Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live

JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU

$
0
0
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
  Rais  Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
  Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. Magufuli kuhusiana na  Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
 Wananchi wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa  noti ya shilingi 10,000/- akitaka kumtuza  Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
Rais Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga  wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016

DC TUNDURU JUMA HOMERA AWATIA MBARONI VIONGOZI 4 KWA TUHUMA ZA KUUZA VIWANJA.

$
0
0

Askari akiwa amewakamata Viongozi wawili wa Serikali ya Kijiji waliokuwa wakituhumiwa kwa ubadhirifu wa viwanja.

Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala akizungumza mbele ya Wananchi .


Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na Wananchi wa Vitongoji vya FrankWeston na Umoja vilivyokumbwa na mgogoro wa ardhi.
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera akimuagiza Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu Japhet Muogopeni Mnyagala kuchukua hatua stahiki kuhusiana na mgogoro wa Ardhi ndani ya Wilaya hiyo.


Wananchi wakimsikiza kwa makini Mhe DC. Juma Zuberi Homera .
 
Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, amewatia mbaroni Viongozi wanne wa Serikali ya vijiji kwa kosa la usimamizi mbovu wa ardhi katika Vitongoji vya Umoja na Frank Weston katika kata ya Nanjoka Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya Bw. Yahaya Issa Abdallah alimueleza DC. Homera kuwa Vitongoji vya Umoja na Frank Weston vimekumbwa na mgogoro wa ardhi kati ya Wenyeji, Wageni na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Tunduru kwa muda mrefu.

Aidha Serikali kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili Wilaya, iliwapimia ardhi Wananchi toka 11/08/2014 lakini ikabainika kuwa mpaka  30/06/2016 bado Wananchi hawakupewa maeneo yao na kuna baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri pamoja na Wageni wapo kwenye orodha ya Wananchi wanaopaswa kugawiwa Viwanja.

Akihutubia kwenye mkutano huo wa hadhara, uliyofanyika katika Shule ya Msingi Umoja, DC Homera aliwaeleza Wananchi kuwa wasiwe na shaka,kwa sababu Serikali ipo upande wao na hakuna atakaye dhurumiwa haki yake, alisema “Namtaka Mhasibu wa Ardhi na Maliasili alete orodha ya waliolipia Ardhi maeneo ambayo siyo ya wakazi, na ambao ni Watumishi wa Halmashauri wafutwe kwenye orodha hiyo na warejeshewe fedha zao”.

Mfano, kuna baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi na Maliasili,ambao wamefanya ujanja ujanja kinyume cha sheria kwa kuwaweka watoto wao kwenye orodha,na majina yao yameorodheshwa hapa,hivyo hatua za kisheria na taratibu zitafanyika kuondoa huu mgongano ambao umejitokeza katika hili pia. 
 
 Kama vile haitoshi ikabainika kuwa kuna kuna baadhi ya Viongozi walikusanya fedha  za wananchi  wapatao 522 na kutowapa risiti,jambo amablo ni hujuma za wazi kabisa  za kuikosesha Halmashauri ya Tunduru Mapato na kupelekea fedha kuwa mikononi mwa wajanja wachache.

Aidha aliwataka Wafanyakazi wa Idara ya Ardhi na Maliasili kujieleza ni kwa nini wamewagawia watu ardhi ambao sio wakazi? kwa nini wamefanya udanganyifu wa kuwa milikisha ardhi Watumishi wa Halmashauri kwa njia za rushwa? na kwa nini wananchi zaidi ya 522 hawajapewa maeneo yao kwa zaidi ya Miaka Miwili?

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa Wilaya ndg. Japhet Muogopeni Mnyagala alikiri kufanya kosa,lakini pia alimuakikishia Mkuu wa Wilaya ndani ya wiki moja wananchi wataanza kugawiwa viwanja na zoezi hilo litaanza Kesho (leo).

Mkuu wa wilaya aliwaagiza askari wakamate viongozi walio kuwa wasimamizi wa upimaji wa maeneo katika vitongoji vya Umoja na Frank Weston ambao ni Mohammed Dumsala, Matola Limelime, Halid Daud na Tekla Damas.

MKUTANO WA LOWASSA NA WANAFUNZI MUHIMBILI WAZUILIWA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mkutano uliokuwa ufanywe na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowaasa.
Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike na baadhi ya vijana wa kikristo ambao ni wanafunzi wa chuo hicho ulikuwa pangwa kufanyika juzi chuoni hapo kuanzia saa za mchana.

Akizungumza mtandao wa www. habari za jamii.com  mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema maandalizi yote ya mkutano huo ambao ulikuwa baada ya ibada yalikuwa yamekamilika.

"Tulifanya taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo ambao ulitukubalia na kumualika ndugu Lowassa lakini tumeshangazwa na zuio lililotolewa na uongozi wa chuo" alisema mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo alisema kuwa saa sita mchana wakati wakimsubiri mgeni rasmi Edward Lowassa awasili mkuu wa chuo hicho na viongozi wengine waliwaita na kuwaeleza kwamba mkutano huo umewekewa zuio kutoka juu hivyo hautafanyika bila ya kutoa sababu .

Msemaji wa Lowassa Abubakar Lihongo alisema wanafunzi hao baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano huo walimuomba radhi Lowassa na kumueleza watamualika tena kipindi kingine wakiwa tayari.

"Mimi naona zuio hilo linatokana na masuala ya kisiasa lakini kuna barua ya wanafunzi hao ipo katika mitandao ya kijamii mkiipata mnaweza kupata picha halisi" alisema Liongo.



Airtel Money yaingia ubia na NMB bank kuongeza ufanisi kwa wakala wake.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya NMB ihudumie wakala wa Airtel Money

Airtel Money yaingia ubia na NMB bank kuongeza ufanisi kwa wakala wake.
  • Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB popote.

    Dar es Salaam jumapili julai 31 kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.

  • Akiongelea ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya Airtel na benki ya NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika na  nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja wengi”

    Tunajisikia fahari kuona NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhairi huduma za kifedha kwa mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa huduma kwa lengo la  kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika swala la huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara kama haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”

    “NMB itahudumia wakala wetu zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima, haya ni maendeleo makubwa sana hata kwa biashara yetu”. alieleza Colaso

    NMB na Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money. Airtel Money imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.

    Mwisho.

SHIDA KUBWA YA MAJI WILAYANI KARAGWE!!

$
0
0
Ukweli ni kwamba ukiwa nje ya wilaya hii ya Karagwe hutawaza kwamba kuna uwezekano wa kuwepo tatizo la maji la kiasi hiki katika maeneo mengi na Mji wa Kayanga ambao ndio makao makuu ya Wilaya yenye majimbo mawili makubwa ya Karagwe na Kyerwa
 Foleni kubwa ya wananchi wakati wakisubilia huduma ya maji maeneo ya Omulushaka Karagwe
 Pichani wanaonekana Wakazi wa kijiji cha Kiyanga  Wilayani Karagwe  Mkoani Kagera wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kutoka katika shimo lilochimbwa bondeni ,na hiki ndicho chanzo kikubwa wanachokitegemea pamoja na kwamba maji hayo ambayo kwa kiasi kikubwa hutegemea kunyesha kwa mvua sio salama kwa binadamu,wakiongea na mwanalibeneke wetu Wakazi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia maji hayo hayo.
Kadhia hii ya maji ni alama mbaya sana kwa wazawa wote wa Karagwe  waishio ndani na nje ya Wilaya ya hii  pia ni aibu na alama kubwa ya usaliti wa wawakilishi wao wote wa vipindi mbalimbali!!
Hakika ni lazima zitumike nguvu za ziada kuwaokoa wananchi  hawa wanaokatiza usingizi kila siku kwenda kupanga foleni ya maji katikati vyanzo mbalimbali.
Credit Photo:@Mc Baraka

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AZINDUA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified".  Mjema alizindua uwanja huo leo katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate akishuhudia tukio hilo.PICHA NA MICHUZI JR
  Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto) akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified" uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa. 
Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo. 
 Mandhari ya uwanja wa Mpira wa Kikapu na Netiboli wa shule ya Sekondari ya Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified".
Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo.

 Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema kuwa amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.

Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya "Be Kidotified". Alisema kuwa amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya kuendeleza michezo na taaluma.

Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli) kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani. 

Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi milioni 50.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini. 

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo vitamwezesha mshiriki kupata ajira. 

Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao ipasavyo. 

Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo, lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi. 

“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ” 

“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation, na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate. 

Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu. 

Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila siku.
 

WASANII, WATANGAZAJI NA WATU MAARUFU KUVUNA MAPESA KUTOKANA NA MITANDAO YAO YA JAMII

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa akiitanga Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
 Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
---
Kampuni inaoongozwa kwa kutoa huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
Huduma hii ya kisasa inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.
Uzinduzi wa kitengo hiki cha matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoleta mapinduzi katika sekta ya matangazo ya biashara nchini umefanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko kutoka makampuni ya FMCG, huduma za mawasiliano,mabenki na taasisi mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na wanamichezo.
Kampuni ya Binary kwa kuanza tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu Zaidi zaidi ya 40 ambao miongoni mwao wapo wasanii wa filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa redio na luninga. Kutokana na ushirikiano huu Binary itawatumia katika huduma za matangazo za wateja mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa zao kidigitali ili kuwafikia watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa urahisi.
Huduma hii mpya ya matangazo katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa huduma zao kuwafikia wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa wasanii na watu maarufu ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya uhakika kutokana na kutumiwa kwao katika huduma ya matangazo na pia ina unafuu kulinganisha na njia nyingine za matangazo.
Profesa Elisante Ole Gabriel alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia wasanii wa tasnia mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa huduma hii nchini ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati huohuo kunufaisha makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii mpya ni jukwaa la aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa inawezesha matangazo kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa kulinganisha na kutangaza kwa kutumia magazeti na ama majarida na inaleta unafuu kwa watangazaji ambao kwa kutumia mtandao wasanii zaidi ya 40 ambao tunashirikiana nao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii matangazo yataweza kuwafikia watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya milioni 20 nchini na tunao uwezo wa kufikia watu wengi zaidi”.
Kuhusiana na huduma hii mpya ya matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema “Tunatumia fursa ya kutumia teknolojia ya digitali katika biashara ambayo itaongeza vipato vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea kuonekana kwa watu wengi katika jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi kwenye fani yao na tasnia yao”
Aliongeza kuwa ushirikiano wa Binary na wasanii katika huduma za matangazo utafanyika kwa uwazi na kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano maalumu ya malipo kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo litakalowekwa kwenye akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na wafuasi wanaotembelea akaunti zao.
“Viwango vya matangazo viko wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila upande utanufaika inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina yake kwa watangazaji kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa kuwa njia zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena kutokana na mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema

R.I.P REGENDARY RAMADHAN JUMA

$
0
0
Pigo jingine kwa mashabiki wa soka Mkoani Kagera na Taifa kwa ujumla baada ya kumpoteza mdau mkubwa ,aliyekuwa mchezaji wa Zamani RTC ,Mwl wetu na Mwl wa timu ya Under 20 msimu huu KAGERA Sugar Fc ,Regendary Rama aka Rama Mtoto hatupo nae tena

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA KAGERA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WIKI YA UNYONYESHAJI KITAIFA MKOANI KAGERA TAREHE 04 AGOSTI, 2O16

$
0
0
Ndugu Waandishi wa Habari, Wiki ya Agosti 1 hadi 7, Tanzania huungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani. Maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 1992 kufuatia Azimio la Innocent (nchini Italia) ambalo linasisitiza umuhimu wa kulinda, kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji na ulishaji bora wa watoto. Wiki ya Unyonyeshaji inatukumbusha kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto na kuendelea kunyonyeshwa mpaka umri wa miaka miwili au zaidi. Aidha, Wiki ya unyonyeshaji, mwaka huu 2016 inaadhimishwa Kitaifa Mkoani kwetu Kagera. Ndugu Waandishi wa Habari, Kauli mbiu ya mwaka huu 2016, ni “UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA: MSINGI KWA MAENDELEO ENDELEVU.” 
 Tunaelewa wazi kuwa pamoja na maendeleo ambayo Mkoa wetu umekuwa ukiyapata katika maeneo mbalimbali, bado utapiamlo umeendelea kuathiri jamii hususani katika nyanja za afya,elimu na uchumi; hivyo kusababisha kasi ya kupungua kwa umaskini kutoridhisha. Lishe duni si tu inaathiri maendeleo ya mtoto lakini pia inaathiri ukuaji wake kimwili na kiakili hatimaye kuathiri mchango wake katika maendeleo ya Taifa katika kipindi chote cha uhai wake.
Ndugu Waandishi wa Habari, Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama ina umuhimu mkubwa sana kwa Mkoa wetu ukizingatia kuwa takribani asilimia 52 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wetu, wamedumaa. Udumavu huu unatokana na lishe duni waliyoipata watoto hawa tangu wakiwa wadogo ikiwemo suala zima la unyonyeshaji. Lazima tuungane wana Kagera kubadilisha hali hii; Mkoa wetu ni kati ya Mikoa yenye chakula cha kutosha na fursa nyingi, hivyo ni lazima tuungane kuondoa huu udumavu kwa watoto.
 Sababu kubwa ya utapiamlo huu kwa watoto ni ulishaji usio sahihi ambao huchangiwa na majukumu mengi yanayomkabili mama na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto. Ni dhahiri kuwa mchango wa mwanamke katika familia, ajira na uzalishaji kwa ujumla ni mkubwa hivyo ni muhimu kuwatia moyo na kuwasaidia wanawake ili waweze kutimiza majukumu ya uzalishaji na utunzaji familia kwa ukamilifu.
Ndugu Waandishi wa Habari, Nasistiza Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004 kuzingatiwa hasa katika mkoa wetu ili kumruhusu mama mwajiriwa anayenyonyesha apewe ruhusa ya masaa mawili kila siku ili akamnyonyeshe mtoto wake, pia mama aliyejifungua mtoto mmoja kupewa likizo ya uzazi ya siku 84 kama amejifungua mtoto mmoja na siku 100 kwa watoto zaidi ya mmoja. Pia baba kupewa likizo ya siku 3 ndani ya wiki moja aliyojifungua mama ili kutoa huduma kwa mama. 
 Aidha sheria hiyo inakataza mama aliye ajiriwa na ambaye ananyonyesha au mjamzito kufanya kazi ngumu au za hatari kwa afya yake au ya mtoto wake. Kwasababu hii, ninatoa wito kwa Taasisi zisizo za Kiserikali, Taasisi za Kijamii na za Kidini, jamii na familia kwa ujumla kuwasaidia wanawake ambao hawapo kwenye ajira rasmi ili waweze kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo.
Ndugu Waandishi wa Habari, (Ushauri) Mtoto anyonyeshwe ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa. Pia mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo. Uji, ugali, ndizi, maziwa ya kopo au ng'ombe, havitakiwi kwa mtoto mwenye umri chini ya miezi sita; Mwili wa mtoto wa umri huu hauna uwezo wa kuvitumia, hivyo mtoto akipewa vyakula hivi hujaza tumbo tu na kumfanya mtoto kujisikia ameshiba na kumzuia kunyonya aidha, mtoto anyonye mara kwa mara kadiri anavyohitaji.
Ndugu Waandishi wa Habari, (Umuhimu wa Maziwa ya mama) Kunyonyesha maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto ndio njia bora na salama ya kumpatia virutubishi vyote muhimu kwa ukuaji na maendeleo yake. Maziwa ya mama yana sifa ya kipekee ya kuwa na kinga ambazo humkinga mtoto dhidi ya magonjwa hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano. Unyonyeshaji sahihi wa maziwa ya mama katika miezi sita ya mwanzo pia huweza kutumika kama njia ya uzazi wa mpango. Tendo la kunyonyesha pia linajenga mahusiano kati ya mama na mtoto wake. Mtoto anapofikia umri miezi sita, anapaswa kuanzishiwa vyakula vya nyongeza, lakini aendelee kunyonyeshwa maziwa ya mama mpaka atimize miaka miwili au zaidi.
Ndugu Waandishi wa Habari, (Mikakati) ili kufanikisha unonyeshaji jamii inashauriwa kutekeleza mikakati ifutayo; Kuanzisha na kuendeleza vikundi vya kusaidia masuala ya unyonyeshaji ambavyo vitawashirikisha baba au wanaume.
Kuhakikisha kuwa vituo vya afya, maduka ya dawa na maduka ya bidhaa mbalimbali yanatekeleza kanuni inayodhibiti uuzaji na usambazaji wa maziwa na vyakula vya watoto.
Kuwaunganisha vijana wa kike na wa kiume ili waweze kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu za kuboresha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Kuhakikisha kuwa vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya vinatekeleza vidokezo kumi vya kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuwa Rafiki wa Mtoto. Nawaombeni wananchi kabla hamjaondoka hakikisheni mnapitia kwenye mabanda yetu hapa chini kuelekezwa juu ya vidokezo hivyo.
Ndugu Waandishi wa Habari, (Wito) Serikali inatambua kuwa bado zipo changamoto nyingi katika kukabiliana na utapiamlo hapa Mkoani mwetu. Pengine, changamoto kubwa kuliko zote ni ile ya uelewa mdogo wa masuala ya lishe katika jamii ikiwemo unyonyeshaji, kuanzia ngazi ya familia hadi kwa watendaji na viongozi wa Serikali. Uelewa mdogo kuhusu masuala ya lishe umesababisha masuala ya lishe kutopewa kipaumbele katika jamii ambako ndiko waliko watoto na wanawake wengi wanaohitaji zaidi huduma bora za lishe.
Nipende kutoa wito kwenu Wanahabari kutumia ujuzi wenu na vyombo vyenu vya Habari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya kuielimisha jamii hasa katika Mkoa wetu wa Kagera juu ya kukabiliana na utapiamlo na umuhimu wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama kama inavyoshauriwa na wataalamu wetu wa lishe ili tuwe na kizazi cha watoto wenye afya zilizoimarika.
Imetolewa na; Sylvester Raphael, Afisa Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
KAGERA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 04 AGOSTI, 2O16

$
0
0
Ndugu Waandishi wa Habari, Katika Mkoa wetu wa Kagera vimeibuka vitendo vya hujuma hasa wakati huu wa majira ya kiangazi (hususani mwezi Juni na Julai 2016) ambapo wananchi wenye nia mbaya na Taifa na Mkoa wetu wamekuwa wakichoma moto ovyo na kuteketeza misitu ya hifadhi ya Serikali, mashamba ya miti ya watu binafsi na mashamba ya mazao ya chakula suala ambalo halikubaliki na ni kinyume na sheria zilizowekwa na nchi yetu.
Ndugu Waandishi wa Habari, Kwa taarifa nilizonazo za uchomaji moto katika Halmashauri za Wilaya tatu mkoani kwetu ni kama ifuatavyo; Kufikia Agosti 3, 2016 katika Manispaa ya Bukoba maeneo yaliyoripotiwa kuchomwa moto ni ekari tisa na nusu (9.5) zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000)
 Katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba zaidi ya ekari 473 za misitu ya hifadhi ya kupandwa na mazao ya chakula imechomwa na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo taarifa zilizonifikia ni kwamba tayari ekari 53 za misitu na mazao ya chakula zimechomwa na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha pia kwa wananchi. Kwa hizo Halmashauri chache za Mkoa wa Kagera unaweza kuona uharibifu mkubwa wa uchomaji moto ulivyosababisha hasara kubwa.

Ndugu Waandishi wa Habari, Kutokana na uharibifu huo wa uchomaji moto katika Mkoa wetu wa Kagera na kwa Mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha sheria ya Tawala za Mikoa, sheria Na. 19 ya mwaka 1997 Kifungu cha 5 kifungu kidogo cha (1) na (2), Sheria hii inanipa Mamlaka na majukumu ya kulinda Amani na Usalama na kuhakikisha uzingatiaji wa sheria katika Mkoa wa Kagera unatimizwa. 
 Aidha, kwa kuzingatia sheria ya misitu Na. 14 ya mwaka 2002 vifungu vya 70 hadi 73 na Kifungu cha 91 vifungu kidogo (1) na (2) vinavyozuia mtu yeyote kuchoma mashamba binafsi na misitu ya hifadhi. Hivyo, ninawaagiza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wote Mkoani Kagera kuhakikisha wanadhibiti uchomaji moto ovyo kwenye Wilaya zao kwa kutumia sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na sheria ndogo za Halmashauri za Wilaya za utunzaji wa mazingira.
Ndugu Waandishi wa Habari, Aidha, naagiza kwa maeneo ambayo yatabainika kuchomwa moto, moto huo uzimwe mara moja kwa ushirikiano wa wananchi na kumbaini mara moja mwananchi aliyehusika kuchoma moto huo katika eneo husika.
 Pia naagiza Viongozi wote kuanzia ngazi ya Kitongoji,Kijiji,Kata,Tarafa na Wilaya wenye jukumu la kisheria kusimamia misitu na mazingira wahakikishe waharifu wa uchomaji moto wanabainika na kukamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, Viongozi watakaoshindwa kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Ndugu Waandishi wa Habari, Vile vile naagiza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha taarifa za kudhibiti uchomaji moto na kubaini waharifu wa uchomaji moto ovyo zitumwe Ofisini kwangu kila siku. Pia Kamati za Mazingira zilizoundwa kupitia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kwa ngazi zote zihakikishe zinatekeleza kazi zake kisheria na kuwasilisha taarifa Mkoani kila Wiki.
Ndugu Waandishi wa Habari, Nawakumbusheni kuwa Misitu ni rasilimali muhimu kwa Taifa na kwa Mkoa wetu wa Kagera kwani misitu ni uhai. Misitu huchangia kuwepo kwa hali nzuri ya hewa, uwepo wa mvua za uhakika na uwepo wa vyanzo vya maji vya kutosha Mkoani kwetu na Taifa kwa ujumla.
 Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 inaitambua misitu ya hifadhi ya asili na ile ya kupandwa na inaeleza wazi ni jukumu la kila Mwananchi kuhakikisha misitu hii inalindwa na kutunzwa. Nawakumbusheni wananchi kuhakikisha wanatunza mazingira na kuacha vitendo vya uchomaji moto ovyo katika mkoa wetu wa Kagera badala yake wanatakiwa kuwa walinzi mazingira katika maeneo yao.
Imetolewa na; Mhe. Meja Jenerali (Mst) Salum M. Kijuu
Mkuu wa Mkoa
KAGERA

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANZIBARI BOSTON

$
0
0
Na Mwandishi wetu Boston 
Karibuni wapenzi Wasomaji wetu katika sehemu ya nne ya mfululizo wetu wa makala ya "Maalim Seif azungumza na Wazanzibari Boston" katika mkutano wake na Wazanzibari uliofanyika katika jimbo la Massachusetts, Marekani 30 Julai 2016.
Katika sehemu iliyopita, Maalim Seif alielezea kile kilichotokea katika uchaguzi wa Oktoba, 2015 mpaka uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016. Sasa endelea na sehemu ya nne:
Baada ya Uchaguzi wa Marudio
Kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, hakikupata uungwaji mkono tangu ndani hadi nje ya visiwa hivyo. Jamii ya Kimataifa ilikataa kushiriki katika uangalizi wa uchaguzi huo kwa vile haukuwa na mashiko yoyote ya Uhalali.
Na kwa upande wa ndani, Chama Kikuu cha upinzani Cha Wananchi (CUF) ambacho kiliususia uchaguzi huo hakikuitambua serikali mpya iliyoundwa na Mheshimiwa Ali Mohammed Shein, na kikaamua kuisusia kama kilivyoususia uchaguzi wenyewe.
Maalim Seif alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wameigomea serekali hiyo na sasa iko taabani, na kusisitiza: "Na wala hatushirikiani nayo kwa jambo lolote lile" Aliendelea kuelezea kuwa CUF walikaa kimya kwa muda, jambo ambalo liliwafanya viongozi wa chama Tawala cha CCM waamini kuwa wamemaliza Simba wa Nyika. "Tulikaa kimya kwa muda na wao wakadai CUF tumeimaliza......, mpaka tulipoanza ziara za Wilaya mbalimbali Unguja na Pemba zikifuatiwa na kuwatembelea wagonjwa..."
Ni vizuri kukumbusha kuwa Maalim Seif alianza ziara zake hizo kwa kuzitembelea wilaya za Pemba ambako alipokelewa na halaiki ya wananchi waliokuwa wakisema "raisi..raisi...raisi". Kufuatia ziara hizo aliitwa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na kuhojiwa kwa muda wa masaa kadhaa.
Mgomo wa wananchi umeimarika, na umekuwa ukiitikisa serikali na kupelekea ukamataji ovyo wa wananchi kinyume na sheria: "Wameghumiwa, mgomo wa wananchi umeshika kasi...., wakaanza kukamata watu kinyume cha sheria" alisisitiza Maalim Seif.
Badala ya kushughulikia maendeleo ya nchi, serikali imejikita kwenye mikakati ya kuimaliza CUF na wafuasi wake. Hata hivyo, mikakati hiyo imekuwa ikiwaathiri wananchama wa CCM pia. Alitoa mfano wa sakata la kukamatwa ng'ombe na wenyewe kutakiwa kwenda kuwagomboa.
"Kila wanachofanya ni kuwamaliza CUF, lakini ukweli ni kwamba wenye ng'ombe wengi ni wanachama wa CCM", alisema . Maalim Seif aliendelea kufafanua juu ya dhulma wanazofanyiwa raia na mali zao na kutoa mfano wa "jumba la treni", kwa kusema "Watu walihamishwa, kwa ajili ya ukarabati wa jengo lile, na mpaka leo hata ramani haipo" Itakumbukwa kuwa michoro ya kile kinachodaiwa kuwa ni ramani mpya ya mwonekano wa jengo hilo litakavyokuwa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Maalim Sif, ilikuwa ni kiini macho tu.
Aidha Maalim Seif alifafanua kuwa Mji Mkongwe ni sehemu ya Turathi za Kimataifa. Kwa hivyo uvunjaji wa jengo lolote la kihistoria unapaswa kupata ridhaa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni. Hata hivyo, mpaka wakati tunaingia mitamboni hakuna karatasi yoyote inayoonesha kuwa tayari Serikali ya Zanzibar imewasiliana na kushauriana na shirika hilo. Kwa hivyo ni wazi kuwa uhamishwaji wa wanachi kutoka jengo la treni ulikuwa na malengo ya kisiasa na kuwadhalilisha wananchi.
Upande wa Tanzania.
Kwa vile Tanzania ni Jamhuri ya Muungano nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar, yanayotokea upande mmoja yanaathiri upande mwengine wa Muungano huo kwa njia moja au nyengine. Kwa hivyo, Makamo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, hakusahau kuigusia hali ilivyo nchini Tanzania chini ya Utawala wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Maalim Seif aliilezea hali ilivyo nchini Tanzania kisiasa kuwa si yakuridhisha, na serikali iliyopo madarakani inaipelekea nchi pabaya.
Maalim Seif alikosoa hatua ya kuzuiliwa vikao vya Bunge kuonehswa moja kwa moja kwenye televisheni, na kusema lengo lake kuu ni kuua upinzani. Hii ni kutokana na kuwa Bunge lenye mijadala huru ndilo linalojenga upinzani.
Akakosoa hatua ya Wabunge 11 wa upinzani kuzuiliwa kushiriki katika vikao vya Bunge bila ya sababu yoyote ya kimsingi: "Nini kosa lao?, alihoji Maalim Seif, na kujibu mwenyewe kuwa: "Kosa lao kubwa ni kuikosoa Serikali".
Alielezea masikitiko yake kuwa majimbo ambayo Wabunge wao wamezuiliwa yatakosa uwakilishi Bungeni kwa muda mrefu kwani wengine wamefungiwa mpaka mwezi wa Januari mwakani.
Akijibu swali iwapo kuna Mbunge yeyote wa CUF kati ya 11 waliofungiwa, Maalim Seif mwenye upeo wa kuona mbali alisema kuwa hakuna Mbunge yeyote kutoka chama hicho kati ya hao walioathirika na hatua hiyo na kusisitiza: "Nia ni kuugawa upinzani, ili waseme kuwa CUF ni wasaliti"
Alifafanua kauli hiyo kwa kusema kuwa kuna Wabunge wengi wa CUF ambao ni wasemaji wazuri na wakosoaji wakubwa wa Serikali, lakini hawakufungiwa ili watu wenye nyoyo dhaifu waone kuwa CUF ni wasaliti, au vibaraka.
Aidha, mwanasiasa huyo shupavu, aliifananisha hali ilivyo Bungeni na uwanja wa vita kutokana na kuwepo kwa askari wengi ambao mara kadhaa wamekuwa wakiingia ndani ya Bunge."Ukienda Bungeni utadhani uwanja wa vita", alisema.
Alitoa mfano wa nchi kama Uturuki amabko kumetokea mitafatuku Bungeni, lakini hakuna Polisi aliyeingia ndani ya Bunge. Halkadhalika Maalim Seif alielezea wasiwasi wake mkubwa juu ya matumizi mabaya ya Sheria ya Mtandao (Cyber Act) nchini Tanzania.
Aliendelea kwa kuelezea kutoridhishwa kwake na jinsi rais Magufuli anavyoingilia kazi za Mawaziri wake, akitoa mfano wa matamshi ya vitisho aliyoyatoa Mheshimiwa Magufuli dhidi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukhusu tangazo lao la kutisha mikutano ya nchio nzima mnamo tarehe mosi Septemba. "Swali kama hilo umwachie Waziri wako wa Mambo ya Ndani kuingiulia", alisema Maalim.
Kukhusu amri ya kuhamia Dodoma, Maalim Seif alisema kuwa hakuna umuhimu wowote wa kuhamia Dodoma kwa lazima, na kukosoa kauli za vitisho za rais Magufuli dhidi ya watendaji amabao hawataki kuhamia Dodoma waache kazi, na kuelezea khofu yake kuwa hakuna maandalizi ya kutosha."Maandalizi gani yamefanywa?" Alihoji Maalim Seif.
Alielezea wasiwasi wake juu ya upatikanaji wa huduma muhimu katika mji wa Dodoma: "Sote Dodoma tunaijua..., kuna watu wana watoto wanakwenda shule, halafu uwaambie wahame kwa ghafla, rais anapohama ni lazima Mabalozi wamfuate, watakaa wapi Mabalozi?" alihji Maalim Seif.
"Kwa hiyo, hivyo ndivyo Tanzania inavyoendeshwa, ninaposema uvunjaji wa haki za binadamu, siyo Zanzibar tu, bali ni Tanzania kwa ujumla" alisema na kuonya kuwa Visiwani kukichafuka, Bara pia kutaathirika" Akijibu swali kukhusu Masheikh wa UAMSHO walioko gerezani Tanzania Bara, Maalim Seif alijibu kwa kusema: "Hatukuona sababu yoyote ya kupelekwa Bara", na kendelea kuwa Mahakama ya Zanzibar ina mamlaka ya kisheria kuwahukumu watu wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali, bila kuwajibika kuwapeleka Bara.
Aliongeza kuwa: "Kama wana makosa, wangeshtakiwa Zanzibar", akisistiza: "Huu ni udhaifu wa serikali iliyopo, kila lisemwalo na Bara, wao hewallah" Ni vizuri kukumbusha kuwa, Masheikh kadhaa wa Jumuiya ya UAMSHO kutoka Zanzibar walikamatwa na kupelekwa Bara bila kufunguliwa mashtaka katika Mahakama za Zanzibar, jambo ambalo lilizusha mjadala wa kisheria.
Masheikh hao wanatuhumiwa kwa makosa ya kile kinachoitwa ugaidi, na kwa muda wa miaka kadhaa sasa wako rumande na wamenyimwa dhamana kwa madai eti upepelezi bado unaendelea. Hata hivyo Wazanzibari wanaamini kuwa Waumini hao hawana hatia yoyote sipokuwa msimamo wao imara wa kutetea hadhi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania, khususan ikizingatiwa kuwa walikuwa msitari wa mbele katika kutetea mamlaka kamilii ya Zanzibar wakati wa mchakato wa Katiba mpya iliyofeli ya Tanzania.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI COTWU (T) KANDA YA DAR ES SALAAM CHAFANYA MKUTANO WAKE MKUU HOTELI YA VILA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shanes Nungu (katikati), akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mussa Mwakalinga na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine.


Wanawake waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanawake wajumbe wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano huo.
Vigogo wa chama hicho wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine, Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa mshikamano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.
Wajumbe wakionesha mshikamano wao wakati wakiimba wimbo maalumu wa mshikamano.
Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo akizungumza katika mkutano huo.
Makatibu wa matawi wa chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania (CMA), Shanes Nungu (wa tatu kushoto).
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi.

MAONESHO YA NANE NANE MKOANI KAGERA YAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA MKOA NA KUKEMEA VIKALI VITENDO VYA UCHOMAJI MOTO HOVYO KAGERA

$
0
0
Maonesho ya Wakulima ya Nanenane ya mwaka huu 2016 Mkoani Kagera tayari yamezinduliwa  rasmi na Mkuu  wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika uwanja wa kilimo wa Kyakairabwa uliopo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba.

Akifungua Maenesho hayo Mhe. Kijuu Agosti 3, 2016 alitembelea mabanda na bustani mbalimbali za vipando vilivyoandaliwa na wadau mbalimbali wa kilimo, mifugo na uvuvi ambao ni kutoka katika Mkoa mzima wa Kagera zikiwemo Halmashauri za Wilaya zote za Kagera.

Aidha Mhe. Kijuu mara baada ya kutembelea shughuli za wadau wa kilimo, Mifugo na Uvuvi  aliongea na wananchi walihudhuria katika maonesho hayo na kutoa wito kwa wananchi ambao hawajafika katika viwanja hivyo kufika ili kujifunza shughuli mbalimbali za kilimo cha kisasa katika kujikomboa na umasikini kwa kutumia eneo dogo na kulima kwa tija.
Kaulimbiu ya maonesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu 2016 ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni Nguzo ya Maendeleo, Vijana shiriki kikamilifu Hapa kazi tu.” Akisistizia Kauli mbiiu hiyo Mhe. Kijuu aliwakumbusha vijana kushiriki katika shughuli za kilimo, ufugaji wa kisasa na ufugaji wa samaki ili kujiajili na kuacha kulalamika kuwa hakuna ajira.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa alitoa agizo kwa Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha wadhibiti vitendo vya uchomaji moto ambapo vitendo hivyo vimekithiri mkoani hapa kwa kuchoma mashamba ya misitu ya hifadhi, misitu ya kupandwa na mashamba ya wananchi hasa kwa kipindi cha miezi miwili ya Juni na Julai 2016.

Wakuu wa Wilaya waliagizwa pia kuhakikisha wanawasimamia viongozi katika ngazi zote na kuwabaini wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uchomaji moto na kuwachukulia hatua kali za kisheria aidha, Kwa viongozi ambao hawatawajibika watachukuliwa hatua kali za kisheria wao wenyewe.
Agizo la pili la Mkuu wa Mkoa wa Kagera lilikuwa ni kuhusu Wanansiasa kufanya mikutano katika maeneo yao na si viongozi wa kisiasa kutoka katika maeneo mengine kwenda sehemu zisizo kuwa zao na kufanya mikutano ya kisiasa na kuwasumbua wananchi katika shughuli zao za maendeleo ambapo Mhe. Kijuu alisema hatakuwa tayari kuwavumilia viongozi wa namna hiyo katika mkoa wake.
Pamoja na kufungua rasmi maonesho ya Nane Nane Mkoani Kagera pia Mkuu huyo wa Mkoa alizindua wiki ya Unyonyeshaji Kitaifa ambayo inaadhimishwa Mkoani Kagera ambapo maonesho yake, Elimu na ushauri vinatolewa katika uwanja huo wa Kyakailabwa na kilele chake kitakuwa ni Julai 7, 2016.

WANANCHI WAZIDI KUFURAHIA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI

$
0
0
Mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho ya Kilimo na Mifugo ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika kwenye uwanja wa Taso Themi akipata maelezo kwenye banda la kampuni ya Simba Cement

Meneja Mauzo wa Simba Cement mkoa wa Arusha,Christopher Mgonja(kulia)akimkabidhi mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo,Thomas Mollel kofia na tisheti .

Bwana Shamba wa kampuni ya mbegu ya Seed Co,Lukinga Miho akizungumzia kampuni hiyo kuanza kuzalisha mbegu za mbogamboga ambazo zina soko kubwa ndani na nje ya nchi.

Wananchi wakipata maelezo ya kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwenye banda la taasisi ya TAHA inayojihusisha na kuhamasisha wakulima kuzalisha kwa wingi kwaajili ya soko la ndani na masoko ya Ulaya .

Wananchi wakipata elimu ya kilimo kwenye uwanja wa maonesho ya Wakuma na wafugaji Kanda ya Kaskazini  uwanja Taso, Themi mkoani Arusha.

Wajasiriamali hawakua nyuma kwenye banda la Halmashauri ya Jiji la Arusha kuonyesha bidhaa zao kwa wananchi waliotembelea maonesho ya mwaka huu.

Wanafunzi nao ni sehemu ya wananchi wanaotembelea maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane pamoja na mambo mengine hujifunza mambo mengi yanaendana na masomo yao kwa vitendo.

Maafisa wa Benki ya NMB mjini Arusha wakitoa huduma kwa wananchi wanaofika kwenye banda lao.

STARTIMES YACHANGIA MADAWATI MKOANI MTWARA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakiwa kwenye baadhi ya madawati yaliyochangiwa na kampuni hiyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati nchi nzima iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Zoezi hio la uchangiaji wa madawati lilifanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mwishoni mwa wiki hii.


 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakiwa wamekaa kwenye madawati hayo. 

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura (kulia) , akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mh. Dkt. Khatib Malimi Kazungu
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo.

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Bi. Anastazia Wambura amepokea madawati hamsini yenye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kwa kampuni ya matangazo ya dijitali ya StarTimes ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki moani Mtwara, Mh. Bi. Wambura amebainisha kuwa zoezi la kuchangia madawati ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri linawahusu watu wote na sio serikali pekee.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuzipongeza taasisi za umma na sekta binafsi kwa mwitikio wao mkubwa wa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika kampeni ya kuchangia madawati. Wote tunafahamu ni kwa kiasi gani shule nyingi nchini zinavyokabiliwa na uhaba wa madawati jambo linalopelekea mazingira magumu ya kufundishia na kujinzia. Lakini kwangu mimi suala la wanafunzi kuongezeka sioni kama ni tatizo bali ni changamoto kwa serikali yetu na jamii kwa ujumla kuendana na mwamko mkubwa wa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule. Kwa muda mrefu sana serikali imekuwa ikiwahamasisha wananchi wake wawapeleke watoto shule na wakafanya hivyo, sasa suala hilo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa na vivyo jinsi walivyoitikia mwamko huo basi waitikie na wa huu wa kuchangia madawati.” Alisema Mh. Bi. Wambura

Naibu Waziri huyo aliendelea kwa kuelezea kuwa serikali ina wajibu wa kuhamasisha maendelea kwa wananchi wake kwa njia mbalimbali ikiwemo hii ya kuwasilisha maeneo ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele kama vile suala la elimu nchini.

“Elimu ndio suala la msingi katika taifa lolote duniani iwe lililoendelea au linaloendelea na ndio maana kwa nchi za wenzetu wanawekeza fedha nyingi katika sekta hii. Nchi yoyote yenye wasomi wengi lazima itakuwa na maendeleo makubwa kutokana na raia wake kuelimika lakini hayo yote haya hayatowezekana kama tusipowawekea mazingira mazuri wanafunzi wetu tangu ngazi ya msingi,” alisema Mh. Naibu Waziri na kumalizia, “Ningependa kumalizia kwa kuwapongeza na kuwashukuru wenzetu wa kampuni ya StarTimes kwa kuguswa na suala hili na kuamua kuja huku Mtwara kuchangia madawati kwani huku ndiko kwenye changamoto kubwa hasa kutokana na taasisi na makampuni mengi kuwepo sehemu za mijini. Tunawashukuru sana na tunawaomba muendelee na moyo huo huo na mfike sehemu nyingine amabko makampuni mengine hayafiki.”

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ni mdau mkubwa wa masuala ya kijamii hususani elimu kwa inafahamu umuhimu wake katika kuleta mapinduzi ya kimaendeleo.

“StarTimes ni mdau mkubwa sana wa masuala ya elimu na kwa muda mrefu tumekuwa tukisaidia shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Uchangiaji wa madawati ni kampeni ya aina yake iliyoanzishwa na Mh. Rais Magufuli na inahitaji kuungwa mkono kwa nguvu zote kwani yeye aliamini kabisa watanzania tunao uwezo huo ila tulikosa tu uhamasishaji. Na ni kweli uhamasishaji ndio uliokosekana kwani mara baada ya kutoa tamko hilo taasisi, makampuni, mashirikia, wananchi na watu binafsi wameonyesha mwitikio mkubwa. Hii ni dalili njema kwamba watanzania tunaweza kuleta maendeleo yetu wenyewe bila ya kungojea msaada kutoka kwa watu wa nje.” Alisema Bi. Hanif

“Leo hii tumekuja huku Mtwara kuja kukabidhi madawati haya, tunafahamu kwamba ni machache lakini yatakuwa ni msaada mkubwa kwa watoto wetu kusoma katika mazingira mazuri. Wanafunzi wanaposoma katika mazingira mazuri hupelekea kuhudhuria vipindi, kuipenda shule, kuelewa vizuri na hatimaye kupelekea kufaulu masomo yao,” alisema na kuhitimisha Bi. Hanif kuwa, “Wananfunzi wanapowekewa mazingira mazuri ya kusomea pia hutoa hamasa kwa walimu kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa kwani ufundishaji unakuwa ni rahisi na vivyo hivyo uelewa kwa wanafunzi. Hivyo basi, ningependa kutoa wito kwa wanafunzi wayatunze madawati haya ili yaje kuwanufaisha na wenzao watakaokuja siku za usoni na tunawaahidi kuwa tuko pamoja nao katika kutatua changamoto zinazowakabili.”

MJINI BUKOBA :MASHINDANO YA POOL TABLE YA NANE NANE KUFANYIKA LEO NEW COFFEE TREE HOTEL

$
0
0
Mashindano ya Pool Table ya Nane nane (“88” Pool Competition 2016) yanatalajia kufanyika leo Jumatatu Aug 8 @New Coffee Tree Hotel kuanzia majira ya Saa 8 Mchana. Wadau wa pooltable mnakaribishwa sana kushuhudia mchezo wa leo utakao wakutanisha wachezaji wakali wenye uwezo wa kutoa kichapo vizuri tu!!
Chini ya Udhamini wa Mkurugenzi wa KCC ,New Coffee Tree Hotel na Bukobawadau Media

 Mr. Rama na Mr Matete katika hili na lile
 Mdau Steven Porotas pichani kulia katika hali ya sintofahamu
Pichani kshoto ni Mchungaji anayewaza kuyaaga mashindano hayo mapema...
 Wadau wa pooltable mnakaribishwa sana kushuhudia mchezo wa leo utakao wakutanisha wachezaji wakali wenye uwezo wa kutoa kichapo vizuri tu!!
Chini ya Udhamini wa Mkurugenzi wa KCC ,New Coffee Tree Hotel na Bukobawadau Media

 Coffee Tree hoteli inatoa huduma nzuri ya vyumba vya kulala kwa mtu mmoja mmoja, wawili wawili au zaidi,Vyumba vyake vinatazama mandhari nzuri ya milima ya Kashura.
Taswira mbalimbali muda mchache kabla ya mashindano hayo kuanza rasmi mchana wa leo Aug 8,2016
Mgahawa wa Coffee Tree hoteli unaoitwa hutoa huduma ya vyakula mbalimbali, vinavyotolewa ama ndani au nje kwenye eneo la wazi lenye hewa safi na upepo mzuri utokao milimani na ziwani Huduma katika mgahawa huu ni pamoja na kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni/usiku. Vyakula hivi ni vya mapishi ya Kiafrika, Kihindi, Kichina, Kimataifa,
na vinginevyo vya kimataifa ambavyo hutayarishwa na wapishi wataalamu katika jiko lenye vifaa mbalimbali vya kisasa.

JESHI LA POLISI NCHINI KUVIFUNGA VYUO VYA UDEREVA VISIVYO NA SIFA

$
0
0
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (wa pili kushoto), akizungumza na wamiliki wa shule za udereva (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta), Hoteli ya Dreamers Buguruni Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla na Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati
 Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla (katikati), akimkabidhi risala yao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni. 


Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.

 Mkutano ukiendelea.
 Mjumbe wa chama hicho, Cosmas Munuo (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
 Mjumbe wa chama hicho, Regina Sulle akiuliza swali kwenye mkutano huo. Kushoto ni mjumbe Fatma Somji na kulia ni Santos Akyo.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (kushoto), akisisita jambo wakati akijibu maswali ya wanachama wa chama hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla.
 Mjumbe wa mkutano huo, Leonard Mtandika akiuliza swali. Kutoka kulia ni Pascol Mtandika na Ibrahim Nyato.
 Mjumbe wa Mkutano huo kutoka mkoani Dodoma, Robert Mwinje (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.. Kushoto ni mjumbe mwenzake,kutoka mkoani Mwanza, Mussa Ramadhan.
 Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni (kulia), akifafanua baadhi ya vifungu vya sheria katika mkutano huo.


Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Mgeni rasmi, DCP Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo ambao ni wanachama wa Chashubuta.
Hapa DCP Mpinga akiagana na wajumbe hao baada ya kufungua mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na  sifa.

Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es Salaam leo.

"Kuanzia sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.

Mpinga alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa na madereva.

Alisema jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havisa sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

Mwenyekiti wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya serikali pekee.

Mkolla alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili kwenda na mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.

JAMII FORUMS YAZINDUA RASMI MRADI WA 'TUSHIRIKISHANE'

$
0
0
Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisha upatikanaji wa maendeleo.

Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.

Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.

Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.
 Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.

Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.

Malengo ya Tushirikishane

Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:
i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)
ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi
iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao
iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.​

Matarajio ya Mradi

Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:

i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii
ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.​

JamiiForums itakuwa inakuletea matukio yote kuhusiana na mradi huu kwa kadiri utekelezaji wake utakavyokuwa unaenda katika kila Jimbo.
 Timu ya Jamii Media ikitambulishwa mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bukoba.
 Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja
 Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja
 Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Mwakyoma akiwasilisha kundi lake juu ya Wajibu wa Mbunge kwa wapiga kura wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani Al Masoud Kalumuna(katikati) ambaye ni diwani wa Ijuganyundo (CCM) na Noorhodah Kabaju (kulia) ambaye ni diwani wa Kashai(CHADEMA)
Mh. Lwakaare Mbunge wa Bukoba Mjini, akishirikiana na wapigakura wa Jimbo lake katika zoezi la kuchambua kazi na wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.
 Washiriki wakifuatulia maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
 Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.
 Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura
 Meya wa Manisapaa ya Bukoba Chief Kalumuna (kushoto) Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.
 Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane katika Jimbo la Bukoba Mjini wakiwa katika picha ya pamoja.

 

NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA AZINDUA RASMI MAFUNZO YA KKK KWA WALIMU 1770 MKOANI KAGERA

$
0
0
Mhandisi Stella Manyanya Akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole Wakiwasikiliza Walimu wa KKK
 Mhandisi Stella Manyanya Mara Baada ya Kuzindua Rasmi Mafunzo ya KKK Kagera Akishuka Ngazi kuondoka.JPG
 Naibu  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Stalla Manyanya Akitoa Hotuba ya Uzinduzi
 Walimu Waliohudhuria Mafunzo ya KKK Mkoani Kagera Wakiimba Wimbo wa Mbele ya Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
Walimu Waliohudhuria Mafunzo ya KKK Mkoani Kagera Wakiimba Wimbo wa Mbele ya Mhe. Mhandisi Stella Manyanya


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya azindua rasmi mafunzo ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa walimu 1770 wa Shule za Msingi 885 za Halmashauri nane za Mkoa wa Kagera  wanaofundisha masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati kwa darasa la tatu na la nne.
Akizindua mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Veta Mkoani Kagera kilichopo katika Manispaa ya Bukoba Mhandisi Manyanya aliwapongeza walimu waliohudhuria awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 1, 2016 kutoka katika Halmashauri za Wilaya za Karagwe na Bukoba kwa kuitikia wito wa mafunzo hayo kwa asilimia 99%.
Pia aliwasistiza walimu hao kuzingatia mafunzo kwa umakini kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha walimu hao wanatoa elimu bora kwa wanafunzi ambapo mwanafunzi yeyote hawezi kupata elimu iliyobora kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) masomo ambayo ndiyo msingi wa kujifunza.
Mhandisi Manyanya alisema kuwa mafunzo ya (KKK) yanaendeshwa katika mikoa 19 ya Tanzania Bara na jumla ya walimu 22995 watapatiwa mafunzo hayo ukiwemo Mkoa wa Kagera utakaonufaika kwa mafunzo hayo kwa walimu 1770 ambao wanatarajiwa kuwanufaisha pia walimu wenzao kwa mafunzo hayo ya (KKK) pindi warejeapo shuleni kwao.
Ombi, Mhandisi Manyanya aliwaomba walimu hao pia kuanzisha madarasa ya watu wazima ili kutoa fursa kwa wananchi ambao hawakuweza kupata elimu ya msingi ili na wao wafundishe kusoma, kuandika na kuhesabu. “Kwa takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ilionekana kuwa bado asilimia 29% ya wananchi kuanzia umri wa miaka 8 hadi 50 hawajui kusoma na kuandika kwahiyo nawaombeni sana tusaidiane kuondoa tatizo hili nchini kwetu.” Aliwaomba walimu hao Mhandisi Manyanya.
Aidha, Mhandisi Manyanya alibainisha kuwa nia ya Serikali ya kujenga Chuo cha VETA cha kisasa Mkoani Kagera katika eneo la Burugo bado ipo palepale kwani imetengwa fedha katika bajeti yake ya mwaka 2016/17 ili watoto watakaokuwa wanamaliza elimu ya Msingi na Sekondari wakapate ujuzi wa ufundi chuoni hapo.
Katika Hatua Nyingine Bw. Benard Merumba Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu Bagamoyo (ADEM) alisema  mafunzo ya (KKK) yanalenga kuwafundisha walimu kutambua na kuelewa Sera mpya ya Elimu ya Mwaka 2016, Kuitambua na kuielewa miongozo ya kufundishia masomo husika.
Vilevile walimu kukutambua mbinu sahihi za kujifunza na kufundisha pamoja na upimaji wa ufanisi wa mada zinazotolewa kwakutumia mbinu shirikishi. Bw.Merumba alisema pia kuwa mafunzo hayo yanaendeshwa na wakufunzi 32 kutoka katika vyuo mbalimbali nchini.
Naye Mwalimu Fides Mnyogwa alisema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuliona hilo na kutoa mafunzo hayo hasa kuhusu mitaala kwa walimu wanaofundisha masomo ya Kiswahili, kiingereza na Hisabati kwani hapo awali walimu walikuwa wanafundisha wanavyojua kila mmoja, lakini mara baada ya kupata mafuzo hayo sasa watapata uelewa wa pamoja na kufundisha kwa mbinu sahihi za aina moja.
Mafunzo yanatarajia kukamilika Septemba 15, 2016 mara baada ya Walimu kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera kupata mafunzo hayo ya (KKK).

MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AFANYA ZIARA YA KUSHUTUKIZA KATIKA MRADI WA MAJI KUONA KAMA ALIUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA WATENDAJI

$
0
0
Mhe. Kinawilo wa2AA Pili Akiongozwa na Mhandisi Mtagaywa wa Kwenda Kuhakiki Tenki la Maji Juu.
 Mhe. Kinawilo (wa pili kutoka kulia) aliyeshika Viungio vya Maji Akimhoji  Bw. Dismas Martin Juu ya Ubora wa Viungio vya Mabomba.
 Mhe. Kinawilo Akiwahoji Diwani wa Kata Nyakibimbili Mwenye Baragashia Haji M. Juma na Anayefuata Mwenyekiti wa Kijiji Kitahya Bw J. Kahigwa.JPG
 Tanki Dogo Linalokusanya Maji  Katika Chanzo
 Mhandisi Mshauri Mwesigwa Mtagaywa aliyeinama Akimwonyesha Mhe. Kinawilo Mabomba Yaliyokatwa na Wananchi kama hujuma ya Miundombinu ya Mradi.
Mhe. Deodatus Kinawilo (wa pili kutoka kushoto waliosimama juu ya Tenki) Mara Baada ya Kuhakiki kuwa Pampu Imo ndani ya Tenki
 Tanki Dogo Linalokusanya Maji  Katika Chanzo.


Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo afanya ziara ya kushutukiza katika Kata Nyakibimbili Kijijini Kitahya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba leo Agosti 9, 2016 katika chanzo cha maji kilichopo kijijini hapo ili kuhakiki kama pampu ya kusukuma maji  kama ilifungwa na ipo katika tenki la maji lilojengwa katika chanzo hicho cha maji.
Mkuu huyo wa Wilaya aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuletewa malalamiko na wananchi kuwa siku mradi huo ulipowekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. George Mbijima Julai 27, 2016 maji yaliyotoka katika ghati la Ibwera yalijazwa kwenye tenki na gari la kubebea maji  kwani pampu ya kusukuma maji haikuwepo katika tenki lilipo kwenye chanzo cha maji.
Baada ya kufika katika chanzo hicho cha maji Mhe. Kinawilo aliyeongozana pia na Kaimu  Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bw. Gregory Fabian,  Mhandisi wa Maji Bw. Dismas Martin, na Mhandisi Mshauri wa Mradi huo Mwesiagwa Mtagaywa wa Kampuni ya (O & A Company Ltd.) alikagua mradi huo na kugundua kuwa pampu ipo na inafanya kazi vizuri ya kusukuma maji.
Aidha, iligundundulika kuwa maji mara baada ya  kusukumwa kutoka kwenye tenki  umbali wa mita 22 kutoka kwenye tenki hilo bomba limekatika kiungio jambo linalosababisha maji kutopanda hadi katika Kata ya Ibwera ambapo Mhe. Kinawilo alimuagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha anamshauri Mkandarasi kufanya marekebisho ya haraka nadani ya wiki moja.
Aidha , katika mradi huo kuliibuliwa suala la wananchi kukata mabomba ya maji katika chanzo hicho na kusababisha maji kutoenda katika tenki linalohudumia vijiji vitatu vya Kitahya, Kibona na Itongo na kusababisha Diwani wa Kata ya Nyakimbimbili Haji Matsawilly Juma kulalamika kuwa maji hayawafikii wananchi na kumwomba Mkuu wa Wilaya kumhimiza Mkandarasi kumaliza kazi ili maji yatoke kwa wananchi kama ilivyotarajiwa.
Maagizo, Mhe. Kinawilo baada ya kushuhudia uharibifu huo alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha Mkandarasi anafunga vifaa vyenye ubora ili thamani ya vifaa iendane na gharama za mraddi huo. Pili alimwagiza Mwenyekiti wa Kijiji Kitaya   Bw.Johnstone Kahigwa aliyedai kuwa kijiji hakikukishirikishwa tangu mwanzo wa mradi kuhakikisha anashirikiana na Halmashauri ya kijiji chake kuilinda miundombinu ya mradi huo kwa sababu mradi upo katika eneo lake.
Vilevile Mhe. Kinawilo alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhikikisha anfanya marekebisho yote ya mradi huo ndani ya wiki moja ili wananchi waanze kupata huduma ya maji. Na mwisho aliwaagiza Watendaji wa Kata za Ibwera na Nyakibimbili kuititsha mkutabno wa pamoja kwa kamati za maji za Vijiji vya Kitaya, Kibona,Itongo na Ibwera ili kuweka mikakati ya kuilinda miundombinu ya mradi huo wa maji.
Mradi huo wa maji ukikamilika unatarajiwa kuhudumia vijiji vinne vya Kitaya, Kibona,Itongo  (Kata Nyakibimbili)na Ibwera (kata Ibwera) una gharama ya zaidi ya shilingi milioni 430 na ulianza katika awamu ya kwanza mwaka 2009 katika upembuzi yakinifu na usanifu, aidha utekelezwaji wake ulianza rasmi  katika awamu ya pili iliyoanza Mwezi Julai, 2013.
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>