Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Busisi wakati akielekea Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV. Misungwi wakati akielekea mkoani Mwanza.
 PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA MAELFU YA WANANCHI WA JIJI LA MWANZA UWANJA WA FURAHISHA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo.

PICHA NA IKULU

MH.LWAKATARE ATEMBELEA JIMBO LAKE NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO LEO AUG 11.

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mh. Lwakatare leo Alhamis Aug 11, ameongozana na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF) kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo itokanayo na mfuko huo na miradi mingine inayohitaji msukumo na kuongezewa nguvu kutoka Serikalini.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba,Chief Kalumuna akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mh.Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare
Mh. Lwakatare akiongea mbele Uongozi wa Shule ya Msingi Kyaikalabwa na wajumbe wa kamati ya Mfuko wa Jimbo alio ongozana nao ambapo shule hiyo uliweza kupokea jumla ya madawati 40
Mh. Lwakatare akisalimia na kumpongeza Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyanda Leonard L.Kamuzora pichani kushoto
Mh. Chief Kalumuna akitoa neno la shukrani kwa Mh. Lwakatare kwa ushirikiano mkubwa anao endelea kuonesha ndani ya Jimbo lake
Pichani anaonena Bwana Alex ambaye ndiye Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini
Muonekano wa Madawati 40 kutoka katika fedha za Mfuko wa Jimbo
Pichani ni Kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Buhembe , Amfle Mbese akikabidhi taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Jimbo kwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mh. Lwakatare 
Mradi wa kuinua Vyumba Viwili vya Madarasa katika shule ya Msingi Buhembe
Muonekano wa ndani ya Chumba cha Darasa kilichokamilika kutoka na fedha za Mfuko wa Jimbo,katika shule ya Msingi Buhembe
 Bwana George Bwatani Diwani wa Kata ya Nyanga akielezea utekelezaji wa mradi wa fedha za Mfuko wa Jimbo
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba,Chief Kalumuna pichani kushoto
 Mh. Regna Diwani wa Viti Maalum
 Madhari kuzunguka mazingira ya shule ya Msingi Buhembe
 Mazingira ya shule ya Msingi Buhembe
 Mmoja wa walimu ya shule ya Msingi Buhembe
 Diwani wa kata ya Kashai Mh. Kabaju N. Abdulkadir

 Taarifa ya fedha ya Mradi wa Mfuko wa Jimbo katika kata ya Rwamishenye
 Taarifa ya kupokea madawati  yatokanayo na fedha za mfuko wa Jimbo katika shule ya Msingi Kyakailabwa
 Taarifa ya matengenezo ya Mradi wa Barabara ya Makongo katika kata ya Kahororo
Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Mfuko wa Jimbo katika kata ya Bakoba
Hii ni taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Ununuzi wa Madawati pamoja na kuinua Vyumba Viwili vya Madarasa katika shule ya Sekondari Kibeta.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Makongo akitolea jambo ufafanuzi
Mh. Mbunge akiendelea kukagua maeneo mbalimbali
Fukweni Karobela Kahororp
Mh. Chief Kalumuna akitoa Ishara kuhusu ya jambo fulani
 Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mh. Lwakatare akielezea fursa za uwekezaji zinazoweza kupatikana katika eneo hilo kutokana na uwepo wa barabara inayopitika Vizuri
Katikati ya mtaa wa Makongo katika kata ya Kahororo
 Matengezo ya barabara yakiendelea katika kata ya Kahororo,kata yaMstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba,Chief Kalumuna


Wananchi wa Mitaa va Makongo na Bushwa vilivyopo katika kata ya kahororo
Mh. Lwakatare akiongea na Wananchi wa Vijiji va Makongo na Bushwa vilivyopo katika kata ya kahororo mapema ya leo Aug 11,wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba,Chief Kalumuna akioa ufafanuzi kuhusu mradi wa Ofisi ya Kijiji unao endelea....
 Jengo la Ofisi ya Kijiji Ujenzi ukiendelea
 Wajumbe walio ongozana na Mbunge wakimsikiliza kwa makini
 Mkazi wa Bushwa Kahororo
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mbunge wao Mh. Lwaks mapema ya leo Aug 11
 Mjumbe wa Mtaa wa Makongo pichani wakati wa Utambulisho
 Meya wa Manispaa ya Bukoba Mh.Chief Kalumuna t. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi
 Jengo la Ofisi ya Afisa Mtendaji Mtaa wa Bushwa na Makongo
 Mh. Chief Kalumuna akiwaelezea wananchi wa Mtaa wa Bushwa na Makongo namna alivoweza kama Diwani kutengeza  barabara kwa kutumia fedha zake binafsi na kumshuru Mh. Mbunge kwa kuchangia Shs  milionni moja (1,ooo,ooo)
 Mandhari nzuri yeneye kuvutia ukiwa maeneo ya Kahororo
Mh. Lwaks akifurahia mandhari na upepe wa ziwa Victoria pembezoni mwa fukwe za Kalobera kata ya Kahororo Manispaa Bukoba

SHULE ZA FEZA HAZITAFUNGWA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
UONGOZI wa  Shule za Feza nchini umeibuka na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii,  kuwa wao  hawana uhusiano na  Fethullah Gulen wala serikali ya Uturuki  kwa vile   hawajawahi kupokea misaada toka pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.
Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule za Feza  zipo hatarini kufungwa kwa madai kuwa  mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Shule za Feza ni kama asasi  zingine zilizosajiliwa kishera na serikali, hivyo ni mali ya watanzania.

“Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda  cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania  na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.

Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.
Aliongeza kuwa  huo ni uwekezaji  wenye mchango katika kukuza pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.
Alisema  wanatoa  wito kwa wazazi  kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo  kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA MAELFU YA WANANCHI WA JIJI LA MWANZA UWANJA WA FURAHISHA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo.

PICHA NA IKULU

CHRISTIAN BELLA ALIVYONOGESHA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI JIJINI MWANZA

$
0
0

 Mwanamuziki nyota Christian Bella akikonga nyoyo za maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akitumbuiza  maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akiimba mbele ya maelfu ya wananchi wa  jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
 Mwanamuziki nyota Christian Bella akipongezwa kwa kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwanamuziki nyota Christian Bella baada ya kukonga nyoyo za maelfu ya wanannchi wa jiji la Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara wa katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Ijumaa Agosti 12, 2016

AJALI YA LORI YATOKEA LEO MJINI BUKOBA AUG 14

$
0
0
Ajali ya Roli imetokea Usiku wa kuamkia leo Mjini Bukoba eneo la Rwamishenye (round about)tunaendelea kufatilia taarifa rasmi zinasema mtu mmoja amepoteza maisha
Taarifa zinasema mtu mmoja (mwanamke )ameoteza maisha baada ya kufikishwa katika Hospital ya Mkoa kutokana na kuvuja damu nyingi katika jeraha alilolipata kichwani na wengine wawili Dereva na Tingo wamejeruhiwa
Kijana akizoa pumba zilizokuwa zimepakiwa kwene Gari hilo
 Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi..

Magufuli aisifia ‘Sizonje’ ya Mrisho Mpoto, ategua fumbo la mashairi yake

$
0
0
Utunzi mahiri wa mashairi na ughani uliotukuka wa Mrisho Mpoto, umeligusa sikio la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameeleza kuwa shabiki mkubwa wa kazi za msanii huyo hususan wimbo wake ‘Sizonje’.
Akizungumza na Mpoto jana, muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli alimueleza msanii huyo kuwa anazifahamu vizuri kazi zake na kwamba anaupenda sana wimbo wake wa ‘Sizonje’ huku akichambua baadhi ya mistari iliyomo kwenye beti za wimbo huo.
Mpoto alikuwa msanii pekee aliyeongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda, Wakuu wote wa Wilaya za Dar es Saalam pamoja na viongozi wengine waliofika katika uwanja huo wa ndege kumpokea Mkuu huyo wa nchi.
“Nasikiliza nyimbo zako sana, ila huu wimbo wako wa Sizonje nimeuelewa sana na nausikiliza kila siku, kwangu umekuwa kama wimbo wa taifa, mwanzoni nilipata tabu kuuelewa lakini sasa hivi… aaaah, nimeuelewa vizuri sana. Halafu Sizonjenamjua, nimtaje?,” yalisikika baadhi ya maneno ya Rais Magufuli kwa Mrisho Mpoto.
Akielezea tukio hilo lililoleta msisimko wa aina yake uwanjani hapo, Mpoto alisema kuwa baada ya kumsikia Rais ameanza kuusifia wimbo wake alishtuka na kujawa na furaha ya aina yake kwani kwa msanii ni jambo la thamani kubwa kusifiwa kazi yake na Mkuu wa Nchi.
Alisema kuwa pamoja na kuusifia wimbo huo, Rais alionesha kuufahamu vizuri zaidi baada ya kuanza kuipitia baadhi ya mistari na kuahidi kumfumbulia fumbo lililofichwa kwenye wimbo huo watakapokutana tena.
“Unapopata thamani kutoka kwa Mkuu wa Nchi inaleta faraja sana," amesema Mpoto. "Kwahiyo, mheshimiwa Rais leo kuniambia kwamba yeye ni shabiki wa kazi zangu na kwamba anapenda sana wimbo wa Sizonje, na akafunguka kwa mistari ‘minane’ ya Sizonje ikiwa ni pamoja na ile inayosema ‘huyu mgeni anayepitia madirishani wakati milango ipo!’ Na akaniambia siku tukikutana ataniambia vile vyumba vitatu kwanini havifunguki,” ameongeza.
Msanii huyo amemshukuru Rais Magufuli kwa kuthamini mchango wake katika sanaa kwakuwa anaamini kuthaminiwa ni hitaji kubwa la kila msanii.
“Kwakweli leo ni siku yenye furaha sana. Najisikia furaha sana. Asante sana mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Umenifanya nimekuwa na siku nzuri sana,” Mpoto amefunguka kwa furaha.
Mwaka huu mwanzoni, Mrisho Mpoto aliachia audio na video ya ‘Sizonje’ aliomshirikisha Banana Zorro ambapo kwa muda mfupi tu, wimbo huo uligeuka kuwa mkubwa na kufanya vizuri. Kutokana na ufanisi wa kazi zake, Mpoto ameendelea kukubalika akipata mikataba ya ubalozi wa mashirika na taasisi kubwa nchini ikiwa ni pamoja na mfuko wa pensheni wa PSPF.

PATA SIMULIZI LA LEO

$
0
0
Baba mmoja alikuwa akila chakula kwa furaha na mke wake ambaye alikuwa siku za mwisho akijitazamia kabla ya kujifungua mtoto wao wa kwanza.
Mara mama akaanza kulalalamika maumivu ya kichwa na baba akaita gari na wakiwa njiani kuelekea hospotali yule mama akafariki.
walipofika hospitali baba akaomba mama afanyiwe upasuaji wa haraka ili waone kama mtoto aliyekuwa tumboni angeweza kupona.
Baada ya upasuaji wa haraka mtoto alitoka akiwa mzima na madaktari wakiwa wanashangaa baba aliendelea kuomba kwa Mungu akisema;
" Eeh Mungu kama umeweza kumwokoa mtoto huyu naamini pia waweza kuurejesha Afya ya mama yake
Ikiwa ni mapenzi yako naomba mke wangu kipenzi apone na kumshuhudia mwanae aliyemgojea kwa siku nyingi na hamu tele.
Ninaomba nikiamini kuwa wewe ni Mungu wa miujiza na mwenye huruma kwa sisi watoto wako AMEN"
Jopo la madaktari waliokuwa wakimsaidia yule mama wakaanza kushangaa kwa mbali mama mapigo ya moyo yakaanza kurudi na baada ya jitihada mama alipona na kila mtu mle ndani aliushangaa ule muujiza huku wakiwa na mshtuko wakamshukuru Mungu.
Sasa naomba nawe usikie maneno haya kwa makini!!!!!!
*Mungu akupe wepesi, amani na furaha kwa kila tatizo litakaloyasibu maisha yako
*Kamwe usichoke kumwomba Mungu hata kwa jambo unaloliona machoni mwako haliwezekani, kwani kwa Mungu hakuna linaloshindikana
*Kuanzia leo katika kila jambo uliloliona kuwa gumu kwako litakuja kuwa rahisi na liwezekanalo
*Kwa kila jambo lililokuwa likichelewa katika maisha yako kuanzia sasa litaanza kwenda haraka nawe utashangaa ukuu wa Mungu.
*Utafurahia mafanikio ya kila jambo na ukishuhudia miujiza katika maisha tyako.
Comment AMEN na kisha share kama unaamini katika miujiza ya Mungu kwenye maisha yako.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 16 AGOSTI, 2O16 UJIO WA WAZIRI RUKUVI

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia tarehe 18-19 Agosti, 2016.
Katika ziara hiyo Mhe. William Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera siku ya Alhamisi tarehe 18 Agosti, 2016 anatarajia kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kuanzia saa 4:10 hadi saa 4:40 Asubuhi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Aidha, kuanzia saa 5:00 Asubuhi hadi saa 10:00 alasili Mhe. Lukuvi ataongea na Wananchi wote walio na kero za ardhi ambazo zimeshindikana kutatuliwa katika ngazi za Wilaya na Mkoa aidha, wawe na viambatanisho halisi na sahihi, mkutano huo utafanyika katika Manispaa ya Bukoba.
Katika siku yake ya pili Mkaoni Kagera tarehe 19 Agosti, 2016 Mhe. William Lukuvi atazindua Balaza la Ardhi la Wilaya ya Muleba kuanzia saa 03:30 hadi saa 03:50 Asubuhi mara baada ya Wajumbe wa Baraza hilo kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika ukumbi wa Ofisi yake.
Kuanzia saa 5:50 hadi saa 08:00 Mchana Mhe. Lukuvi atazungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba, Wenyeviti wa Baraza la Ardhi, NHC na Wataalam wa Ardhi kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba.
Wito kwa wananchi wote hususani wenye kero za muda mrefu kuhusu Ardhi na zimeshindikana kutatuliwa wanahamasishwa kuhudhuria mkutano wa Waziri ili kupata utatuzi wa kero zao. Pia vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari mnaombwa kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ya Mhe. Lukuvi ili kuwahabarisha wananchi hasa wa Mkoa wetu wa Kagera juu ya yale yote yatakayojili katika ziara hiyo.
Imetolewa na: Sylvester M. Raphael (Afisa Habari)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
16 Agosti, 2016

ALI KIBA LADY JAY DEE WAFUNIKA TAMASHA LA SEREBUKA 2016 LILILOANDALIWA NA KAMPUNI YA STARTIMES

$
0
0
 Msanii, Ally Salehe 'Ali Kiba' akishambulia jukwaa wakati akitumbuiza kwenye  tamasha la kutimiza miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili tokea kuanzishwa Kwake. Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jana ambapo lilidhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.
 Msanii, Snura Mushi, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
 Msanii, Juma Kassim 'Juma Nature, akitumbuiza kwenye 
tamasha hilo.
 Msanii Stamina akipagawisha  kwenye tamasha hilo.
Wananchi wakifuatilia Tamasha la Serebula Festival la kuazimisha miaka miwili ya chanel ya startimes Swahili iliyoandaliwa na kampuni ya Bluelines kwa kushirikiana na uwawei jijini Dare s Salaam jana 



Na Dotto Mwaibale

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura Lady Jay Dee na Ali Salehe Ali Kiba wameonesha umahiri wao wa kuimba kwa kutumia 'live band' katika tamasha la Serebuka na Festival 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mashabiki walioudhuria tamashan hilo walianza kuonesha shangwe baada ya Lady Jay Dee kupanda jukaani na kuimba tungo na alioimba wimbo wa Ndindindi mashabiki walilipuka kwa vifijo.

Shangwe hizo zilidumu hata kwa msanii Ali Kiba ambapo walimtaka aendelee kuimba licha ya muda wa kuendelea na tamasha hilo kuwa umekwisha.

Ali Kiba aliwachangua zaidia mashabiki walipoimba wimbo wa Aje ambpo dakika za mwisho jukwaani hapo akapanda mwanadada na kushuka na msanii huyo na kuacha mashabiki wakishangilia kwa shangwe.

Wasanii wengine ambao walionesha uhai katika tamasha hilo, Bonivecture Kabobo 'Stamina' ambaye mashabiki walionesha kumuunga mkoano kutokana na aina ya uimbaji wake kuteka mashabiki.

Pia katika tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya King'amuzi cha Starv Times liliudhuriwa ma Juma Kasimu 'Juma Nature', Madee,Yamoto Band, Snura  na wengineo ambao waliimba kwa kutumia 'Play Back'.

Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival liliandaliwa  na Kampuni ya StarTimes na  Kudhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.

BALOZI DR.KAMALA AENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA KATA YA KITOBO AUG 16,2016

$
0
0
Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge,mkoani Kagera ameendelea na ziara yake  leo Jumanne Aug 15 Katika kata ya Kitobo na kuongea na wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara wenye lengo wa kujua kero mbalimbali na kuahidi kuzipatia ufumbuzi 
 Diwani wa Kata ya Kitobo akitolea jambo ufafanuzi.
 Mwananchi akielezea kero yake kwa Mbunge wake
 Mzee Kabandwa Rweyemamu wakati akielezea Kero yake kwa Mh. Mbunge Balozi Dr. Kamala
 Bw. Elpidius Pancrasi ambaye ni Bwana Mifugo katika katika ya Kitobo akimuelea Mbunge Balozi Dr. Kamala namna anavyotoa ushirikiano kwa wananchi ndani ya kata hiyo
 Pichani kushoto ni Bw. Daudi Buberwa Afisa Kilimo kata Kitobo
 Afisa Mipango wa Wilaya ya Missenyi akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano huo
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akipokea zawadi kutoka kwa Vikundi vya akinana wa Kata Kitobo baada ya kumaliza mkutano wake katika kata hiyo uliofanyika mapema ya leo Jumanne Aug 15 na kuahidi kuyatekeleza yaliyomo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM
Katibu wa Wazazi Wilaya ya Missenyi Mama Rehema akiwa amebeba zawadi hizo mara baada ya kukabidhiwa, Mama Rehema ameongozana na Mh.Mbunge Balozi Dr. Kamala katika ziara hiyo

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AUG 17

RAIS DKT MAGUFULI AMPATIA BAJAJI MLEMAVU THOMAS KONE ANAYEJITUMA

$
0
0
Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akipanda  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akiujaribu  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akitoa salamu za Rais kwa  Bw. Thomas Kone (35) kuhusiana na Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone
  Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimpongeza mwnahabari Mbozi Katala alieandika na kutumia picha za  Bw. Thomas Kone (35)  na kuopelekea kupata  Bajaji y  mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba na wafanyakazi wa TBC ambao mwanahabari wao Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone

Hongera kwako Mdau wetu Frank Theo kwa safari ya masomo yako ya PhD!

$
0
0
Hongera kwako Mdau wetu Frank Theo kwa safari ya masomo yako ya PhD! 
Tunayanukuu maneno hako haya katika kukupongeza wewe na familia yako;'Ni kwa neema zake mungu nimekuwa hivi nilivyo. Hatimaye safari yangu ya masomo yangu ya PhD imehitimishwa leo. Namshukuru sana mungu kwa kunilinda mpaka siku hii ya leo mpaka kumaliza hii PhD kwa mafanikio. Namshukuru sana mke wangu mpenzi Joymertha Frank na wanangu Collins na Hellen kwa kunitia nguvu na sala zenu. Asanteni ndugu jamaa na marafiki kwa sala zenu na mbarikiwe sana..'

SHINDANO LA MISS ILALA 2016 LAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo. Shindano hilo limezinduliwa sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Miss Ilala tangu ianze mwaka 1996. 
 Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo.
 Warembo wanao wania taji la Miss Ilala 2016, wakipozi mbele ya wageni waalikwa katika halfa maalum ya uzinduzi wa shindano hilo iliyofanyika jijini Dar es Salam usiku wa kuamkia leo. Source: Father Kidevu Blog.
 Mwandaaji wa shindano la Miss Ilala 2016, Teddy Kitundu ambaye pia ni diwani wa viti Maalum Ilala, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa shindano hilo Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kulia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania , Bossco Majaliwa (kulia) na Mkuu wa Itifaki wa Kamati hiyo, Albert Makoye. Miss Ilala inafanyika ikiwa ni mwaka wa 20 tangu lianze shindano hilo mwaka 1996.
 Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akizungumza kwaniaba ya Kamati katika uzinduzi huo.
 Mmoja wa wadhamini akizungumza katika uzinduzi huo. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.
 Mratibu wa shindano hilo la Miss Ilala 2016, Eric akizungumza
 Warembo waliowahi kushirikishindano la Miss Ilala wakifungua shampein katika uzinduzi huo.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa akigonganisha glasi na warembo wanaowania taji la Miss Ilala 2016.
 Warembo wakigonganisha glasi na wadau wa urembo waliohudhuria hafla hiyo.
 Warembo wakigonganisha glasi na wadau wa urembo waliohudhuria hafla hiyo.
 Mdau akilamba unikoni na mlimbwende wa zamani wa Miss Tanzania
 Warembo wakijiselfisha wakati wa hafla hiyo
 Wadau wa urembo wakiwa katika hafla hiyo.
 Mwandishi wa habari za michezo na sanaa ya urembo, Michael Mauruce (kushoto)  akimsikiliza Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.

BALOZI DR.KAMALA AENDELEA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KWA KASI KUBWA NA VITENDO

$
0
0
Balozi Dr Diodorus Kamala,Mbunge wa Jimbo la Nkenge wa tatu kutoka kushoto pichani alipotembele eneo Kijiji cha Ishozi katika Kata ya  Bugandika Wilayani Missenyi,eneo linalo lalamikiwa na Wananchi kuwa limehingizwa katika hifadhi ya Maliasili kinyume na utaratibu.
 Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Vijiji vya Bugango na Ishozi -Bugandika wakimuonyesha Mh. Mbunge wao  Balozi Dr. Kamala eneo linalolalamikiwa na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo. 
Eneo la wazi linalotumiwa na wafugaji wa maeneo haya
Makazi ya mmoja wa wafungaji wa eneo hili
Mch. Mageke Paul ,Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bugandika akichunguza Ubora wa Generator lililokabidhiwa shuleni hapo na Mbunge wa Jimbo wa Nkenge Balozi Dr. Kamala ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi zake alizo zitoa kipindi cha uchaguzi
Balozi Dr. Kamala kwa siku ya Jana ameweza kukabidhi Generator kwenye sekondari ya Bugandika iliyopo Wilaya ya Missenyi na kusaidia maeneo mbalimbali Kata Jimboni lake
Balozi Dr. Kamala amehitimisha ziara yake nyenye lengo ya kuziona kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Jimboni humo hususani ya Maji katika Vijiji vya Igulugati,Rukurungo -Bugandika,na ile ya Kilimilile,Ruzinga, Kenyana,Bugango na Kakunyu.
Mh Balozi Kamala alitumia fursa hiyo kuongea na wananchi katika kata zote 20 zilizopo Jimboni kwenye Jimbo la Nkenge ili kujua changamoto mbalimbali
pia ameweza kuchangia vikundi mbalimbali vya Wajasiliamali na miradi ya kimaendelea kwa kuchangia fedha,madawati na katika sekta ya michezo amechangia kwa kutoa Jezi na mipira kwa timu mbalimbali ili ziweze kushiriki katika mashindano Jimboni Nkenge.
Katika ziara hiyo Balozi Dr.Kamala amebaini kuwapo kwa migogoro mingi ya ardhi kuliko maeneo mengine nchini na kuwataka wananchi kusubiri matokeo ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa.
Mh Balozi Kamala alitumia fursa hii kuwataka wananchi kufanya kazi kiwa bidii ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya 'HAPA KAZI TU'.
 Balozi Dr. Kamala amewata wananchi katika vijiji mbalimbali kutokuendekeza unywaji pombe uliokithiri hasa nyakati za kazi na ameaagiza Aliwaagiza madiwani wote na watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kupambana na umaskini uliokithiri kwa wananchi.
Aidha Mh Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala katika ziara hiyo ya pili Jimboni kwake ameendelea kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa kipindi cha miaka mitano, pia kwa kumchagua kwa kura nyingi Mh John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuwachagua madiwani wa chama cha mapinduzi.








Diwani wa Bugandika Moody Migeyo akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano wa Mbunge Balozi Dr. Kamala uliofanyika jana Alhamisi Aug 18 katika Kijiji cha Ishozi




















Balozi Dr. Kamala akisalimiana na Viongozi wa Kata ya Kashenye-Kiziba Wilayani Missenyi ,pichani katikati ni Diwani wa Kata Kashenye(Omulangira)Adeodatus Rugaibula.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Bwana Projestus Tegemaisho pichani.


Balozi Dr. Kamala akiongea na Wavuvi

WAZIRI LUKUVI ATATUA KERO ZA WANANCHI WA KAGERA KUHUSU ARDHI AWAPANGUSA MACHOZI WALIODHURUMIWA ARDHI ZAO MUDA MREFU

$
0
0
Mhe. Lukuvi (Kulia) Akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu Vitabu vya Orodha ya Makampuni Yaliyosajiliwa katika Masuala ya Upimaji wa Ardhi
Mhe. Lukuvi (wa pili kutoka Kulia) Akiongea na Watendaji wa Serikali
Mhe. William Lukuvi Akiwasili Ofisini kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera Tarehe 18.09.2016
Mhe. William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wandaji Mbalimbali wa Serikali Wakimsikiliza Mhe. William Lukuvi.


WAZIRI LUKUVI ATATUA KERO ZA WANANCHI WA KAGERA KUHUSU ARDHI AWAPANGUSA MACHOZI WALIODHURUMIWA ARDHI ZAO MUDA MREFU
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awapangusa machozi wananchi wa Mkoa wa Kagera waliokuwa wamedhurumiwa ardhi zao na walio kuwa  na kero za ardhi za siku nyingi ambapo alisikiliza kero hizo kwa umakini na kuzipatia ufumbuzi wa papo kwa hapo na kutoa haki kwa waliostahili.
Akiwa Mkoani Kagera katika ziara yake ya siku mbili Mhe. Lukuvi aliitumia siku yake ya kwanza ya tarehe 19/8/2016 kusikiliza, kupokea na kutatua kero mbalimbali za muda mrefu na zilizoshindikana  kwa wananchi  kuhusu ardhi ambapo kero nyingi alizisuluhisha na kuzipatia ufumbuzi.
Aidha kwa wananchi waliokuwawamejipatia ardhi kwa njia ya udanganyifu au kwa kuwatapeli wananchi wenzao waliamuliwa kurejesha ardhi hizo kwa wamiliki halali wenye hati zinazoonyesha mmiliki halali ni nani pia Halmashauri ya Manispaa iliamuliwa kuwapatia viwanja wananchi ambao walichukuliwa viwanja vyao na kuhaidiwa kupatiwa viwanja vingine ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti 2016.
Katika kutoa haki kwa wananchi Mhe. Waziri Lukuvi alifuta umiliki wa ardhi ya Bw. George Rogers ambye alikuwa Mtanzania lakini aliamua kuchukua uraia  wa nchi ya Uingereza ambaye alikuwa na mgogoro na wananchi wa kata ya Nyanga katika Manispaa ya Bukoba.
Bw. Rogers raia wa Uingereza alifutiwa umiliki wa ardhi aliyokuwa anaimiliki katika eneo la Kata ya Nyanga Manispaa ya Bukoba kitalu namba 1(b) kilicho kuwa na ekari zaidi ya 1800, pia alifutiwa umiliki wa eneo la Kibuye katika Manispaa ya Bukoba lenye vitalu 9 na kufutiwa pia umiliki wa ekari 60 alizokuwa anazimiliki katika eneo la Bugolora Wilayani Missenyi.
Akitangaza kufuta umiliki wa maeneo yote hayo Mhe. Lukuvi Alisema kuwa Bw. Rogers na Kampuni yake ya Rockshild Quality Food Products Ltd hawakufuata utaratibu wa umilikaji wa ardhi bali yeye na Kampuni yake walijipatia ardhi hiyo kwa njia za udanganyifu kutoka kwa wananchi.
Aidha Mhe. Lukuvi alisema kuwa raia wa nchi za Kigeni hawaruhusiwi kuingia mitaani na kuanza kujinunulia ardhi kwa wananchi bali wanatakiwa kupitia katika kituo cha uwekezaji (Tanzania Ivestment Center) ambao wanayo dhamana ya kuwapatia wawekezaji au raia wa nchi za nje sehemu au ardhi za kuwekeza mahala popote nchini.
Mbali na kutatua migogoro ya mwananchi mmoja mmoja Mhe. Lukuvi alisema kuwa migogoro mikubwa kama ya wafugaji  na wakulima, mgogoro wa wananchi wa Kakunyu Wilayani Missenyi na Ranchi za Taifa tayari unashughulikiwa na Wizara nne ambazo ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi alisema kuwa ameamua kugawa majukumu ya wizara yake katika kanda ambapo masuala yote yanayohusu ardhi hayaendi tena Dar es Saalam bali yanamaliziwa katika kanda hizo na Mkoa wa Kagera upo katika Kanda ya Ziwa ambayo ipo jijini Mwanza.
Mhe. Lukuvi kwenye ziara yake Mkoani Kagera alifuatana na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Bw. Joseph Shewiyo, Msajili Msaidizi wa Hati Kanda ya Ziwa Bi Magrgeareth Mziray, na Msajili Msaidizi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Kanda ya Ziwa Bi Dorothy Philip ambapo Wataalam hao wakishirikiana na Maafisa Ardhi wa Halmashauri za Wilaya walimsaidia Mhe. Waziri Lukuvi kupata ufafanuzi wa kero mbalimbali na kupata ufumbuzi wa keo hizo katika Mkutano na wananchi uliofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Bukoba.


MAAGIZO NA MAELEKEZO YA WAZIRI WILLIAM LUKUVI KWA WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI KAGERA KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa Mkoani Kagera katika siku yake ya pili mara baada ya siku ya kwanza kuitumia kutatua migogoro ya wananchi kuhusu ardhi siku ya pili ya tarehe 19.08.2016 aliitumia kuaongea na watendaji  mbalimbali wa Serikali akiwa mkoani hapa. 
Eneo la kwanza aliloliongelea Mhe. Lukuvi ni kuhusu migogoro ya ardhi kwa wanachi  iliyo mingi ilisababishwa na Watendaji wa Serikali waliopewa dhamana ya kushughulikia suala la ardhi, ambapo aliwaonya Watendaji wote kuacha tabia hiyo mara moja. Agizo, aliwaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa wote nchini kuwachukulia hatua za kinidhamu au kuwafukuza kazi  Watendaji hasa Maafisa Ardhi watakobainika kusababisha migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Katika Agizo hilo Mhe. Lukuvi alimpa Onyo kali Mthamini wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Projestus Katabalo kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea bila kufuata sheria, taratibu na kanuni za utekelezaji wa zoaezi la uthamini.
Eneo la pili, Mhe. Lukuvi alisema kuwa kupitia Wizara yake Serikali imepanga ndani ya miaka kumi kuwa itakuwa imepanga, imepima na kumilikisha ardhi yote ya Taifa la Tanzania. Agizo,Mhe. Lukuvi aliagiza Mikoa yote nchini kuanza kuweka mipango ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi. Aidha aliuagiza uongozi wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha unatoa hati miliki elfu kumi za ardhi kwa mwaka huu wa fedha 2016/17ambapo lengo la kitaifa ni hati Laki nne.
Agizo la pili ni kuhusu kupima maeneo yote ya Serikali (Serikali za Mitaa na Serikali Kuu) pamoja na kubaini majengo yote ya Serikali ambapo yeye kama Waziri mwenye dhamana atatoa hati maalum yenye msamaha wa kodi ya kumiliki maeneo ya Serikali ili yaachwe bila kuingiliwa na wananchi.
Agizo la tatu, ni Maafisa Mipango Miji kuhakikisha wanaainisha maeneo yote yaliyoiva kuwa miji ili yapangwe, kupimwa na kumilikishwa kwa hati za muda mrefu badala ya hati za kimila. Agizola nne ni maeneo yote ambayo wananchi walijenga miaka ya zamani na yapo katika miji (Makazi Holela) nyumba zisivunjwe bali wananchi Warasmishiwe makazi hayo kwa kuyapanga.
Eneo la Tatu aliloongelea Mhe. Lukuvi ni Kuhusu Migogoro Mikubwa  ambapo alisema kuwa katika migogoro hiyo mfano wakulima na wafugaji, alisema kuwa Serikali imeamua kuunda kamati ya Wizara nne ili kamati hiyo ipitie migogoro yote mikubwa  na kutoa ushauri kwa Mawaziri wa Wizara hizo husika ili kukomesha kabisa migogoro hiyo.
Wizara hizo nia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, TAMISEMI, na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Angalizo mikoa yote iliagizwa kuacha ugawaji wa Kata na Vijiji wakati wa Uchaguzi Mkuu bila kuihusisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwani mipaka inayotolewa na Mikoa inashindikana kuonana na mipaka ambayohupimwa  ardhini na Wizara ya Ardhi. Ili kusuluhisha hilo aliagiza Wizara yake kupewa taarifa pale Mikoa inapotaka kugawa maeneo yake lakini kwa sababu za msingi bila shinikizo la wanasiasa.
Katika kuhitimisha Mhe. Lukuvi alisema kuwa Wizara yake inatengeneza sera ya Ardhi, Nyumba na Makazi ambaop aliagiza Maafisa Mipango Miji wote nchini katika Halmashauri, Miji, Majiji, na Manispaa kuhakikisha wanaitisha vikao vya wadau ili kuamua aina ya rangi zipakwe katika miji badala ya kila nyumba kupakwa rangi yake na lengo ni kuifanya miji ipendeze kwa kuwa na mpangilio wa upakaji wa rangi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu alimshukuru Mhe. Lukuvi kwa kufanya ziara yake Mkoani Kagera na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambapo alimuhaidi Mhe. Lukuvi  kuwa maelekezoa na maagizo yake yote yatafanyiwa kazi  na wahusika ili kuhakikisha migogoro ya ardhi inakomeshwa Mkoani Kagera.

GHALA LA KAMPUNI YA BOSS SHOPPING CENTRE LTD LIKITEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Askari wa Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto wakizima moto uliokuwa ukiteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd zilimo kuwa zikihifadhiwa bidhaa mbalimbali eneo la Viwanda Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo mchana.
 wananchi wakijadiliana jambo eneo la tukio.
 Kazi ya uokoaji ikiendelea.

 Askari wa uokoaji wakiwa kazini.
 Mmoja wa wamiliki wa ghala hilo akisaini fomu  ya uzimaji wa moto huo.
 Moto ukiendelea kuwaka

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Na Dotto Mwaibale

MOTO mkubwa umeteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd lililokuwa likitumika kuhifadhia bidhaa mbalimbali maeneo ya viwandani Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio mmoja wa wamiliki wa ghala hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa hakuwa msemaji alisema moto huo ulianza saa 9 mchana.

"Tumepata hasara kubwa katika ghala hili tulikuwa tukihifadhi friji, TV, sabufa kwa ujumla ni Boss Bland Home" alisema.

Alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Baadhi ya waokoaji walikuwepo eneo la tukio walilalamikia Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto kwa kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji ya kutosha hivyo kushindwa kuhudhibiti moto huo kwa wakati ambapo ilizuka taharuki na kwa wamiliki wa viwanda vilivyokuwa jirani na ghala hilo.

Jitihada za gazeti hili kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ili kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda baada ya kumpigia simu ambayo ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa. 

MKUTANO WA WACHUNGAJI WA KKKT/DKMG 2016

$
0
0
Mkutano wa wachungaji wa KKKT/DKMG 2016 wafanyika Ntoma VTC tangu August 15 hadi 19 chini ya uongozi wa Askofu Dr. Abednego Keshomshahara.  Mchungaji Joseph Bocko awakilisha Kanisa la Kiinjili Kilutheri Marekani katika mkutano huo.
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>