Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live

HAPPY BIRTHDAY BLOGGER MC BARAKA

$
0
0
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, Aug 23. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema ambayo sistahili,Napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana, niitumie kwa mambo mema,Nizingatie wajibu wa kuvitumia kikamilifu vipaji alivyonipa Mungu kwa manufaa ya wanadamu. 

Siwezi kujivunia chochote nilichoweza kufanya, bali ni kumshukuru Mungu na kuendelea kumtegemea na kila ninaposherehekea kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa kwangu, fikra zinanituma kufananisha mchango wangu Kimkoa na Kitaifa sawa na ule wa watu maarufu,Ukweli ni kwamba ninajitahidi lakini mchango wangu bado ni hafifu sana. Mengi nimefanya kupitia Bukobawadau Blog Media ninachoweza kusema ni kwamba changamoto ni kubwa sana! 
I will always praise God

DC GABRIEL DAQARRO AAPISHWA AAHIDI MAKUBWA ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akiapa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa wilaya mpya ya Arusha,Gabriel Daqarro(kulia)wanaoshuhudia ni Katibu Tawala mkoa,Richard Kwitega na Afisa wa Itifaki,Mukhsin Khasim.
Viongozi mbalimbali katika Jiji la Arusha wakifatilia tukio hilo.
Mwenyekiti wa CCM na Mbunge mstaafu wa Longido,Lekule Laizer(kushoto) akimskiliza Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Arusha DC,Mathias Manga.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

KIKAO MAALUM CHA UVCCM MANISPAA BUKOBA

$
0
0
 Kikao maalum cha Jumuiya UVCCM Manispaa Bukoba chini ya Mwenyekiti wao Mpya Bwana Ashraf Kazinja kilichofanyika mwishoni mwa juma lililopita katikaUkumbi wa Red Cross Mjini Bukoba,Kikao hicho kilichokuwa na agenda mbalimbali kimehudhuriwa na Makada wa chama cha Mapinduzi CCM Manispaa Bukoba na Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo.
Katika kikao hicho wajumbe wamepata kukumbushwa majukumu yao kiutendaji  na kuelimishwa kuhusu mahusiano ya Chama na Serikali na nafasi ya UVCCM katika uenezi wa siasa za Chama.
 Pichani kushoto ni Mwenekiti wa UVCCM Manispaa Bukoba Ashraf Kazinja na kulia ni Bwana Erick Kaimba ambae ni Katibu  mtafiti Sera na Msemaji wa UVCCM Manispaa Bukoba.
 Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichofanika Siku ya Jumamosi Aug 20 katika Ukumbi wa Red Cross Mjini Bukoba.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Bw. Gerald (Chakaza  akizungumza na Mwenekiti wa UVCCM Manispaa Bukoba, Ashraf Kazinja
 Katika kikao hicho Wajumbe wamepata fursa kupata mafunzo ya Ujasiriamali ,na uendeshaji wa Miradi yaliyotolewa na Bwana Richard George ambaye ni Afisa mendelea ya Jamii mwandamizi wa halmashauri ya Manispaa Bukoba
Baadhi ya Viongozi wa Matawi wakiendelea kufatilia maswala mbalimbali yanajiri ukumbini hapo
 Bwana Shafii ambae ni Mjumbe katika kikao hicho  akiuliza swali.
Afisa mendelea ya Jamii mwandamizi wa halmashauri ya Manispaa Bukoba,Richard George  wakati akiendelea kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wajumbe waliohudhuria kikao cha UVCCM Manispaa Bukoba.
 Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Bukoba Bwana Philbart Katabazi (Nyerere)pichani
 Baadhi ya Wajumbe na Viongozi wakiendelea kushiriki kikao cha UVCCM Manispaa Bukoba
 Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika kikao hiki ambacho ni kikao cha pili cha UVCCM Manispaa Bukoba baada ya kumpata mwenekiti wao Mpya Bwana Ashraf Kazinja aliyechagulia tarehe 8 March 2016  kuziba pengo liliachwa na aliyekuwa mwenekiti  Bwana Chief Kalumuna.
Bwana Sitobero ambaye ni Katibu wa UVCCM Bukoba Vijijini na Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa Kagera akiwaeleza Wajumbe kuhusu nafasi ya Vijana katika utekelezaji wa Ilani ya CCM
 Bwana Najim Bwanika pichani kulia , Mjumbe wa Kikao hicho kilichofanyika siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa Red Cross Mjini Bukoba
 Wajumbe wakiendelea kushiriki Kikao hicho.
  Katibu mtafiti Sera na Msemaji wa UVCCM Manispaa Bukoba,Erick Kaimba pichani
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe wapatao 240 walioweza kijadili maswala mbalimbali na kuelimisha kuhusu Uhai wa Jumuiya,imani kazi, Muundo wa UVCCM  na Wajibu wa Mwanachama.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AUG 27

MKUU WA MKOA WA KAGERA AWAAGIZA VIONGOZI MKOANI HUMO KUSIMAMIA HUDUMA ZA AFYA KIKAMILIFU

$
0
0


MKUU WA MKOA WA KAGERA AWAAGIZA VIONGOZI MKOANI HUMO KUSIMAMIA HUDUMA ZA AFYA KIKAMILIFU
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu awaagiza viongozi katika Halmashauri za Wilaya kuchukukua jukumu la kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali za afya katika  Mkao wa Kagera  ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kikamilifu katika jamii.
Mhe. Kijuu alitoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha wadau wa afya Agosti 23, 2016 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera  kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya na Wadau mbalimbali wa Serikali na wasiokuwa wa Serikali wanaoshirikiana katika kutoa huduma mbalimbali za afya Kagera.
Katika Agizo hilo Mkuu wa Mkoa alisistiza mambo makuu na muhimu matatu kama ifuatavyo; Kwanza aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha wanajadili kwa kina na kuweka mikakati ya kutoa huduma ya chanjo  katika Halmashauri za Wilaya ili ziweze kufikia asilimia 95% ya Kitaifa .
Pili ni kuhakikisha viongozi wanapitishwa na kuelimishwa kwa undani zaidi na wataalamu wa afya kuhusu vigezo vilivyotolewa na wafadhili wanaotoa fedha za Busket Fundi ili kushirikiana katika usimamizi kwenye Halmashauri za Wilaya kukamilisha mahitaji ya vigezo hivyo ili zikidhi vigezo hivyo na kupata fedha za wafadhili zikawahudumie wananchi kupitia sekta ya afya.
Mhe. Kijuu alisema kuwa katika majaribio ya awali yaliyofanyika katika kutathmini vigezo hivyo ilionyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ilipata asilimia 93%, Muleba 83%, Bukoba 14% aidha Biharamulo ilipata asilimia 0% (sifuri)  na Halmashauri nyingine kutokana na wataalam wa afya kutoingiza takwimu za afya katika mfumo wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Mhe. Kijuu pia aliwakumbusha viongozi hao kuhakikisha wanasimamia na kuchukua tahadhali zote juu ya kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo aliagiza vituo vyote vya afya hapa Mkoani Kagera kuanza kutoa huduma za upasuaji wa dharura  kwa Halmashauri za Wilaya ambazo hazijaanza kutoa huduma hiyo zianze mara moja, pia kuimarisha Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ili kupata fedha za tele kwa tele.
Naye Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kagera Dk. Thomas Rutachunzibwa aliwashukuru wadau wote wa afya wa Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha huduma za afya Mkoani Kagera zinaimarika na aliwaomba kuendelea na ushirikiano wao mzuri ili kuboresha afya za wananchi wa Mkoa wa Kagera .

MKUU WA MKOA WA KAGERA AZINDUA RASMI MPANGO MKAKATI WA KULINDA RASLIMALI ZA UVUVI ILI KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu azindua Mpango Mkakati wa Kulinda Raslimali za Uvuvi Mkoani Kagera ili kuondokana na uvuvi haramu na madhara yake yanayosababisha kupungua kwa samaki katika Ziwa Victoria na kupelekea kudhoofisha uchumi wa Mkoa na Mwananchi mmoja mmoja wanaojishughulisha na shghuli za uvuvi.
Mpango Mkakati huo umezinduliwa leo Agosti 24, 2016 na Mkuu wa Mkoa katika Mwalo wa Malehe Kituo cha Kanyigo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ambapo aliteketeza nyavu haramu zilizokamatwa katika doria mbalimbali kupitia kituo hicho zenye thamani ya shilingi milioni 205, 510,000/- 
 Kabla ya kuzindua Mpango Mkakati huo Mhe. Kijuu alikitembelea Kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Vicfish ili kujionea uzalishaji wa kiwanda hicho ambapo Meneja wa Kiwanda Bw.Nurdin Salum Juma alitoa taarifa kuwa uwezo wa kiwanda hicho ni kuzalisha tani 60 kwa siku lakini kutokana na madhara ya uvuvi haramu kiwanda hicho kinazalisha tani 6 hadi 8 kwa siku sababu ukosefu wa samaki.
Naye Kaimu Afisa Mfawidhi Ofisi ya Usimamizi Raslimali za Uvuvi Mkoa wa Kagera Bw. Gabriel Mageni alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa kuanzia kipindi cha mwaka 2012 hadi sasa Agosti 2016 ofisi yake imefanikiwa kufanya doria na kukamata zana za uvuvi haramu katika Vituo vya Kanyigo, Bukoba na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kama ifuatavyo:
Makokoro ya Sangara 192 yenye thamani ya shilingi milioni 96,000,000/-, Timba 3,319 zenye thamani ya shilingi milioni 232, 330,000/-, Nyavu za Makila 2,410 zenye thamani ya shilingi milioni 24, 100,000/-, Nyavu za dagaa chini ya (milimita 88) 25 zenye thamani yashilingi milioni 17,500,000/- na Kokoro ndogo za vyambo 16 zenye thamani ya shilingi milioni 3,200,000/-, Jumla kuu ni shilingi milioni 373,130,000/-.
 Aidha, Bw. Mageni alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa changamoto kubwa wanayoipata katika ofisi yake ni kuachiwa suala la uvuvi haramu wao peke yao kama Maafisa Uvuvi badala ya Taasisi zote za Serikali na binafsi na Wananchi kupambana na uvuvi haramu, Pili ni kutopata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji na Kata hasa watendaji na Wenyeviti wanaozunguka katika Ziwa Victoria.
Akiwahutubia wananchi na wavuvi katika Mwalo wa Malehe Mhe. Kijuu aliwaeleza kuwa Mkakati aliouzindua utakuwa shirikishi hasa viongozi na wanachi ili kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, aidha, alitoa rai kuwa kiongozi au Mtendaji yeyote atakayegundulika kuhusika au kukutotoa ushirikiano katika suala la uvuvi haramu atashghulikiwa ipasavyo kisheria.
Aidha, aliwataka wananchi wote wanaojihusisha na uvuvi haramu kuacha mara moja ili kuruhusu samaki kuzaliana na kuvuliwa kwa utaratibu ulio mzuri. Katika hatua nyingine aliwahamasisha wavuvi kujihusisha na miradi ya ufugaji samaki katika mabwawa kuliko kutegemea Ziwa la Victoria peke yake.
Mpango Mkakati wa Kulinda Raslimali za Uvuvi Mkoani Kagera unalenga kuzuia uvuvi haramu katika Maziwa yanayopatikana katika Mkoa kwa kuendesha doria za mara kwa mara na endelevu, kuhamasisha wavuvi kukopa na kuwekeza katika uvuvi wa kisasa, na kutunza mazingira na mazalia ya samaki ili kuongeza wingi na upatikanaji wa samaki hasa katika Ziwa Victoiria.
Mpango huo utawahusisha wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wananchi, Wavuv,i Wenye Viwanda na Viongozi katika ngazi mbalimbali za Serikali hasa kuanzia katika ngazi ya Kitongoji, Kijiji na Kata ili kuhakikisha uvuvi haramu unakomeshwa mara moja katika Mkoa wa Kagera.

WAZIRI KAIRUKI AUAGIZA MKOA WA KAGERA KUHAKIKISHA DATA CHAFU ZOTE ZINAONDOLEWA KATIKA MFUMO WA UTUMISHI MARA MOJA

$
0
0
Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akiwa Mkoani Kagera aliawaagiza viongozi wa Mkoa kuhakikisha wanaondoa data chafu za Watumishi katika mfumo wa utumishi ili kuondokana tatizo la watumishi hewa.
Mhe. Kairuki alitoa agizo hilo alipokuwa akiongea na Mkuu wa Mkoa Meja Jenarali Mstaafu Salum M. Kijuu ofisini kwake mara baada ya kuwasili Mkoani hapa kwaajili ya kikao kazi cha kuongea na Watumishi wa Serikali kutoka katika Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali Mkoani Kagera.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa katika Mkoa wako kuna data chafu kama ifuatavyo, katika Sekretarieti ya Mkoa zipo data chafu 21, Bukoba Manispaa 70, Biharamulo 296, Halmashauri ya Wilaya Bukoba 429, Karagwe 211, Muleba 51, Ngara 454, Missenyi 1,608 na Kyerwa 234.” Mhe. Kairuki alitoa takwimu hizo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kusistiza data hizo kuondolewa katika mfumo mara moja.
 Aidha Mhe. Kairuki alifafanua kuwa data hizo chafu zilibainika wakati Wizara yake ikifanya uhakiki wa Watumishi kujiridhisha na takwimu zilizotolewa kuhusu watumishi hewa na kubaini kuwa kuna data chafu ambazo zinasababishwa na baadhi ya Watumishi kutokuwa na akaunti za benki za kupitishia mishahra yao.
Pia baadhi ya nyaraka za Watumishi kutofautiana majina na majina halisi wanayoyatumia kazini na yaliyopo katika mfumo wa Taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS). Vilevile baadhi ya Watumishi kuonekana kuwa tayari wamezidi umri wa miaka 60 ya kustaafu kwa lazima lakini bado wanaonekana kuwa bado wapo kazini na wanalipwa mishara ya Serikali. 
 Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu akitoa taarifa ya Mkoa kwa Mhe. Kairuki alisema kuwa Mkoa wa Kagera una Watumishi 19, 982 aidha, katika zoezi la kuhakiki Watumishi hewa Mkoa ulibaini watumishi hewa 274 waliolipwa kiasi cha shilingi bilioni 1,153,690,895.63 na fedha zilizorejeshwa ni shilingi Milioni 103, 725,731.23 sawa na asilimia 8.8%
Vile vile Mhe. Kijuu alimweleza Waziri Kairuki kuwa Mkoa unakabiliwa na tatizo la baadhi ya nafasi za watendaji kukaimiwa ambapo nafasi hizo ni 59. Jambo ambalo linasababisha baadhi ya maamuzi katika ngazi mbalimbali kutotolewa kwa wakati na kwa usahihi kutokana na Makaimu hao kutokuwa na madara kamili.
Akitoa ufafanuzi Mhe. Kairuki alisema kuwa uhakiki ni zoezi endelevu na kazi hiyo itafanyika kwa kuangalia alama za vidole ili kubaini wale wanaotumia vyeti vya watu wengine na kusisitiza hakuna Mtumishi atakayeonewa katika zoezi hilo.
Alisema pamoja na hilo uhakiki utafanyika kwa kuangalia taarifa mbalimbali za kiutumishi, ikiwamo waliobadili majina endapo kama taratibu za kisheria zilifuatwa ili kubaini waliofanya hivyo kwa nia ovu.
 Waziri Kairuki aliainisha kuwa Watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali waangaliwe kama wana sifa zinazostahili ili kubaini wale waliopo na wenye sifa lakini hawajapewa.
Aliwaelekeza Maafisa Utumishi kujielimisha kuhusu Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma ili kuepuka malalamiko miongoni mwa Watumishi na kusema ofisi yake inaandaa mfumo ambao Watumishi wa Umma nchini watawasilisha malalamiko yao kwake pale ambapo hawataridhika na huduma wanazopewa kwa waajiri wao.
Mwisho Mhe. Kairuki alitumia muda mwingi katika kikao kazi na Watumishi kusikiliza kero mbalimbali na masuala mbalimbali yahusuyo watumishi na kuyatafutia ufumbuzi hapo kwa papo.

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUBILEI YA DHAHABU (MIAKA 50) YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe wakati akiwasili kuhudhuria  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani  tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani  tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakiwa tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  na wageni waalikwa akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli  katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 MC Mavunde akipiga kinanda wakati wa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

  Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Wanakwaya katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Kiongozi wa kwaya  katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Bw. Nicholaus Mkapa, mtoto wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  akisoma somo la kwanza   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongea na wana familia, waumini na wageni waalikwa katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni waalikwa  wakiwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akimvisha pete Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akivishwa pete na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakifurahia jambo baada ya zoezi hilo
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" hao wenye furaha 
  Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" . Kulia ni  Balozi Anthony Nyaki aliyesimamia harusi yao siku kama ya leo miaka 50 iliyopita. Matron alikuwa Marehemu Lucy Lameck.
  "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wanaketi baada ya ukumbusho wa viapo vya ndoa yao katika  kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akiongea na kadamnasi 

  Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni wakiendelea na misa
 Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa
 Sir Andy Chande akiungana na waalikwa katika misa hiyo
 Mohamed Dewji na mkewe wakiwa katika misa hiyo
 Mstari wa mbele
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg Philip Mangula na mkewe pamoja na wageni wengine
 Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa
 Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi, Maspika wastafu Mzee Pius Msekwa na Mama Anne makinda na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue
 Sehemu ya waalikwa
 Jaji Mkuu mstaafu Mhe. Barnabas Samatta na mkewe pamoja na waalikwa wengine
 Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Marten Lumbanga na mkewe pamoja na Waziri mstaafu Profesa Philemon Sarungi na mkewe Mama Sarungi
 Waalikwa
 Wageni waalikwa 
 Waalikwa
 Sehemu ya waalikwa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiongoza wana familia kupeleka matolea altereni
 Kwaya 
 Sehemu ya waalikwa
 Waalikwa
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa 
 Misa ikiendelea
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa 
 Misa ikendelea
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mama Anna Mkapa
Mama Janeth Magufuli na Mama Maria Nyerere wakiwatakia amani Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa

 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati malumu ya ndoa kutoka Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

WAZIRI JENISTA ATOA SOMO ​KWA ​MAB​E​​​​NKI, FINCA YAPETA

$
0
0
Sekta za kifedha zinazohusika na utoaji wa mikopo nchini zimetakiwa kutenga utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wa wadogo, kati na wakubwa ili kuleta unafuu wa masharti ya ukopaji. Hayo yalisemwa katika kilele cha mafunzo ya Wiki ya Huduma ya Kifedha na Uwekezaji na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Walemavu Jenista Mhagama alipokuwa anafunga siku ya mwisho ya mafunzo hayo Agosti 27.

Mhagama alisema kuwa mafunzo kwa wajasiriamali yamekuwa yakitolewa mara kwa mara ila kikwazo kimekuwa ni mkopo hususani kwa wajasiriamali wanaoenda kukopa masharti wanashindwa yakiwemo uwekaji wa hati ya nyumba kama dhamana na riba kubwa.
“Tanzania kuna takribani wajasiriamali milioni tano, ila wengi wao wanashindwa kupiga hatua kutokana na masharti mazito ya mikopo, mfano mama anauza vitumbua unamwamabia alete hati ya nyumba na wakati kapanga chumba kimoja” Alisema Mhagama.
 Alieleza kuwa banki na wadau wote wa maendeleo wakutane ili kujadili ni namna gani wanavyoweza kupunguza masharti kwa wajasiriamali wadogo ili kuwakomboa na kupunguza tatizo la ajira na umasikini nchini. Mhagama ambae pia ni Mbunge wa Peramiho alisema kuwa Serikali itakuwa tayari kufanya majadiliano kuona namna ya kumsaidia mjasiriamali mdogo na wa kati huku akiwapongeza Banki ya Finca kwa kupunguza gharama za ukopaji kwa wananchi.

Meneja Masoko na Afisa Mahusiano wa Bank ya Finca, Spacio Aboubakar alisema walijitahidi kufatilia vikwazo vyote vinavyowakwamisha wajasiriamali na kuvifanyia kazi na kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa masharti kwa mkopaji na ulipaji wa riba. Banki ya Finca imekuwa mkombozi kwa wajasiriamali nchini katika maonyesho hayo walifanikiwa kusajili zaidi ya wajasiriamali 4000 wapya.

Katika mafunzo hayo wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali vilishiriki ikiwemo Vikoba pia washindi walikabidhiwa fedha taslimu laki tano ili kuwapa motisha wajasiriamali wengine kushiriki miaka inayofata. Nuru Salim ni mmoja wa washindi wa zoezi lililofanywa na banki ya Finca na kuibuka mshindi alisema wamama wajitokeze kwa wingi kujifunza na kupata elimu ya uwekezaji na ujasiriamali ili kuepukana na tatizo la kuwa tegemezi.
“Mimi najihusisha na uuzaji wa nguo za wanawake Kariakoo, ila hapohapo nauza vitafunwa ninavyotengeza mwenyewe kama vitumbua ila nimekuja hapa kuongeza vitu vipya” Aleleza Nuru.

Maonyesho hayo yalikuwa ya tano na huwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta za banki, bima na uwekezaji kutoa elimu kwa wajasiriamali zaidi ya 20,000 na muitikio mkubwa ulikuwa wa wamama kuliko vijana na wanaume.

Mwandishi: Muyonga Jumanne (Mwananchi)

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AUG 29

TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

$
0
0
Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane

Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Bukoba mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Wilfred Lwakatare.

Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Bukoba mjini.

Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Bukoba mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE

a. Ujenzi wa soko kuu la Bukoba, soko la Kashai na Stendi kuu ya mabasi Bukoba

b. Mikopo ya vikundi vya kijasiriamali vya akina mama na vijana

c. Urasimishaji wa makazi

d. Bima za afya kwa wananchi angalau​ 5000

Mada hii itatumika zaidi na Wana Bukoba kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:-

1. Mh. Mbunge Wilfred Lwakatare
2. Katibu Alex Xavery (Katibu)
3. Happiness Essau (Afisa habari Bukoba)
4. Chief Karumuna (Mayor wa Bukoba)
5. Jimmy Kalugendo (Naibu Mayor)
6. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Bukoba mjini.
 
CREDIT :JF
Karibuni...

KAGERA SUGAR WAFURAHIA KURUDI NYUMBANI, WAJIFUA KWA MARA YA KWANZA KAITABA LEO HII.

$
0
0
Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar, Wanamkurukumbi wakiteta jambo leo kwenye Uwanja wa Kagera Sugar kwa mara ya kwanza Tangu Uwanja huo ukamilike hivi karibuni. Na sasa ukiwa tayari kwa Michezo mbalimbali ikiwemo Mitanange ya Ligi Kuu Vodacom. Kagera Sugar wanajifua kujiandaa kwa Mchezo wao wa tarehe 3 Septemba, 2016 dhidi ya Mwadui kutoka Shinyanga ambapo nmchezo huo utapigwa katika Uwanja huo ambao umejengwa tayari kwa Viwango vya Fifa. ‘Wanankurukumbi’ walipambana hadi siku ya mwisho kukwepa mkasi wa kushuka daraja msimu uliopita wakiwa na kocha wao Adolf Rishard na sasa wakiwa na Kocha mpya msimu huu mpya 2016/2017 Mecky Mexime ambao pia wamefanya usajili wakiwemo makipa. Leo wameanza kujifua kwenye Uwanja wao kwa ajili ya kuhakikisha hawakumbwi na gharika iliyowakosa msimu uliopita na hatimae kufanya vyema kwa msimu huu ambao umeanza kwa aina yake wakianzia ugenini mechi zao mbili za mwanzo.
Wakiomba kabla ya kufanya Mazoezi leo hii jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama ambaye pia ni Katibu wa KRFA (katikati) kulia ni Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), WALLACE KARIA nao walikuwepo Uwanjani hapo kujionea Uwanja huo ambao umemalizika kwa kusuasua.


Mecky Meximeakitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba, Wakijiandaa kuikaribisha Timu ya Mwadui hivi karibuni.
Kwa Makini Wachezaji wa Kagera Sugar wakisikiliza Viongozi wao

Wachezaji wa Kagera Suga wakijifua leo hii hioni kwenye Uwanja wa Kaitaba
Kocha mpya wa Kagera Sugar Mecky Mexime



Dokta wa Timu ya Kagera Sugar(kulia) akiteta jambo na Mwamed (kushoto)

Walinda mlango wa Kagera Sugar wakijifua Vikali leo hii
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangaru
Mashabiki wamejitokeza kwa Wingi kuwakaribisha Kagera Sugar ambao walichezea Misimu miwili nje ya Uwanja wa Kaitaba. Msimu ulopita Kagera waliwapa presha kubwa wapenzi wao hadi dakika za mwisho ambapo walikuwa wanapigania kutoshuka daraja.


Mashabiki wakiwacheki Kagera Sugar leo wakati wa Mazoezi Kaitaba


Mashabiki wa Kagera Sugar leo wamejitokeza kwa wingi kuwaona wenzao 'Wanankurukumbi' wakati wa mazoezi

Mashabiki na Wapenzi mbalimbali wa timu ya Kagera Sugar wamejitokeza kwa Wingi hii leo kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kupita kwa ujenzi wa uwanja huo.




Mazoezi makali kujiandaa na Mzunguko wa Tatu wa Ligi kuu Vodacom

Makipa wa Kagera Sugar wakijiuliza jambo leo wakati wa mazoezi yao kwa mara ya kwanza tangu Uwanja huo umalizike kujengwa hivi karibuni. Kagera Sugar wanajiandaa na Mchezo wao wa Ligi kuu Vodaom tarehe 3.



Mapumziko, Wachezaji wa Kagera Sugar wakipata maji ya kunywa.Kocha Mkuu wa Kagera Mecky Mexime
Shabiki wa Kagera Sugar
Straika wa Bukoba Veteran Salum Bonge nae alikuwepo Uwanjani hapo
Mecky Mexime

DALADALA LAGONGA MAGARI MATATU MAJI MATITU TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

$
0
0
 Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
 Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
 Daladala hiloegonga gari namba T 458 CAN.
 Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
 Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.

Na Dotto Mwaibale

MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.

Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo  asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.

Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.

" Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema Juma.

Alisema baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.

Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.

Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.

R.I.P BI ESTHER JOSEPH RWEGASIRA

$
0
0
R.I.P Diwani msitaafu kata Kanyiko Bi Esther Joseph Rwegasira.
Kifo kimetokea alfajiri yatarehe 27 Aug huko nchini India alipokuwa anapatiwa matibu.

Mwili wake umewasili Jijini Dar Jioni ya leo Jumanne Aug 30 ,mwili wa Marehemu Bi ESther utalala katika hospitali ya Lugalo mpaka siku ya kesho Jumatano itakapofanyika Ibada maalum (last respects ) katika kanisa la St.Peters church Jijini Dar na kufatiwa na Safari ya kuelekea Bukoba .
Mwili wa Marehemu Bi Esther Rwegasira utawasili siku ya Alhamisi Saa 7:30 mchana katika Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba na mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa Tarehe 2 Aug Nyumbani kwake Kijijini Kanyigo.

#Bukobawadau Media tunatoa pole kwa wafiwa wote!
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!

KATIBU CHADEMA MWANZA ABWAGA

$
0
0
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, John Nzwalile amejivua nyazifa zake tatu pamoja na uanachama wa chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa na ubabaishaji.
Mbali na ukatibu wa mkoa, Nzwalile alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho taifa.

R.I.P MZEE UDD IDD MIRUKO

$
0
0
R.I.P Mzee Udd Idd mwenyekiti wa Mtaa wa Bilele Manispaa Bukoba.
Kifo cha marehemu mzee Udd Idd kimetokea mapema ya leo katika Hospitali ya Mkoa Kagera, Shughuli ya mazishi inatalajiwa kufanyika Kesho jumatano Aug 31 katika Makaburi ya Kishenge Bukoba.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un..!!

CHADEMA WASITISHA MAANDAMANO YA (UKUTA)

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe amesitisha shughuli za maandamano zilizokuwa zimepewa jina la (UKUTA) kwa Muda wa mwezi mmoja baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi Mbalimbali, ambapo maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika Septemba mosi nchi nzima.

PATA HABARI ZA UHAKIKA ZA KUPATWA NA JUA KUPITIA TOVUTI ZA DAILYNEWS NA HABARILEO ONLINE KUTOKA RUJEWA

$
0
0
Kaa tayari kupata habari na matukio motomoto yatakayo kua yakijiri kutoka eneo la Rujewa, Wilayani Mbararali mkoani Mbeya ambako tukio kubwa la kihistoria Duniani linakwemda kushuhudiwa hapo kesho kwa JUA KUPATWA KIPETE.

Kampuni yako ya magazeti ya Serikali (TSN) ambao ni wachapaji magezti ya Daily News, Habarileo, Spotileo, Sunday News na Habaroleo Jumapili itakuwa ikikurushia matukio hayo kupitia  mitandao yake ya http://www.dailynews.co.tz na http://www.habarileo.co.tz 

HAPA KAZI TU.....HAKUNA KULAZA HABARI.

RC ARUSHA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI

$
0
0

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto)  alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo nae akiwa ameambata na Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Mheshimiwa Angela Kizigha.
Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia)  baada ya mazungumzo yao.
Nteghenjwa Hosseah – Arusha


Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea  na  ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini  ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi  baada ya kuteuliwa kushika  wadhifa huo hivi karibuni.


Mh.Gambo amekutana na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji  Solomon Masangwa , Askofu wa  Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi  na Askofu  Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount  Kilimanjaro.


Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.


Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph  Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani  halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya  mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali  zitakazowawezesha kufanya  shughuli za uzalishaji mali.


Amewataka  wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari  kupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa  elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.


Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.



Aidha alishauri  kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo  ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.


Mh. Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili  watoe mawazo yao katika kuiboresha na  kuifanya itekelezeke   kwa wepesi zaidi.

FAMILIA YA AL- HAJI ABBAKARI GALIATANO WASHIRIKI NA WADAU KATIKA DUA YA PAMOJA!

$
0
0
Familia ya Al-haji Abbakari Galiatano kwa ukarimu na upendo waungana na jamaa na marafiki wa familia Nyumbani kwa Bwana Abdul Galiatano katika dua maalum ya familia hiyo ya kuwaombea na kuwatakia maghufira ndugu zao waliotangulia mbele ya haki na kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha ndugu Abdul Galiatano kuingia katika nyumba yake. 
 Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa juma lililopita na kufuatiwa na pongezi kutoka kwa Viongozi mbalimbali na mawaidha yakuwataka wanafamilia kuendeleza upendo na mshikamano baina yao.
 Mzee Al haji Abbakari Galiatano akiendelea kushiriki  dua hiyo
 Baadhi ya ndugu na marafiki wa familia walihudhuria shughuli ya dua hiyo iliyofanyika Mwishoni mwa juma Nyumbani kwa Bwana Abdul Galiatano mitaa ya Omukigusha Mjini Bukoba.
Aliyesimama pichani ni Al haji Sadick Galiatano wakati mawaidha yakiendelea kutolewa
Kutoka kushoto pichani ni Khalid Galiatano, Badru.S.Galiatano na Abdul Galiatano

 Bwana Majid Kichwabuta  pichani
 Mdau Optaty Henry (Katibu) mmoja ya walioweza kushiriki dua hiyo
Shughuli ya dua ikiendelea.

Bi Mwajabu Galiatano na Bi Murungi Kichwabuta wakiweka ubani
Sehemu ya wadau wa familia ya Al haji Abbakari Galiatano wakiendelea kushiriki dua hiyo
Aliyewahi kushika wadhifa wa mkuu wa Mkoa na kustaafu Bw. Mohammed Babu pichani akitoa nasaha na shukrani kwa familia 
Bw. Mohammed Babu akiendelea kutia neno la shukrani.
 Sheikh akitoa nasaha zake kwa wanafamilia
 Bwana Majid akionyeshwa kuguswa na maneno ya Sheikh
 Vivyo hivyo haji Sadick akinyanyuka kwa ajili ya kumtunza Sheikh.
Sheikh akipongezwa baada ya kutoa  mawaidha yakuwataka na kuwahimiza wanafamilia kuendeleza upendo na mshikamano baina yao.
Baadhi ya wadau pichani walioweza kupata furasa ya kushirika shughuli ya dua hiyo
 Mrs Abdul pichani kushoto na Mama Mkwe wake ,Bi Mdogo wa Al haji Abbakari Galiatano
 Sehemu ya wanawake waliohudhuria shughuli hiyo,
 Kutakabaliwa kwa dua kunaendana na Chakula
 Baadhi ya washiriki wa shughuli hii wakipata huduma ya Chakula
 Wadau wakiendelea kupata chakula
 Kwa pamoja wadau wakishiriki chakula  mara baada ya dua
 Matukio zaidi ya picha yanaendelea...
Viewing all 4177 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>