamii. Ilikuwa kama ndoto iliyokuwa kweli baada ya mmiliki kuongeza gari na hiyo nyumba kama vitu anavyovimiliki.
Lakini leo hii, mali zimezeeka na kwa hali ya kawaida ya asili hiyo nyumba itabomolewa na atakuja mtu mwingine mwenye udambwi dambwi wa kutosha akasimamisha mjengo wa maana. Na hilo gari litapelekwa kwa wanunua skrepa.
Mtu atakayeishi kwenye nyumba kama hiyo HIVI SASA, pasina kumkufuru mwenyezi Mungu tunaweza tukamuona huyo mtu yupo katika daraja la chini kabisa la maisha.
Ni nini maana yake?
"Nothing in life is worth fighting for" Nguo yako unayoipenda sana kwa mwingine anaona kama dekio tu nyumbani kwake, akiba yako yote iliyopo benki kwa mwingine hiyo pesa ni ya mchango katika hafla fulani, girlfriend wako/ boyfriend wako/ mchumba wako alikuwa ni x wa mwingine. Kila changudoa unaemuona maeneo ya starehe kuna kipindi alikuwa bikra.
Ni nini maana ya haya yote?
Maisha ni mafupi sana kujihisi kuwa wewe bi bora kuliko mwingine. Steve jobs amewahi kusema "we all naked to death" kwa kiswahili "binadamu wote tu uchi mbele ya kifo" hakuna kitu kitakachotuokoa na kifo. Nimekua nikiona watu wakijikweza kwa utajiri wao. Uzuri wao, elimu zao na umaarufu.
Hakuna kitu ambacho utafanikiwa kukipata ambacho hakuna binadamu mwenzako amewahi kukipata. Kuna kitu kimoja tu ambacho wewe binadamu unapaswa kujivunia nacho. Ambacho ni "MAISHA YA KUMPENDEZA MUNGU" hivyo basi kuwa mwema kwa binadamu wenzako, acha dharau na nyodo. Siku zote Tengeneza marafiki na si maadui.
Kumbuka watu unaowadharau hivi sasa wakati upo juu, kuna kipindi utaanguka na utatamani msaada wao na usiupate. Hivyo basi usiwasababishie matatizo watu wengine kwa maana siku moja watakuja kuwa tatizo kwako. Usiendeshwe na umiliki wako wa mali kwa maana siku moja isiyo na jina mali itatoweka au wewe ndio utatoweka.
Tushikamane, Dunia itakuwa mahala salama pa kuishi kama tutauishi upendo ambao umekuwa ukifundishwa na vitabu vyetu vya dini.
Ni ujumbe wangu wa leo na ninawapenda sana.

Like Share It

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU JULY 2016

$
0
0
 Bila shaka unakumbuka na umepata kutumia sabuni za MAGWAJI kwa kuogea kabla ya Ujio wa sabuni ya Imperial (kutoka Kenya)
Hakika ni changamoto kubwa kwa ndugu zetu huko Vijijini mpaka sasa Sabuni za Magwaji zinatumika,wananchi wanaishi kwa masikitiko sawa na dhama za  kunywa chai iliyochanganywa na pipi badala ya Sukari na kupikia samli ya ng’ombe wetu badala ya mafuta ya kupikia safi yanayotoka nje au yale ya  pamba yetu...!
 Hapa tunakutana na Wauzaji wa mabumunda /Baragala moja inauzwa kwa sarafu ya shilingi 10 tu!
 Hii ni Live kutoka katika Gulio la Jumamosi katika Mji Mdogo wa Nshamba wilayani Muleba.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Ngao katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016

PICHA NA IKULU

MAALIM SEIF KUNGURUMA TENA MAREKANI

$
0
0
Na Mwandishi wetu,  Philladelphia
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anatazamiwa kunguruma tena chini Marekani wiki hii.
Maalim Seif Sharif Hamad  akiwasili katika uwanja wa ndege Philladelphia
Gwiji huyo wa siasa ambaye aliwasili jijini Philladelphia hapo jana, anatarajiwa kuwakhutubia Watanzania katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii katika jiji la Boston.
Katibu huyo Mkuu wa CUF pamoja na ujumbe anaofuatana nao aliwasili nchini humu akitokea Uingereza baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya iliyochukua muda wa zaidi ya wiki moja. 
Akiwa Ulaya Maalim Seif alitembelea Uiengerza na kufanya mikutano na Maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Uingereza, Vyama vya kisisasa na Taasisi mbalimbali. Baadaye alielekea nchini Ubelgiji ambako alifanya ziara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na kufikisha madai ya Wazanzibari ya kurejeshewa haki yao ya Kidemokrasia.
Aidha alitembelea nchini Uholanzi ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na maofisa wa Mahakama ya Ukhalifu ya Kimataifa na kufikisha kilio cha Wazanzibari dhidi ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu unaendelea Visiwani Zanzibar.
Ziara hiyo ya Ulaya ilikuja katika kile maofisa wa CUF walichokielezea kuwa ni awamu ya pili ya ziara za nje za mwanasiasa huyo mkongwe katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa kwa mgogoro wa Kisiasa Zanzibar.
Maalim Seif ambaye anafuatana na Mkuuwa Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CUF Bwana Issa Kheir Hussein, yupo nchini Marekani kuitikia mwaliko wa kuhudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democratic ulioanza jana jijini Philladelphia, mkutano ambao unatazamiwa kumpitisha Bi Hillary Clinton kuwa mgombea wa Urais wa Marekani kwa kuoitia tiketi ya Chama hicho.
Katika mkutano wake wa hadhara na Watanzania, Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, anatazamiwa kuzungumzia zoezi zima la uchaguzi huo uliofutwa, na kusisitza madai ya Chama chake ya kurejeshewa haki yao waliyoporwa katika uchaguzi huo, na mwenendo mzima wa Demokrasia nchini Tanzania.
Itafaa kukumbusha kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kuzuru Marekani katika kipindi cha chini ya miezi miwili. Mwezi uliopita, Maalim Seif alikuwepo nchini humu na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kisiasa na mashirika binafsi, na kutembelea Umoja wa Mataifa ambako alifikisha madai ya Chama chake ya ukandamizaji wa demokrasia nchini Tanzania. Aidha alizungumza na Watanzania waishio nchini Marekani katika jiji la Washington.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Kushoto ni ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimewangalia  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier akisaini kitabu alichotunga kabla ya kumkabidhi Rais alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea kitabu kutoka kwa   Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Katikati ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier  na ujumbe wake aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wa tatu kulia ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero, kulia ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Fedha za Nje Bw. Johannes Jovin akifuatiwa na Mkrugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy. Kushoto ni Mshauri wa Rais Masuala ya Uchumi Profesa Longinus Rutasitara akifuatiwa na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala.

PICHA NA IKULU

BENKI YA POSTA YAPATA FAIDA YA SH BILIONI 8.84 KABLA YA KODI KWA NUSU YA KWANZA YA MWAKA 2016

$
0
0
Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
***********
NUSU ya kwanza ya Mwaka 2016 iliyoisha mwezi Juni, imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Pamoja na changamoto mbalimbali ambazo bado zinaikabili benki yetu, kwa kipindi kirefu sasa, lakini Benki imefanikiwa kupata faida kabla ya kodi ya shilling bilioni 8.84 ukilinganisha  shillingi bilioni 5.48  zilizopatikana kipindi kama hicho mwaka 2015,ambayo ni sawasawa na ukuaji wa asilimia 61.47%. 



Ukuaji huu wa faida katika kipindi hiki cha nusu mwaka wa 2016 umewezesha kukua kwa mtaji wa wawekezaji hadi kufikia shillingi billioni 48 kutoka shillingi bilioni 37 mwezi Juni mwaka 2015.

Mapato ya Benki kwa nusu mwaka 2016 yaliongezeka hadi kufikia shilling bilioni 42.5 kutoka bilion 34 iliyofikiwa nusu ya mwaka 2015, huu ni  ukuaji wa asilimia 38%. Vilevile katika kipindi hichohicho amana za wateja ziliongezeka na kufikia shilingi bilioni 294.64 kutoka shilingi bilioni 263.68 June mwaka 2015, ukuaji wa asilimia 11.74%.

Mikopo imeongezeka hadi kufikia shillingi billioni 278 kutoka shilingi billioni 241.51 Juni mwaka 2015, ongezeko la asilimia 15.22%. Sehemu kubwa ya mikopo hii imetolewa kwa wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na wafanyakazi wa sekta  ya umma na serikali kuu.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Rasilimali za benki zilikuwa hadi kufikia shilling 390.8 bilioni mwezi Juni mwaka huu 2016 kutoka shillingi billioni 333.96 Juni mwaka 2015 ongezeko la asilimia 17.16%.

Benki ya Posta kwa mwaka 2016, iliendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, mwanzoni mwa mwaka huu benki ilifungua tawi lake jipya la Songea, Mkoani Ruvuma, ambapo Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, pamoja na tawi la Babati Mkoani Manyara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Msajili wa Hazina Bw.Lawrence Mafuru. 

Matawi hayo mawili yamejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na TPB. Benki ilihamishia Makao yake Makuu kutoka jengo la Extelecoms lililopo mtaa wa Samora na kuhamia kwenye Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama. 

Pia, benki imehamisha tawi lake la Moshi kwenda kwenye jengo jipya la NSSF, na hivi karibuni itahamisha matawi yake yaliyoko Kahama na Tanga kwenda kwenye majengo mapya na ya kisasa. Hizi zote ni jitihada za benki za kuongeza ufanisi na pia kutoa huduma zake kwenye mandhari bora naya kisasa zaidi.

Hadi hivi sasa TPB inayo matawi 30 na madogo (min branches) 30, Mashine za kutolea pesa (ATM) zinazo milikiwa na benki ya posta ni 38 na 200 za umoja wamabenki (Umoja switch), hivyo kuwawezesha wateja wetu kupata huduma ya pesa nchi nzima.

Pia benki inao mawakala wa benki 133 kupitia TPC,na vituo vya huduma 200 kupitia mawakala binafsi.

Benki ya posta inaendelea na jitihada zake za kuongeza wigo wa biashara kwa njia mbalimbali, zikiwemo:

kutoa  mikopo kwa vikundi vidogo vidogo  (group lending), ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 6.5 bilioni na huduma ya  kuwakopesha wazee (wastaafu loan) kupitia mifuko ya jamii  kama vile  PSPF,NSSF na ZFF, ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 56 bilioni.

Kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), enki imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 541 ili kuviinua kiuchumi vikundi vilivyo chini ya Baraza hilo.

Kufungua account za vikundi visivyo rasmi(VICOBA informal groups) ambapo hadi sasa akaunti 30 elfu zimefunguliwa.

Huduma za kibenki  kupitia simu za kiganjani,ambapo kwa kipindi cha nusu ya mwaka huu akaunti 271,427 zilifunguliwa, kulinganisha na akaunti 236,981 zilizofunguliwa hadi mwishoni mwa mwaka jana. Hili ni ongezeko la akaunti 34,446, sawasawa na asilimia 15.      
                                
Benki ya Posta imejidhatiti kuendelea kutoa huduma bora, nafuu na za kisasa kwa maana ya kutumia teknolojia zaidi katika kipindi hiki. Tunaamini kwamba bado kwa kutumia teknolojia ya TPB POPOTE tutaweza kuwafikia Watanzania walio wengi hasa vijijini ambao bado hawajaingia kwenye mfumo wa kifedha.

Pia benki itaendeleza na kuboresha mahusiano yake na makampuni za simu ili kuweza kupeleka huduma zake karibu zaidi na wananchi, na pia ushirikano wake na Saccos pamoja na Vicoba.

Benki ya Posta inapenda kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu. Tunaahidi hatutawaangusha, na tutaendelea kuboresha huduma zetu zenye gharama nafuu.

Pia shukrani za pekee ziende kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa uongozi wao thabiti na usimamizi imara, unaoendelea kuhakikisha kuwa benki inakuwa miongoni mwa taasisi bora za kifedha hapa nchini.

SIMBA APIGWA 2-0 NA JKT RUVU KATIKA FAINALI ZA FASDO FOOTBALL CUP JIJINI DAR.

$
0
0
 Timu ya Simba chini ya Umri wa Miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza dhidi ya JKT Ruvu
 Timu ya JKT Ruvu chini ya umri wa miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja kabla mechi haijaanza dhidi ya Simba
 Mkurugenzi mtendaji wa Faru Arts and Sport Development Organization (FASDO)  Tedvan Chande Nabora akikagua timu zote mbili kabla ya mpira haujaanza
 Mpira ukiwa unaendelea huku ikiwa ni vuta nikuvute ambapo JKT Ruvu waliibuka washindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba, pia simba walikosa penalti.
 Mgeni Rasmi katika Mashindano ya mpira wa Miguu wa FASDO, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akiwa anafuatilia Mchezo huo
Mashabiki wa upande wa Simba wakifuatilia kwa makini Mchezo huo
 Mashabiki upande wa JKT Ruvu wakiwa wanafuatilia kwa makini mchuano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akionesha kombe pamoja na zawadi ya mshindi wa kwanza kiasi cha Tsh 2,000,000 wakati wa fainali hizo, zilizofanyika katika viwanja vya JMK jijini Dar

Refa Bora katika mashindano ya mpira wa miguu ya FASDO akikabidhiwa zawadi ya Kitita chake cha Laki moja
 Washindi wa pili katika Mchezo huo timu ya Simba wakiwa wanapokea zawadi yao ya Tsh 1,000,000
Mgeni rasmi katika fainali hizo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akikabidhi kitita cha Tsh 2,000,000 kwa nahodha wa timu ya JKT Ruvu ambao ndio waliibuka kidedea.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akikabidhi Kombe kwa timu ya JKT Ruvu baada ya kuibuka washindi
 Wakiwa wanalipokea rasmi kombe lao baada ya ushindi
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole (Kulia) akikabidhiwa zawadi ya picha  kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya FASDO
 Timu ya JKT Ruvu wakifurahi baada ya kuibuka washindi.


WATEJA WAFURAHIA MICHUANO YA ICC INAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES

$
0
0

 Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na timu ya StarTimes na maveterani wa uwanja wa Mwembe Yanga – Temeke kabla ya mchezo wa kirafiki uwanjani hapo. StarTimes iliweka kambi uwanjani hapo ikiwa ni uzinduzi wa michuano ya ICC mwaka 2016 iliyokwishaanza kutimua vumbi Julai 22 wiki iliyopita ambapo ilidhamiria kuonyesha mchuano mkali wa ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.
 Baadhi ya wateja na mashabiki wa soka waliojitokeza kutazama mchezo wa  ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.
 
Mmoja wa wateja waliofika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, akipata maelekezo juu ya huduma za StarTimes kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wateja wa StarTimes na watanzania kwa ujumla wameipongeza kampuni inayouza na kusambaza visimbuzi vya matangazo ya dijitali, Starimes, kwa kuwaletea michuano ya kombe la mabingwa kimataifa au ICC mwaka 2016 moja kwa moja kupitia chaneli yake ya ST WORLD FOOTBALL.

Hayo yalisemwa na wateja mbalimbali waliohudhuria tamasha la uzinduzi wa michuano hiyo iliyoanza katika viwanja vya Temeke, Mwembe Yanga.

Katika tamasha hilo StarTimes walitinga viwanjani hapo na timu kamili ya wafanyakazi wake wa vitengo mbalimbali ambapo pia walifunga luninga uwanjani ili kuonyesha moja kwa moja mtanange wa watani wa jadi kutoka jiji la Manchester unaojulikana kama ‘Manchester Derby’ uliopangwa kufanyika jijini Beijing China lakini kutokana na hali ya hewa mbaya ikabidi uahirishwe.

Akizungumza katika viwanja hivyo Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka alibainisha kuwa, “Siku ya leo tumefika viwanjani hapa kwa lengo kubwa la kutaka kuwapa fursa wateja wetu kujionea uhondo wa michuano ya ICC inayonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi vyetu. Michuano hii inayofanyika katika nchi ya Marekani, Ulaya, Australia na China inazishirikisha timu kubwa duniani kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United na City, Juventus, Chelsea, Liverpool na nyiginezo.”

“Michuano hiyo imekwishaanza tangu Ijumaa ya wiki iliyoishia ambapo tumekwishashuhudia tayari timu kama Manchester United, Borussia Dortmund, Celtic, Leicester City, Inter Milan na PSG zimekwishatinga uwanjani. Siku ya leo tumekuja hapa kwa lengo la kuonyesha Manchester Derby lakini tunasikikita kuwa mchezo huo umeahirishwa kutokana na hali ya hewa mbaya kulikumba jiji la Beijing ambamo mchezo huo ulipangwa kuchezwa. Lakini badala yake tunaonyesha mchezo wa marudio baina ya Manchester United na Borussia Dortmund.” Aliongezea Bw. Kisaka

Meneja huyo wa Mauzo alimalizia kwa kusema, “Ningependa kuchukua fursa hii kwa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kufurahiamichuano hii mikubwa zaidi ambayo ni ya awali au maandalizi kabla ya ligi kuu mbalimbali kuanza mwishoni mwa mwezi wa Agosti. 

StarTimes pia tunaonyesha ligi hizo ambapo wateja watafurahia mechi zote za ligi za Bundesliga na Serie A kupitia chaneli zetu za michezo za SPORT ARENA, SPORTS FOCUS, WORLD FOOTBALL, SPORT LIFE NA SPORT PREMIUM na bila kusahau ligi za Ufaransa na Ubelgiji kupita chaneli ya FOX SPORTS. 

Ili kufaidi michuano hii ya ICC mwaka 2016 wateja itawabidi kulipia malipo kiduchu ya kifurushi cha Mambo kwa shilingi 12,000/- tu na kuweza kutazama mechi zote moja kwa moja ambazo zitarajiwa kuisha Agosti 13.”

Michuano ya ICC mwaka 2016 imekwishaanza Julai 22 ambapo mechi ya kwanza iliyofungua pazia ilikuwa ni kati ya Machester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund iliibamiza United kwa mabao 4 – 1. Michezo mingine iliyokwishachezwa ni pamoja na PSG kuitandika 3 -1 Inter Milan na Leicester City kuwashinda Celtic kwa mikwaju 6 – 5 ya penati baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1 – 1 ndani ya dakika 90.


Siku ya leo Jumanne kutakuwa na mechi nyingine ambapo mabingwa wa Italia, Juventus watashuka dimbani kuwakabili timu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza katika mishale ya saa 7 mchana kwa muda wa hapa nyumbani Tanzania kupitia chaneli ya WORLD FOOTBALL ndani ya ya StarTimes pekee.

KARIBU KIPEPEO DESIGNER (jack)

$
0
0










Jack  kipepeo designer ni washonaji wa nguo katika mitindo tofauti tofauti
Kwa wanawake  wanaume na watoto. Mishono ya vitenge na vivalio vya kisasa
Karibu sana kipepeo designer  (jacky)
Anapatikana migera (kwa phocas)
Simu: 0762 682 450/ 0788 833 723

HOMA YA INI B NA C KUTOKOMEZWA IFIKAPO MWAKA 2030

$
0
0
 Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo mchana.
 Bango likihimiza kuungana kutokomeza homa ya ini.
 Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya Mwembe Yanga. Katikati ni Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan.
 Vijana waliopo kwenye mtandao wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa TanPud Tanzania, Godfrey Ten, akizungumza katika maadhimisho hayo.



 Ofisa Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa Asasi za Kiraia kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya Tanzania, Salome Mbonile, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Pasada, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo.

 Maadhimisho yakiendelea.
 Vijana waathirika na dawa za kulevya wakicheza kwenye maadhimisho hayo.
 Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde akizungumza kuhusu ugonjwa huo.
Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.

Dotto Mwaibale

UGONJWA wa homa ini umepangwa kutokomezwa ifika mwaka 2030 imefahamika ambapo watu wapatao  milioni 1.4 upoteza maisha ulimwenguni kutokana na maambuki ya ugonjwa huo ulimwenguni hasa kwa wale wanaotumia mihadarati kwa njia ya kujidunga.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufahamu kuhusu na kuungana na juhudi za ulimwengu za kutokomeza homa ya ini.

Alisema mada ya kampeni ya kimataifa ya homa ya ini ya mwaka huu ni utokomezaji ambao ni mwaka muhimu kwa homa ya ini.

Alisema lengo la maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia, wafanyakazi wa huduma za afya, taasisi na vikundi vya utetezi na ushawishi ni kuongeza ufahamu wa homa ya ini B na C hasa kwa makundi hatarishi kama watumiaji wa mihadarati wanaojidunga.

Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde alisema katika mkutano mkuu wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ni serikali zote ziliazimia kwa pamoja kuidhinisha mkakati wa ulimwengu wa utokomezaji wa homa ya ini.

Alisema hadi Februari 2016 nchi 36 zilikuwa zina mipango ya kitaifa ya utokomezaji wa homa ya ini na nchi 33 zipo katika mikakati ya kuandaa mipango hiyo.

"Mkakati unalenga kutokomeza homa ya ini B na C ifikapo mwaka 2030 ambapo unahusisha malengo ya tiba ambayo iwapo yatafikiwa yatapunguza vifo vinavyosababishwa na homa ya ini kwa asilimia 65 na kuongeza huduma ya tiba kwa asilimia 80 hivyo kuokoa maisha ya watu milioni 7.1 ifikapo mwaka 2030" alisema Dk.  Aikaeli

MPANGO WA OFISI YA WAZIRI MKUU KUHAMIA DODOMA WIKI IJAYO WAKAMILIKA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu, na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb)amepokea  Mpango Mkakati  wa Kuhamia Dodoma  wiki ijayo wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.
Mhagama amekutana wna wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi katika kukamilisha Mpango Mkakati huo ili kukamilisha utekelezaji huo. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali akiwasilisha Issa Nchasi akiwaitisha wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Mpango wa Ofisi hiyo kuhamia Dodoma wiki ijayo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama na Naibu Waziri anayeshughulikia ( Watu Wenye Ulemavu )Abdallah Possi  pamoja na wakuu wa Idara wakifuatilia uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma wa Ofisi hiyo, leo  Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai, 2016.
 Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es  Salaam tarehe 28 Julai, 2016.
 Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa kuhamia Dodoma katika  JIjini Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.

Imetolewa na;
Afisa Habari,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Waziri Mkuu.

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. --- Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo. Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi. Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.  Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu. --- Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu. "Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema Kingi. Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).
Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development. Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu. Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo. 
Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi.
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development
Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza. --- Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza. Alisema kuwa aliwatafuta baada ya kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu. "Mbali na hilo kwa sasa tuna shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza lugha ya Kiingereza na maktaba," alisema mkurugenzi huyo na kuendelea: Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola 10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa. Nae Bi. Riziki Hassan Selenge alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka shule watoto wao. Upande wake Mwenyekiti mstaafu, 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Akitoa historia fupi Bw. Sadiki alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993 kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.  

MARAIS WASTAAFU NCHI ZA AFRIKA WAWASILI JIJINI DAR KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA UONGOZI WA MWAKA 2016

$
0
0

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki (pichani kulia) akiwasili leo jijini Dar Es Salaam akiwa na Mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja,kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Mkutano huo utakaodumu kwa siku mbili utawajumuisha wadau mbalimbali.PICHA NA MICHUZI JR.MMG.
Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akisalimiana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wa siku mbili.Pichani kati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .
Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Mheshimiwa Thabo Mbeki akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thamsanga Dennis Msekelu baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 utakoanza kesho hapa jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.

Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jioni ya leo jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 unaotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro kwa siku mbili.
Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano akikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya UONGOZI mara baada ya kuwasili jijini Dar Es Salaam jioni ya leo kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Uongozi wa mwaka 2016 wa siku mbili,utakoanza hapo kesho jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.Pichani shoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja .

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SEKRETARIETI NA WAFANYAKAZI WA CHAMA DODOMA MJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuongea na sekretarieti ya CCM kwa mara ya kwanza katika  makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma Jana
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Secretarieti ya CCM  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma Jana
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma Jana
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kupata picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma Jana
PICHA NA IKULU

TASWIRA YA MJI MDOGO WA NSHAMBA MULEBA

$
0
0

Pichani wanaonekana Wananchi wakifua mtoni Kutokana na shida ya maji kwa baadhi ya maeneo hali hii huwa ndio suluhisho kwa jamii fulani huko Vijijini kwetu, hapa ni maeneo ya Kalela Nshamba Wilayani Muleba
Wanaonekana baadhi ya watuwaliokuwa wakifua mtoni hapo wengi wao wakiwa wanawake
Kutoka maeneo ya Mto Kichuro barabara ya Kalela Nshamba Wilayani Muleba, Camera yetu ikikufikishia unachostahili.
Mitaa ya Mji Mdogo wa Kibiashara wa Nshamba -Muleba.
Mdau Abdul pichani kama alivyokutwa akivinjali katika mitaa ya Mji Mdogo wa Nshamba.
Bila shaka unakumbuka na umepata kutumia sabuni za MAGWAJI kwa kuogea kabla ya Ujio wa sabuni ya Imperial (kutoka Kenya)
Hakika ni changamoto kubwa kwa ndugu zetu huko Vijijini mpaka sasa Sabuni za Magwaji zinatumika,wananchi wanaishi kwa masikitiko sawa na dhama za kunywa chai iliyochanganywa na pipi badala ya Sukari na kupikia samli ya ng’ombe wetu badala ya mafuta ya kupikia safi yanayotoka nje au yale ya pamba yetu...!
Hapa tunakutana na Wauzaji wa mabumunda /Baragala moja inauzwa kwa sarafu ya shilingi 10 tu!
Hii ni Live kutoka katika Gulio la Jumamosi katika Mji Mdogo wa Kibiashara wa Nshamba wilayani Muleba.

Camera yetu ikiendelea kukuangazia mitaa mbalimbali iliyopo Mjini Nshamba Wilayani Muleba
Pitapita za hapa na pale wanaonekana Wananchi wa Nshamba wakiendelea kufanya mahemezi yao kwa ajili ya matumizi mbalimbali
Hapa kinachotakiwa ni kufanyiwa marekebisho tu,hakika utalipenda hilo gari pichani ni roli aina ya Leyland maalum kwa ajili ya mizigo,hiyo ni Nshamba Muleba

Kutoka Mji Mdogo wa Nshamba Wilayani Muleba #Bukobawadau Media, tunaendelea kutoa Shukrani kubwa kwako wewe msomaji kuendelea kutembelea mtandao wetu!

Muonekano wa Msikiti wa uliopo Nshamba

Bukobawadau Nshamba Muleba July,2016
Barabara ya Tappa kutoka na kuelekea Muleba Mjini
Moja ya jengo la ghorofa lililopo Nshamba maarufu kwa Mshuti

Kagambo Trans ndivyo linavyosomeka roli aina ya Fuso pichani #Nshamba July 2016
Mdau pichani kama alivyokutwa na Camera yetu mitaa ya Nshamba Mjini July,2016
Kijana Abad Rasheed anaonekana pichani kupitia Mdandao wenu wa Bukobawadau # Nshamba
Kutoka Mji Mdogo wa Nshamba Wilayani Muleba #Bukobawadau Media, tunaendelea kutoa Shukrani kubwa kwako wewe msomaji kuendelea kutembelea mtandao wetu!

 Kwa hisani kubwa ya www,proaktiv.co.tz

TKIFO CHA JOSEPH SANGA WA TANZANIA DAIMA!

$
0
0
TANZIA.Mpiga picha mkongwe wa habari nchini ambaye amewahi kuwa mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga (pichani) amefariki dunia. Senga ndiye aliyepiga picha ya Daudi Mwangosi wakati anauawa na askari Polisi katikat Mji Mdogo wa Nyololo, mkoani Iringa. Mungu ampumzishe kwa amani.!!
 Ameandika Dotto Bulendu wa Star Tv;Simanzi,siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi,SHUJAA JOSEPH SENGA,amefariki dunia usiku huu.
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Bila Joseph Senga,shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,milio ya risasi ikisikika,na kuzitunza,zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi,leo hii asingekuwa Senga,nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.Nakulilia Senga..
Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua,Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.
Nenda Senga,picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.

SIA PIUS NDIYE WINDHOEK DRAUGHT MISS SINZA 2016

$
0
0
 Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd akisema chochote kwenye shindano hilo.
 Mtoa huduma wa kampuni hiyo akitoa huduma kwa wadau wa windhoek.
 Wadau wa Windhoek ndani ya Defrance Hotel katika shindano hilo.
 Hapa ni windhoek tu kwa kwenda mbele.
 Wadau wa windhoek wakiwa kwenye shindano hilo.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Jerome Rugemalira (kushoto), akigongesha chupa ya windhoek na mdau wa kinywaji hicho, iliyokatika muonekano mpya katika shindano hilo.
 Wacheza shoo wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia wakishambulia jukwaa katika shindano hilo.
 Wasanii wa kampuni ya mabibo wakionesha umahiri wa kucheza wakati wa shindano hilo.
 Washiriki wa shindano hilo wakijitambulisha kwa kucheza kabla ya kuanza kwa shindano hilo.
 Wanenguaji wa Bendi ya FM Academia wakiwa kazini.

 Washiriki wakiwa katika vazi la ubunifu.
 Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.
 Baadhi ya washiriki ambao hawakufanikiwa kuingia tano bora.
 Warembo walioingia tano bora. Kutoka kulia ni Catherine Listone, Sia Pius, Hafsa Mahamood, Saida Khalifa na Faith Msuya.
 "Jamani tuchangechange mapene tuongeze windhoek meza imekauka hapa"
 Hapa ni furaha tu kwa kusonga mbele.
 Majaji wakiwa tayari kuwatangaza washindi.
 Mdau wa Windhoek na mashindano ya Miss Tanzania, Rutha Lucas akitoa sh.100,000 kwa kila mshiriki wa shindano hilo ikiwa ni kifuta jasho.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto),  akimkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano hilo kitita cha sh.500,000.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabishi mshindi huyo moja ya katoni ya windhoek kati ya tano zilizotolewa na kampuni hiyo kwa mshindi huyo ambapo pia mshindi wa pili na watatu walikabidhiwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Sinza 2016 imemtangaza Sia Pius kuwa mshindi wa Windhoek Draught Miss Sinza 2016 baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Defrance iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana usiku.

Pius aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake tisa waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Catherine Listoni huku ya tatu ikichukuliwa na Hafsa Mahamood.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spiritis kupitia bia ya Windhoek pamoja na wadhamini wengine.

Mshindi wa kwanza wa shindano hilo alizawadiwa sh.500,000 wakati wa pili akijipatia sh.300,000 na watatu akiondoka na kitita cha sh.200,000 huku washiriki wengine wakiondoka na kifuta jasho cha sh.100,000 kila mmoja.

Washindi hao watatu wataingia moja kwa moja katika shindano la kumsaka Miss Kinondoni 2016 litakalofanyika mwezi ujao.

BOHARI LATEKETEA KWA MOTO SINZA LEGO JIJINI DAR JIONI HII

$
0
0
Bohari likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea
Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto ,  hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua 

Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa vyenginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiriki wake hakufahamika kwa mara moja limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili.  Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.

LOWASSA, MBOWE NA NAPE WAONGOZA KUUAGA MWILI WA MPIGAPICHA MAREHEMU SENGA

$
0
0
 Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akifuatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Annastazia Wambura, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe pamoja na waombolezaji wengine wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, marehemu Joseph Senga, Sinza Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda kwao wilayani Kwimba, Mwanza kwa mazishi kesho.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Waombolezaji wakiiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda wilayani Kwimba kwa mazishi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Joseph Senga
 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akitoa heshima za mwisho
  Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Joseph Senga
 Mjane wa marehemu Senga, Winfrida Senga akiuaga mwili wa mumewe
 Mtoto wa marehemu Joseph Senga, Esther akiuaga mwili wa marehemu babake
 Mtoto Kapama Senga akisaidiwa alipokuwa akiuaga mwili wa babake
 Mwakilishi wa Chama cha Wapiga Picha za Habari Tanzania, Seleman Mpochi akitoa salamu za rambirambi pamoja na kuwasilisha mchango uliochangwa na wapigapicha kusaidia shuguli za mazishi za aliyekuwa mpiga picha mwenzanoa, marehemu Joseph Senga.

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akijdiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
 Lowassa akiwa na Nape Nauye pamoja na Freeman Mbowe
 Familia ya marehemu Senga
 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika akitoa salamu za chama hicho
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi
 Waombolezaji wakiwa katika shughuli hizo
 Freeman Mbowe ambaye ni mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, akielezea pengo lililoachwa na marehemu Senga katika gaezeti hilo pamoja na Chadema
 Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi za serikali wakati wa kuuga mwili wa marehemu Senga
 Nape akaipeana mkono na Lowassa baada ya kutoa salam za rambi rambi
 Nape akiteta jambo na Mbowe

 Mbunge wa Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba, Richard Ndassa, ambaye amewahi fanya kazi na marehemu Senga gazeti la Mfanyakazi, akiuaga mwili wa marehemu Senga
 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na baadaye kuhamia Chadema, Mgeja akiauaga mwili wa marehemu Senga
 Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Senga
 Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa akitoa heshima za mwisho  wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Senga
 Mpiga Picha wa Gazeti la Mtanzania ambaye pia amewahi kufanya kazi na marehemu Senga katika gazeti la Mfanyakazi, Deus Mhagale akiuaga mwili wa marehemu Senga
 Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda, ambaye pia amewahi fanya kai na marehemu Joseph Senga gazeti la Mfanyakazi akiuaga mwili wa marehemu
 Waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiuaga mwili wa marehemu Senga
 Wafanyakazi wa Gazerti la Tanzania Daima waliokuwa wanafanyakazi na marehemu Senga wakiwambele ya jeneza la mwili wa Senga
 Wapiga picha wakiuingiza kwenye gari mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao, marehemu Senga

Baadhi ya wadau waliokuwa miongoni mwa waombolezaji. Kutoka kushoto ni, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tganzania, Matina Nkuru,  Muhidin Sufiani,Rukia Mtingwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanania, Jackson Mmbando
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>