Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4180 articles
Browse latest View live

NDIVYO MAMBO YATAKAVYO KUWA MAGEZETI YETU YA UDAKU

$
0
0
IDRISS, WEMA WAKUTWA POZI TATA
WEMA: AN HAPPY WITH HIS SUCCESS
IDRISS:WEMA NI KAMA DADA YANGU
DIAMOND AHAHA KUZUIA UKARIBU WA WEMA NA IDRISS
IDRISS, WEMA SIYO SIRI TENA
MAMA WEMA: NAPENDA WAOANE KABISA SI KUCHEZEANA
WEMA: IT WAS MY DREAM TO HAVE HIM IN MY SOUL SINCE 2006
IDRISS AMTESA DIAMOND
IDRISS, WEMA WAMFANYA DIAMOND KUWA MASELE CHA POMBE
KADINDA ROHO KWATU UHUSIANO WA IDRISS NA WEMA
MAMA IDRISS: SIWEZI KUINGILIA MAPENZI YAO
 Mdada aibuka toka Yombo Dovya: NIMEZAA NA IDRISS TOKEA 1999
Mdada toka Shimo la udongo: IDRISS NI MUME EANGU HALALI WA NDOA
AUNTY EZEKIEL NA WEMA NDANI YA BIFU ZITO, KISA IDRISS.
IDRISS AONYWA KUTOKUWA KARIBU NA LULU, YASIJE MKUTA YA KANUMBA.

KAJALA AWABWAGA SHILOLE, WEMA,WOLPER, LULU, AUNTY NA ODAMA JUU YA PENZI LA IDRISS
 Najaribu kutengeneza heading za magazeti ya udaku bongo baada ya Idriss kuukwaa ushindi wa BBA
CREDIT;JOE

AMEZWA NA NYOKA AINA YA ANACONDA

$
0
0
 Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.
Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
 Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka huyo.
 Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ''
Paul na vazi alilotumia kuingia ndani ya Nyoka kabla ya kushindwa na kusalimu amri
 "nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''
''Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ''
Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa anaumizwa.
''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.'' alisema Paul.
Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa tatu
BBC

JOSE & MTESI ISSA WEDDING!!

$
0
0
 
Maharusi Bw. Jose Ledo na Bi Mtesi Issa katika shughuli ya ndoa yao iliyofanyika mwishoni mwa Juma katika hotel ya Ocean Paradise iliyopo katika Kijiji cha Pwani Mchangani ,Zanzibar.
   
Muda mchache baada ya tukio la ndoa wanapata picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu. 
Bibi harusi Bi Mtesi Issa katika furaha na Kaka yake pichani ni Mlangira Focas Lutinwa.
Pichani kushoto ni Mr Richard Kahama katika picha na maharusi Mr & Mrs Jose Ledo (katikati)wakifuatiwa na rafiki yao Bi Lulu pichani kulia 
Mlangira Focas Lutinwa  na Mkewe Bi Halima Nsubuga katika picha na maharusi.
 
Matukio ya picha mbalimbambali katika fukwe za hoteli ya kitalii Ocean Paradise
  
Moja kwa moja kutoka katika hoteli yenye hadhi na sifa  ni Ocean Paradise Zanzibar pichani kushoto wanaonekana Maharusi wakipata tui la nazi 
Bi Halima Nsubuga pichani kushoto katika pozi la aina yake..,kulia anaonekana Mme wake Mlangira Focas Lutinwa akimcheck kwa tabasamu pana!
 Siku moja kabla ilifanyika sherehe ya kumuaga Bi Mtesi Issa (Send off Party),Shughuli hiyo ilifanika Jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Danken House – Mikocheni.
 Pichani  anaonekana Mama mzazi 'Omwamikazi'  Apolonaria Lutinwa  akiwa na Mjukuu wake Kelvin Lutinwa.
Shughuli ya Send off Party ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wakiwemo viongozi wa taasisi mbalimbali.
Sehemu ya waalikwa pichani kushoto ni  Eng.Elasto Machume , Mr. Ben Kataruga (katikati) anayefuata ni Mr. Jamal Malinzi
Bi Mtesi Issa akimkabidhi zawadi ya Keki  mmewe mtalajiwa Mspanish Mr.Jose Ledo
Bi Mtesi anapiga maguti kumkabidhi mama zawadi yake ya keki.
Wanapeana mikono ya pongezi na shukrani
Sehemu ya wanafamilia Katika picha ya pamoja na Mama Mzazi wa Bi Mtesi 'Omwamikazi Omwamikazi'  Apolonaria Lutinwa
MUHIMU :BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Muonekano wa Bi Halima Nshubuga katika Send off Party ya Bi Mtesi
 
BUKOBAWADAU BLOG TUNAWAPA HONGERA MAHARUSI MR & MRS JOSE!!
  Muhimu kwa wale waliotaka nyongeza ya picha zaidi za send off party jiunge nasi kwa ku-like ukurasa wetu wa facebook kupitia hapa>>Bukobawadau Entertainment Media

KATIKA KUWAJIBIKA KUMBE LOWASSA JEMBE

$
0
0
NA PRUDENCE KARUGENDO

KUMBE  ni vigumu kupata uzuri au ubaya wa kitu kama kitu hicho hujakilinganisha na vitu vingine. Kukilinganisha ndiko kunaweza kutoa picha sahihi ya kipi kizuri kipi kibaya. Bila kuvilinganisha vitu na kupata picha sahihi ya jinsi vilivyo inaweza kutolewa hukumu ya ubaya au ya uzuri kwa kuoneana au kupendeleana.

Sakata la wizi wa pesa za umma kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow limeibua mengi, kama nilivyoonyesha kwenye makala yangu ya juma lililopita,  bado sakata hilo linaendelea kuibua mengine mengi. Lingine lililoibuliwa na kuwekwa peupe ni la ujasiri wa wasimamizi wa shughuli za serikali, mawaziri wakuu. Kwa hapa niwataje Edward Ngoyai Lowassa, aliyewajibika kwa kujiuzulu nafasi hiyo kufuatia Kashfa ya Richmond, na Mizengo Kayanza Pinda, anayegoma kuwajibika kwa kujiuzulu kufuatia kashfa mbaya kuliko zote kuwahi kutokea tangu nchi yetu ijitawale, kashfa ya “Tegeta Escrow Account”.

Tukijaribu kuzilinganisha kashfa hizi mbili, Richmond na Tegeta Escrow Account, tutaona kwamba Richmond, hata kama ilikuwa imelenga kwenye faida, lakini lengo lake kuu lilikuwa ni kuinusuru nchi isiingie kwenye janga la giza. Hiyo ni tofauti na akaunti ya Tegeta escrow ambayo ni ya pesa zilizokuwa na mashaka.

Tofauti inakuwa hivi, moja ni ya kushindwa kuwekeza na nyingine ni ya kukwapua pesa ya umma.

Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa ajili ya kuzihifadhi pesa zilizokuwa zikitolewa na Tanesco kwa IPTL huku kampuni hiyo ya umma ikiwa inanung’unikia uhalali wake, kusudi ukweli ukipatikana wa kiasi gani halali kampuni hiyo ilipaswa kuilipa IPTL ndipo pesa hizo ziende kwa mwenyewe, kwa IPTL  au kurudi kwa aliyezitoa. Mpaka hapo pesa hizo zilikuwa bado ni umma.

Mmoja wa waliotoa ushahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Migogoro ya Kibiashara, London Uingereza, kuhusu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow zilipaswa ziende kwa nani kati ya Tanesco na IPTL, Patrick Rutabanzibwa, anasema baada ya kutoa ushahidi wake katika mahakama hiyo dalili zote zilionyesha kuwa pesa hizo ni mali ya Tanesco kutokana na IPTL kuzidisha kwa makusudi ghalama za madai yake kwa Tanesco.

Rutabanzibwa anasema kwamba baada ya ukweli huo kujulikana ndipo ikaonekana kwamba pesa yote iliyokuwa kwenye akaunti ya Tegeta escrow ilipaswa iende Tanesco na bado Tanesco iendelee kuidai IPTL kiasi kingine kilichobaki.

Kilichotakiwa kufanywa kabla ya hapo ni serikali kupitia shirika lake la Tanesco kufanya mahesabu ili kujua kwa uhakika ghalama halisi waliyopaswa kuidai IPTL mbali na pesa iliyokuwa kwenye akaunti ya escrow. Lakini hicho hakikufanyika, kilichozuia mahesabu hayo kufanyika hakiko wazi. Ila inahisiwa kwamba ni kwa vile pesa hiyo ilishaanza kudokolewa kwenye akaunti ya escrow.

Na kwa vile hesabu hiyo ya ni kiasi gani cha pesa ambayo Tanesco ilipaswa kuidai IPTL haikufanyika kwa kuzishirikisha pande zote mbili, ndiyo maana CAG akasema kwamba pesa ya kwenye akaunti ya escrow ingeweza kuwa ya umma au isiwe ya umma. Hiyo ni kwa vile mahesabu ambayo yangetegua kitendawili hicho hayakufanyika.

Kwa ufupi ni kwamba lengo la IPTL halikuwa kuinusuru Tanzania isiingie gizani kama ilivyokuwa kwa Richmond,  bali kuifanyaTanzania kichaka kilichonona ambacho kila mtu angeweza kujifunzia uwindaji na kutoka ndani na mnyama, awe swala, digidigi na hata tembo! Yaani mahali pa kujizolea pesa.

Sio lengo la makala haya kutoa historia ya pesa hiyo chafu, isipokuwa tunataka kuonyesha kwa uhakika kuwa pesa hiyo ilikuwa mali ya umma  ambayo waziri mkuu, akiwa msimamizi wa shughuli zote za serikali ikiwemo pesa hiyo, alitakiwa kuwa na habari ya nini kinaendelea.
 Lowassa, tofauti na Pinda, baada ya mkakati wake kugeuka kashfa hakuwa na kigugumizi cha sikujua, kibusara aliona kuwa huo ni mzigo ulio kichwani kwake, akakubali kuutua kutokana na picha iliyoonyesha kwamba umemuelemea, akakubali kuwajibika mwenyewe ili kuilindia heshima nafasi hiyo ya waziri mkuu.
Kwa kuona hivyo wote walioguswa na kashfa hiyo hawakuwa na lingine la kufanya zaidi ya kuachia ngazi wenyewe bila kusubiri kupigiwa “nduru”, neno la Kihaya linaloashiria tukio la hatari.

Uamuzi huo wa Lowassa uliokoa mambo mengi ukiwemo muda wa Bunge, ghalama za kuliendesha Bunge mpaka usiku wa manane na hata siku ambazo si za vikao vya Bunge nakadhalika. Uamuzi huo wa Lowassa tusipouita ujasiri unaotokana na mtu kujituma akijua anautumikia umma tuuiteje?

Hata kama Spika Makinda hakutamka majina bilashaka alimaanisha tukio hilo la Lowassa pale aliposema kwamba waliowahi kuguswa na tukio la aina hiyo hawakupoteza muda kwa vile walikubali kuwajibika wenyewe, lakini hawa wamegoma. Ni wazi  alimaanisha ujasiri wa Lowassa.

Hata hivyo sote tunaelewa kwamba waziri mkuu, Mizengo Pinda, au mtoto wa mkulima,  kama yeye anavyopendelea kujulikakana, sio mtu mwenye dalili za ufisadi. Ila pale unapotokea ufisadi,  hasa ulio chini yake kama huu,  anatakiwa atuhakikishie bila kuacha chembe yoyote ya mashaka kuwa hahusiki nao.

Lakini kitendo cha kung’ang’ania kiti kwa madai ya kwamba hakujua kama kuna ufisadi unaotendeka chini yake kinatulazimisha tumuangalie vibaya, kinatufanya tumuangalie kama mtu aliyeuatamia ufisadi makusudi na kuufanya uimarike akiwa ametuficha tusiuone ila tuje kuambulia tu madhara yake.

Waziri mkuu kama alivyo Pinda anatakiwa afanye mambo kwa kusukumwa na mguso alionao kwa wananchi na kwa nchi yake, hapaswi kuongoza kwa kutumia hisia na dhana, anatakiwa atumie utashi ulio kwenye maamuzi yake mwenyewe. Sababu mara nyingi Pinda anapendelea kutumia maneno ya “mimi nadhani, mimi nahisi, mimi nafikiri (bila uhakika) nakadhalika, maneno yanayomuondoa kwenye utashi wake wa maamuzi.

Yeye akiwa waziri mkuu akifanya mambo kwa kuhisi na kudhani anategemea ni nani afanye mabo kwa uhakika uliokamilika?

Jambo zuri na jepesi ambalo angelifanya Pinda na kuendelea kuvuta imani za wananchi ni kujitenga kabisa na ufisadi huo alioutamia kwa kuondoka hapo alipo ili rais akamjaribu mtu mwingine.

Kuwajibika sio mwisho wa kuwatumikia wananchi. Mzee Ali Hassan Mwinyi aliwahi kuwajibika katika miaka ya 1970, kuwajibika huko kulibaki katika kumbukumbu za wananchi na baadaye kukachangia kumpa Mwinyi urais kwa kishindo mwishoni mwa mwaka 1985. Tayari wananchi walikuwa na imani naye kuwa yuko makini kuwalinda kutokana na kuguswa na yanayowapata. Lakini asiyekuwa tayari kuwajibika utampimaje kuwa yuko tayari kukulinda?

Sababu hata kama haya yametokea bila Pinda kuelewa, kitendo cha yeye kuukalia uchafu ambao wananchi wameishauona na kumuonyesha bila yeye kushtuka ni uzembe usiomithilika. Ni imani yangu kuwa wananchi hawapendezwi kuwa na kiongozi mzembe, maana uzembe hauwezi kuwahakikishia usalama wao na mustakabali mwema wa nchi yao.

Sakata hili la Tegeta Escrow linanifanya nimalizie makala yangu haya kwa kumpongeza Edward Lowassa kwa ujasiri wake wa kukataa kujifunga pamoja na uzembe, hivyo akaamua bila kushurutishwa kuachia ngazi, pamoja na uhondo wa ngazi hizo ulivyo. Sababu hicho ni kitendo cha kijasiri kwelikweli, huu ni ushuhuda tosha kwamba wengine kinawashinda.


0784 989 512

MATUKIO MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam 
 Baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa jirani wakiwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dare Salaam katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo hufanyika kila mwaka. Picha na Ikulu.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini pamoja na Wananchi wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

PICHA YA VIJUKUU WA MALKIA YAZUA GUMZO!

$
0
0
 Gumzo lenyewe ni hilo hapo chini Kutoka Sandrarose.com (Sandra Rose ni blogger Mwingereza mweusi aishiye Atlanta)
 Uh oh: LeBron James Broke Royal Protocol by Not Showering and Touching Duchess Kate
The British are angry that NBA Superstar LeBron James broke royal protocol when he met the Duke and Duchess of Cambridge last night.

Earlier I told you that LeBron showered before meeting the royal couple at the Barclays Center after a NBA game. Well it seems I was wrong. LeBron was unwashed and wearing sweaty gym clothes when he met the royal couple.
Mr. James did not dignify himself or the royals by at least changing his sweaty clothes before meeting with Prince William and Duchess Kate Middleton following the Cavaliers vs Brooklyn Nets game. We British are taught as children that cleanliness is next to Godliness.
Furthermore, Mr. James broke royal protocol by touching the Duchess without authorization. Look at Kate’s body language as LeBron put his arm around her shoulder.
We Brits are not the touchy feely sort like you Americans. Touching is not allowed unless by invitation. Sadly, American children are not taught the importance of respecting the boundaries of someone else’s personal space.
I’m embarrassed for LeBron. I thought he knew better.
Hii ni kutoka Daily Mail:
Etiquette expert William Hanson told MailOnline that although the Duchess is unlikely to give Mr James the cold shoulder, he still should have kept his arm away from her.
‘Americans are much more tactile than we Brits and this is another example of an American being too touchy feely with British royalty. You’d have think they’d have learned by now.’
The 6ft 8in basketball star also appeared alongside the royals in a sweaty top, which some may regard as bad form.
Mr Hanson added: ‘A shower would have been preferable but he had just finished a game – so even more reason for him not have opened his pits by lifting his arm and placing it around Her Royal Highness!’

IKULU:JK hatawaadhibu vigogo wa escrow bila ya uchunguzi

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
 Dar es Salaam. Ikulu imesema pamoja na kuwa Rais Jakaya Kikwete amekwishapokea maazimio ya Bunge kuhusu wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, hawezi kuwachukulia hatua mpaka hapo uchunguzi kuhusu suala hilo utakapokamilika.
“Rais lazima aagize vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake na baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia. Watu wengi walitaka Rais Kikwete achukue hatua baada ya kupewa maazimio ya Bunge. Jambo hilo haliwezekani,” Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa na makosa ya kimaadili au jinai baada ya uchunguzi.
Alisema uchunguzi kuhusu uchotwaji wa mabilioni hayo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia utazingatiwa na Rais katika kutoa uamuzi.
“Maazimio ya Bunge ni mazuri ila inatakiwa muda kwanza ili Rais naye apate taarifa za uchunguzi zaidi. Maazimio hayo ni muhimu na si ya kupuuzwa hata kidogo,” alisema.
Alisema vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu suala hilo ni vile ambavyo vilitajwa kufanya hivyo katika maazimio manane ya Bunge.
Bavicha wamtaka Kikwete achukue hatua
Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete kuacha kuhamisha wakuu wa mikoa na badala yake atoe uamuzi wa kuwashughulisha watuhumiwa wote waliohusika na kashfa ya escrow.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Bavicha, Mwita Julius alisema: “Wakati huu si mzuri wa kuanza kuhamisha wakuu wa mikoa kwa kuwa ni gharama, ni muda wa kuwachukulia hatua wahusika wote waliotajwa bungeni wakihusika na sakata la escrow.”
Alisema Rais anatakiwa kuwashughulikia wateule wake wote waliotajwa bungeni kwani wananchi wanasubiri kuona mabadiliko hayo kwa haraka.
Juzi, Rais Kikwete aliteua mkuu mmoja wa mkoa na kuwahamisha wengine sita.
Nyongeza na Hussein Issa na Hadija Salum.
MWANANCHI

MKURUGENZI AMTIMUA MWANDISHI WA HABARI

$
0
0
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Cornel Ngudungi  (mwenye miwani) akiwa katika moja ya mikutano yake.
 Mwanahabari wa Radio na magazeti Mkoani Kagera Shaaban Ndyamukama  katika kuwajibika 
NGARA.
Wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya  Kikwete akisisitiza watendaji wa serikali  kufanya kazi na vyombo vya habari hali imekuwa tofauti kwa baadhi yao na kulazimika kuwatimua wanahabari kwenye ofisi zao
Hali hiyo imejitokeza jana wilayani Ngara  mkoani Kagera ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri  ya wilaya hiyo Cornel Ngudungi  alipomfukuza mwandishi wa habari  Shaaban Ndyamukama aliyetaka kujua maendeleo ya kampeni za uchaguzi
Ngundungi ametoa kauli hiyo  ofisini kwake  muda mfupi baada ya kumfukuza mwandishi huyo  kwa madai kuwa anaandika  habari  za  kuichafua  halmashauri  ya wilaya hiyo na kukiuka maadili ya uandishi
Mkurugenzi huyo amesema  haoni umuhimu wa kutumia vyombo  vya habari kutoa taarifa za maendeleo  kwa wananchi kwa madai kuwa  yeye hataki kuandikwa wala kutangazwa kwenye vyombo vya habari
Ngudungi amesema  haoni haja  ya kufanya kazi na vyombo vya habari kwa sababu baadhi ya  waandishi wanapotosha jamii kwa kuripoti taarifa zisizo sahihi hali ambayo  inapelekea  kulaumiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa
“Nilitumwa kufanya kazi za wananchi sio na waandishi wa habari wananchi wakishaona ninawafanyia nini inatosha” aliongeza mwandishi anayepewa habari na kuiandika kinyume na jinsi alivyopewa siwezi kushirikiana naye” Alisema
Akizungumza na wanahabari wenzake nje ya ofisi ya mkurugenzi huyo mwandishi huyo amesema alifika kutaka kujua idadi ya vituo vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani humo na jinsi kampeni zilivyo na changamoto zake
 Ndyamukama amesema kwa kuzingatia na kufuata misingi ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu  wananchi wanayo haki ya kupata habari kupitia chombo chochote cha habari kama vile Radio Magazeti na Luninga
Imedaiwa kuwa mwanahabari huyo aliandika taarifa za mmoja wa wafanyakazi kazi wa kituo cha Afya cha Lukole aliyetuhumiwa kuwapiga  wagonjwa na kwamba taarifa hizo zilikuwa bado kuhakikiwa na mkurugenzi huyo
Hata hivyo mkuu wa mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu amelaani kitendo hicho cha mwanahabari kufukuzwa akitafuta taariza za maendeleo ya wananchi na kudai kuwa atafuatilia kujiridhisha ili hatua zichukuliwe
“Kama hali hiyo imejitokeza badi mkurugenzi anahitaji kuelimishwa kwani wananchi wana haki ya kupewa taarifa za maendeleo ya halmashauri na masuala mengfineyo kwenye wilaya yao” Alisema Kanyasu
Pamoja na hayo imefahamika kuwa baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wakiwemo wakuu wa idara hawana mamlaka ya kutoa taarifa za maendeleo kwenye vitengo vyao na kusababisha baadhi yao kulalamikiwa na wananchi.
Wilaya  ya Ngara inavyo vijiji 75 vyenye  vitongoji 394 vitakavyotumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa  na idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 133,317  sawa na 134%  kati ya  walengwa  99, 259  kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 .

''MASIKINI HALALI MCHANA'' WAUZAJI WA VIFAA BORA VYA UMEME MJINI BUKOBA

$
0
0
 Masikini halali mchana  ni duka la umeme limejikita katika usambazaji wa vifaa halisi (Orijino) vya umeme na korokoro zake zote,Ni wauzaji wa rejareja na jumla kwa bei nafuu na stahiki.
 'Masikini halali mchana'wana bidhaa za kutosha za vifaa aina mbalimbali vya Umeme, wanapatikana  Mtaa wa Migeyo ndani ya Manispaa ya Mji Bukoba
 Pichani anaonekana Mkurugenzi wa Duka la 'Masikini halali mchana' akiwa anajifaharisha kuuza vifaa vya umeme vya kisasa vinavyopatikana dukani hapo ambavyo ni pamoja na taa za aina zote, soketi, nyaya ,Solar pamoja na vipozeo umeme mbalimbali
 pia linaweza kuhudumia wateja waliopo nje ya Mji wa Bukoba kwa kufanya mawasiliano ya moja kwa moja kupitia anwani na simu zao. Hivyo wana uwezo wa kukufikishia mzigo ukiwa katika hali nzuri na salama bila kupata tatizo lolote kwani uaminifu kwao ndio kitu cha upekee
 kwa vifaa bora na vya uhakika vya Umeme fika Mtaa wa Migeyo walipo 'Masikini halali Mchana
Jipatie ving;'amzi vya star timesVifaa vya Solar ,Vifaa vya Umeme na Vyombo mbalimbali vya Electroniki ndani ya Masikini halali Mchana
 Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja na mabadiliko ya matumizi ya bidhaa na vifaa vinavyoendana na wakati uliopo sasa hilo linathibitishwa na Masikini halali mchana kwa kuuza bidhaa na mahitaji ya kisasa
 Katika hili na lile kama inavyo onewkana pichani
Hivyo Usihangaike tena kutafuta vifaa umeme pamoja na Ving'amuzi kwani Ukifika 'Masikini halali mchana' unauhakika wa kupata bidhaa bora zenye kiwango kinachokidhi mahitaji

FIKA YUMMY'S GROCERY KWA MAHITAJI YAKO YA NYUMBANI

$
0
0
Mjini Bukoba Unaweza kupata Mahitaji yako ya nyumbani kwa bidhaa bora na halisi  ukifika Yumm's Grocery waliopo  mtaa wa Kawawa/Postal Road jirani kabisa na Jengo la ELCT.
Ndani ya  YUMMY'S GROCERY ni chaguo sahihi kwa mahitaji yote muhimu kwa matumizi ya binadamu, kuanzia vyakula, mboga, vifaa vya nyumbani, sokoni, maofisini, mashuleni...you name it!
Tunakutana na Shop manager akiwa katulia ,ile tunataka kujua kuna nini anaanza kutaja bidhaa mpaka sasa hivi anaendelea...anasema kuna snacks kama ice cream, chocolate, biskuti ,soda sambusa Chips kwa nje, senene ,maziwa nk bila kusahau  Matunda aina mbalimbali  
Mdau msomaji bila tufahamu wazi kuwa mahitaji ya nyumbani kama chakula, ni ya lazima katika kuhakikisha ustawi wa familia tembelea sasa YUMMY'S GROCERY upate kufanya Manunuzi yako ya bidhaa za nyumbani kama mchele, sukari ,dawa ya mboga (chumvi) , unga wa mahindi na ngano, sabuni, mafuta ya kupikia, na vingine vingi, muendelezo wa picha zifuatazo chini zinajieleza
 Jambo moja inabidi tutambue kuwa sehemu kubwa ya dunia aina ya raw materials za vyakula ni ile ile lakini namna ya upatikanaji na upikaji ndio hutofautiana...Je unajua kilipo Kichuguu cha Senene?!
 YUMMY'S GROCERY: MAARUFU KWA MR. KIRAJA- wapo Kawawa/Postal Road jirani na  Msikiti wa Ijumaa  usawa wa ofisi za Kadetfu zilizopo katika Jengo la ELCT UJIRANI MWEMA katikati ya Mji wa Bukoba 
 Jamaa aliendea kutaja bidhaa  mpaka mteja unaweza kuingia shaka....!!
Kwa kifupi ni kwamba jamaa wamejipanga wapo kisasa zaidi  vitu vya urembo kama kawaida,perfumes, saa za ukutani na saa za mikononi ,vifaa kwa ajili ya kufanyia usafi hadi vifaa vya  kuchezea watoto.
 Muonekano wa bidhaa mbalimbali
 Hapo YUMMY'S GROCERY unapata michomo safi kabisa ,Nyama,kuku,chips ,mayai nk.
Yaani full hekaheka...
YUMMY'S GROCERY ..WE ARE COMMITTED TO SERVE YOU!!!

RAIS DK JAKAYA KIKWETE ATUNUKU NISHANI YA MIAKA 50 YA MUUNGANO IKULU DAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la tatu Amani Issack Abraham Sepetu kwa niaba ya Baba yake Issack Abraham Sepetu (marehemu) katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la pili Augustino Stephene Ramadhan katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la pili Mohammed Fakih Mohammed katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la pili Ali Salum Ahmed katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne Bibi Johari Yussufu Akida katika hafla kutunuku nishani iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne Haji Machano  Haji  katika hafla kutunuku nishani iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (kutoka kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda wakiwa  hafla kutunuku nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la tatu Ali Ameir Mohamed katika hafla kutunuku nishani iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara juzi.Picha na Ikulu.

MKUU MPYA WA MKOA WA KAGERA AJITAMBULISHA WILAYANI NA KUKAGUA UJENZI WA MAABARA PAMOJA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella atembelea Halamashauri za Wilaya za Mkoa wa Kagera kujitambulisha kwa  Madiwani, Watendaji wa halmashauri  za Wilaya pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni pamojana kukagua ujenzi wa maabara katika shule zote za serikali.
Ziara hiyo ilianza Desemba 4, 2014 katika Wilaya ya Missenyi  na kufuatiwa Wilaya za Muleba Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo. Mkuu wa Mkoa John Mongella alitumia nafasi hiyo kuijimbulisha pia kutoa ufafanunuzi wa majukumu makuu na muhimu ya mkuu wa mkoa katika nafasi yake.

Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo katika mkoa, kusimamia ulinzi na usalama katika mkoa na jukumu la tatu ni kusimamia utii wa sheria katika mkoa. Katika mikutano aliyoifanya na wadau na watendaji wa Halmashauri aliyatolea ufafanuzi kwa ufasaha majukumu yake.
Katika kutekeleza majuku yake mkuu huyo wa mkoa alifafanua zaidi  juu ya uwajibikaji wa watendaji wa serikali kwa kutumia mfumo uliopo kutoa  huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri za Wilaya kwa kila mtendaji kuwajibika katika nafasi yake ya kazi  aliopo.
 John Mongella  alitoa onyo kali kwa watendaji wa Halmashauri ambao hawatimizi wajibu wao wa kwenda  vijijini kufuatilia maendeleo ya wananchi, alisema atakikisha anawachukulia hatua kali pale itakapobainika kuwa kazi yao ni kushinda ofisini bila kwenda kwa wananchi.
Aidha alitoa maelekezo kwa watendaji wa kata na madiwani  kuwa na siku maalum za kwenda katika halmashauri zao na siyo kila siku kushinda katika ofisi za Wakurugenzi na kufanya kazi za wataalamu. Pia aliwaagiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri nao kutenga siku za kukukaa ofisini na siku za kwenda vijijini kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya ofisi zao.
Ujenzi wa Maabara: Mkuu wa Mkoa John Mongella pia alitembelea na kukagua ujenzi wa maabara tatu kila shule ya serikali unavyotekelezwa mkoani Kagera ambapo mwisho wa kukabidhi maabara hizo ulikuwa Desemba 9, 2014 kulingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete la mwaka jana Februari 2013.
Katika Halmashauri za Wilaya za Missenyi, Muleba, Kyerwa, Karagwe, Ngara na Biharamulo ujenzi wa maabara katika shule zote za serikali unaendelea ambapo vyumba  vitatu vya masomo ya Fizikia, Kemia na Biologia vinaendelea kukamilishwa ikiwa ni pamoja na miundombinu ya maji na gesi ndani yake.
 Mkuu wa mkoa John Mongella pamoja na kukuagua na kupima na kuhakikisha maabara hizo zinajengwa kwa kufuata michoro ya serikali pia alikuwa akijihakikishia kama vipimo vinafuatwa na kila kitu kinachooneshwa kwenye ramani za majengo hayo kimewekwa kama ramani inavyoonesha,  aidha aliagiza ifikapo January 2015 kila maabara iwe imekamilika tayari kwa  wanafunzi kuzitumia maabara hizo.
Miradi ya Maji: Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella hakusita kukagua miradi ya maendeleo ambayo imeshindwa kukamilika kwa mwakati hususani miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya  ya Muleba  ya vijiji 10 na miradi ya Quick win katika vijiji vinne vya Kamachumu, Izigo, Rwanda na Itoju.
Katika miradi hiyo ambayo tayari serikali imetoa mamilioni ya fedha imeshindwa kukamilika kwa  wakati na kupelekea wananchi katika maeneo hayo kuendelea kupata adha ya maji jambao ambalo lilimfanya Mkuu huyo Mkoa kuwaagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kumpelekea taarifa baadaya wiki mbili.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkuu wa Mkoa John Mongella alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha mradi wa maji wa Ngara mjini unakamilika na kufanya kazi ifikapo  Januari 30, 2015 mara baada ya kugundua kuwa tayari milioni 30 zilitumika ndivyo sivyo.
Aidha alimwagiza mweka hazina wa halmashauri hiyo kuhakikisha mapato ya ndani ya mwezi Desemba 2014 yanaelekezwa katika mradi huo ili huduma ya maji ipatikane haraka katika mji wa Ngara. Pia Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngara kuhakikisha anasimamia kesi ya ubadhilifu wa milioni 30 ili mhusika awajibishwe kisheria.

MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA KAGERA FARMERS CO-OPERATIVE BANK (KFCB) LTD WAFANYIKA DEC 11,2014 MJINI BUKOBA

$
0
0
Mkutano mkuu wa kawaida wa kumi na tano wa Kagera Farmers Co-Operative Bank (KFCB)Ltd uliofanyika tarehe 11/12/2014 katika ukumbi wa Bukoba Co-Op hotel zamani (Yaasila) uliopo ndani ya Manispaa ya Bukoba ,Mgeni rasmi alikuwa Mrajis wa vyama vya ushirika Nchini.
 Pichani ni wajumbe wa Bodi ya (KFCB)yenye jumla ya wajumbe watano wakiwa ni watatu wa kuchaguliwa na wawili wa kuteuliwa.
Wengine walio hudhuria Mkutano huo ni pamoja na Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kagera,wawakilishi kutoka Benki kuu ya Tanzania ,wajumbe wa mkutano mkuu na waalikwa mbalimbali.
 Mwenyekiti wa (KFCB) Gozbart Rugumila akiongoza mkutano huo.
Aidha katika mkutano  aliweza kutengua Bodi ya wajumbe watano imepanguliwa na kufanyika uchaguzi  mpya ulio simamiwa na  Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Kagera pichani .,Uchaguzi ambao  wajumbe watatu waliweza kuchaguliwa.
Waliochaguliwa  ni Mwenyekiti Ndugu Gozbart Rugumila naTheonest Rutamingwa kuwa makamu mwenyekiti ,mjumbe wa tatu ni Mr. Pius Mushuga .
 Taswira meza kuu
 Akiongea mbele ya Mgeni Rasmi ,Mwenyekiti wa bodi amesema;''Ninaamini umeishapata maelezo mafupi kuhusu benki yetu na huenda  umebaini kuwa changamoto  kubwa tulionayo ni ufinyu wa mtaji,wenye mali kutotumia benki yao katika shughuli zao za kibenki ikiwa ni pamoja na kufunga akaunti zao na kuhamia benki nyingine''
Swala la Mtaji limekuwa likiongelewa katika kila kikao cha mkutano Mkuu.
Mpaka sasa benki ina jumla ya mtaji wa Tshs.2,011,660,000.Mtaji ambao ni mdogo sana kulingana na changamoto za biashara ya kibenki yenye ushindani mkubwa.
Mwenyekiti anaendelea kusema kuwa;..Swala la wanahisa kuongeza hisa licha ya kuwa la lazima kwa mujibu wa sheria,ni muhimu pia kwa biashara ya benki kwani uwezo wa benki kufanya biasha ambapo biashara kuu ni kukopesha kunahitaji mtaji mkubwa.
Kulingana na changamoto kadha wa kadha ,benki imeshindwwa kupata faida kwa ama matumizi ya kudumu au yasiyobadilika kuwa makubwa tofauti na kipato kinachopatikana,Matumizi hayo hasa ni mishahara ya wafanyakazi na maslahi yao mengine. 
Kwa kuzingatia hali hio benki imeamua kupunguza matumizi ya uendeshaji ikiwami pamoja na wafanyakazi na utaratibu unaendelea.
'Benki inaamini wafanyakazi watakaobaki watafanya kazi kwa ufanisi na kuifanya benki itengeneze faida'pichani anaonekana Mr. Maluma afisa mikopo (KFCB)
Mjumbe  akijaribu kutoa ushauri kutokana na maelezo yaliyo tolewa juu  kudorora kwa uchumi duniani mwaka 2008 na kupelekea benki ya KFCB kuto kutengamaa kama ilivyo kusudia.
 Kaimu meneja mkuu wa Benki ya KFCB akitolea jambo ufafanuzi
Mjumbe akiuliza swali 
 Meneja wa (KFCB) akifafanua hali ya changamoto zilizopo kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ushirika na ujasiriamali na elimu ya kuheshimu mikataba ya mikopo kwa wateja  sambamba na juhudi mbalimbali zilizofanyika katika kukusanya madeni mbalimbali
 Sehemu ya wanahabari
 Mmoja wa Staff Benki ya wakulima ya mkoa wa Kagera (KFCB Ltd).
 Mwakilishi kutoka benki kuu ya Tanzania (BOT) akitolea jambo ufafanuzi
 Kushoto ni Bw Frank Muganyizi mwenyekiti mpya wa KCU (1990)Ltd ,anaye fuata ni Meneja Mkuu wa KCU (1990)Ltd  Ndugu Vedasto Ngaiza
Ni mkutano mkuu wa kawaida wa kumi na tano wa Kagera Farmers Co-0perative Bank (KFCB)
 Wajumbe wa mkutano mkuu kutoka  maeneo mbalimbali wakiendelea kuuliza maswali.
 Kwa umakini mkubwa wajumbe wakipitia  makaburasha
Benki pia ina mkataba na mfuko wa pembejeo wa kukopesha fedha kwa ajili ya pembejeo za kilimo.
Mjumbe akichangia swala la Umuhimu wa Saccos
 Mzee wa kazi Mc Lutakwa kama anavyo onekana pichani.
Muonekano wa wajumbe mkutano ukiendelea.
 Wakati mchakato wa kura unaendelea
Camera etu ikicheck na wadau walio hudhuria mkutano huu.
Muonekano wa Wajumbe wakati mkutano ukiendelea.
 Mwakilishi wa NSSF.
Mwakilishi kutoka ofisi  ya Mrajisi wa vyama vya ushirika Nchini
 Ndugu Rugumira ambaye ndiye mwenekiti wakati akiomba tena nafasi hiyo
Mjumbe mpya katika bodi ya KFCB  Ndugu Pius Mushuga pichani kulia wakati akijinadi
 Mwisho Mwenyekiti na wajumbe wa bodi wanatoa shukrani za dhati kwa Idara ya maendeleo ya Ushirika kwa ushirikiano mkubwa walionao ikiwa ni pamoja na Uongozi wa 'UNION' KCU (1990)Ltd  na mfuko wa udhamini wa mazao (KFTF)
Bango la Bukoba Co-Op hotel
 Sehemu ya Maegesho.

HAFLA YA KUMPONGEZA MWL-MARTHA BISHANGA YAFANA NDANI YA BUKOBA CO-OP..!!

$
0
0


Hafla ya kumpongeza Mwl. Martha Bishanga kwa kustaafu utumishi wa Umma yafana Sana,Hafla hii imefanyika Usiku wa jana Dec 12,katika Ukumbi wa Bukoba Co-Op Hotel.
 Mwalimu Martha Bishanga pichani kushoto na mpambe wake,ambaye ni rafiki yake karibu Mama Matungwa mtaalam wa  Decoration::Advents Deco and Planning kama mtakavyo jionea kumbi umepambwa na kupambika ipasavyo
Mara baada ya mstaafu kuingia ukumbini, Shughuli ikafunguliwa kwa sala takatifu iliyo ongozwa na Bi  Mecktrida Michael Pichani
 EEEE BANA EEEE Muonekano wa Kitu Keki iliyotengenezwa na mtaalam wa fani Mama Simeo!!
 Jamani pale kwenye kutoa sifa mtu na apewe sifa zake BUKOBAWADAU tunachoweza kusema hii ya leo ni  kiboko Kwa Keki..Ni Sheeedah !!
 Bi Georgia Kalikawe na Mama Lugusha pichani ni sehemu ya waalikwa
Meza mbalimbali za waalikwa walio hudhuria hafla hii ndani ya Ukumbi wa Bukoba Co-Op,
 Kushoto ni Mh. Anathory Aman na Mkewe.
  Kutoka katika familia za kichief  ni Bi Anitha Rugalabamu na Mr Devo Rugaibura (Mr & Mrs Divo.
 Kuvaa ni njia mojawapo ya kujiamini kwa mwanamke,Pichani anaonekana Bibie Laty katika 'Smile' Mtoto mkalee, mtoto msomi, ana pozi na muelewa!
 Muonekano wa meza mbalimbali za waalikwa ukumbini.
 Mwalimu Martha Bishanga akitoa Utambulisho.
Watoto wa Mstaafu Mwalimu Martha  Bishanga pichani
Walimu wenzake katika Utambulisho
 Pichani kulia anaonekana Mr. Mkayo
 Kwa vazi hili Credit kwako  Dada Hope Kazimbazi wa Makoko maarufu kama Manywele,tunakupa Credit kwa sababu kuna watu wanashindwa kutofautisha nguo ya kuvaa disco na kwenye party..!!
Katika hili na lile ndivyo mambo yanavyo endelea ukumbini hapo.
 Mr & Mrs Anathor Amani wanapokea zawadi yao ya Keki
 Zawadi kwa Kaka yake ambaye ndiye kiongozi wa Ukoo Dr. Bishanga.
Kwa niaba ya Mme wake Mzee Ngaiza Meneja wa KCU (1990)Zawadi inapokelewa na mwane mkubwa  Ndugu Rweyemamu Victar Ngaiza
 Mdau Samuel Stephen mwenyekiti wa Kamati ya Chakula mara baada ya kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya kamati nzima ya maandalizi ya hafla hii.
Shughuli ya kukabidhi zaidi ya Keki 20 kwa ndugu jamaa na marafiki likiendelea kwa kasi.
 Walimu wa Shule ya msingi Kashai,Shule aliyokuwa anafundisha Mwalimu Bishanga hadi kustaafu .
 Mama Adventina matungwa akipokea zawadi yake ya Keki
 Bi Editha  katibu wa kamati ya maandalizi akikabidhiwa zawadi yake ya Keki
 Watoto na wajukuu wa Mwalimu  Martha Bishanga katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya Keki
Sehemu ya Watoto wa kuzaliwa na Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga.
Mama Semeo na Mama Matungwa katika hili na lile wakati Mstaafu akiendelea kukabidhi zawadi ya keki kwa makundi mbalimbali kulingana na umuhimu katika maisha yake ya kazi mpaka kustaafu
Kuhusiana na Keki jamani  mchakato ukiendelea
 Juu ya Keki Hongera Sanamama Simeo,hongera  Dada Angel na kamati yamaandalizi.
 Anaonekana Bibie Editha wa Nicodemus kama kawaida ni mtu tabasamu wakati wote.
Kivutio kingine katika hafla hii ni Wanamama walivyo onyesha umahiri wa kufungua  champagne.
 Wakimpongeza mama yao mzazi
 Bi Anjoy mara baada ya kumpongeza Mama yake Mzazi
 Anaitwa Jamal Kalumuna
 Bi Sharifa wa Athman ShaR wa Badru Mangi Saidi
 Bi Jamila Jamal pichani kulia.
 Pongezi zikiendelea kumiminika
Hakika watu wote wanaonekana wenye furaha katika kumpongeza mstaafu Mwalimu Bishanga.
Katika kuzoom anaonekana Mdau akifanya 'kutweet'
Mwanadada Sarah pichani
 Katika hili na lile ndivyo anavyo onekana mmoja wa waalikwa Ukumbini
Kundi maarufu la Mwanadada Mery likiendelea kutoa burudani safi ya Ngoma za asili.
 Star wa Usiku huu alikuwa  Mr. Kilangani, aliyeweza kutoa historia ya Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga kwa njia ya ushairi  yaani sauti iliyo kati ya kuimba na kuongea tena kwa lugha ya asili "Kihaya'
Kibwakizo kikubwa katika ushairi huo kinasema ...'Martha Akanganyira Owomulikubona Omumaisho ganyu, Mwana wa ta Sebastiani Bishanga na ma Paulina Kokunywegeza, Omwabo ni Kiziba Kanyigo Omukyaro kwa Kikukwe...
 'Orugandarwe Mulwanikazi nazira Ente ya Runya,naruga  omumalembo nyarutembo... 'Endelea kuwa nasi mpaka mwisho kwa ushairi kamili hapo badae.
 Mh. Aman mara baada ya kukabidhi zawadi yake ,anampongeza Mstaafu Mwalimu Bishanga
 Mwanadada Hope mara  baada ya kukabidhi zawadi yake kwa mstaafu
Mzee Mshashu akikabidhi zawadi yake
 Walimu wa Shule ya Msingi Kashai wakiwa na zawadi yao
 Bi Angel akiongea kama muweka hazina wa kamati ya maandalizi
Athman na Murshid wakifanya mawasiliano
 Wanafamilia wakishusha bonge laburudani
 Burudani kutoka kwa wanafamilia ikiendelea.
 Sehemu ya Waalikwa wakipata msosi
 Utaratibu wa kupata huduma ya Chakula ukiendelea..
 Ndugu Athmani Bahati akipati mulo safi.
 Taswira mbalimbali mapema kabla ya sherehe ya kumpongeza Mwl-Martha Bishanga kuanza.
 Wakati Bi Husna Khaldi anaingia Ukumbini
 Wakati familia ya Mama Seleda ikiingia Ukumbini
 Mwanzoni wakiingia Ukumbini walimu wa Shule ya Sekondari Kashai
 Upande wa Mapokezi
 Dada Angel  akiwajibika 
KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA  2oo INGIA HAPA>>Bukobawadau Entertainment Media

CHRISTIAN BELLA & MALAIKA BAND KUFANYA YAO NDANI LINAS NIGHT CLUB - DEC 26,2014!

$
0
0
BENDI ya muziki wa Dansi ya Malaika chini ya Christian Bella 'Obama' Mzee wa masauti, Christian Bella 'Obama' kufanya yake ndani ya Linas Night Club usiku wa tarehe 26,12,2014 hii ni Sheedah nyingine kwa wakazi wa Mji wa Bukoba na Viunga vyake
Unaambiwa ata ukiwa na njaa basi  Ukimsikiliza Christian Bella (njaa kwisha kabisa)kutoka na uwezo wake na Style ya kipekee kwenye muziki wa dansi!

UKUMBI MPYA ANGELINA SOCIAL HALL KUZINDULIWA DEC 26,2014

$
0
0
Angelina Social Hall ni ukumbi mpya wa sherehe mbalimbali na mikutano wenye kila sifa na kila kitu cha kisasa kuzinduliwa Dec 26,2014 Mjini Bukoba maeneo ya Rwamishenye /Kiteyangwa .
Mgeni Rasmi atakuwa Mh.Balozi Khamis Kagasheki ,Mbunge wa Bukoba Mjini.
Angelina Social Hall ni Ukumbi wenye uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 1000 waliokaa kwenye viti umetengenezwa kisasa zaidi na kuongeza nakhish ndani ya Manispaa Bukoba.
 ANGELINA SOCIAL HALL IN BUKOBA MUNICIPALITY GLAND OPENING CEREMONY FRIDAY 26th/DEC/2014 ,LOCATED IN RWAMISHENYE/KITEYAGWA AREA, ALONG THE ROAD TO PEACE SECONDARY SCHOOL.
THE HON. AMBASSADOR KHAMIS SUED KAGASHEKI TO BE A GUEST OF HONOUR
 MUHIMU:BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241

KARATASI ZA KUPIGIA KURA ZANASWA D'SALAAM

$
0
0
 Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho nchini kote. Picha na Venance Nestory
Dar es Salaam. Wakati Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukitarajiwa kufanyika kesho nchi nzima, wafuasi wa (Chadema) na Jeshi la Polisi, wamekamata karatasi zinazodaiwa za kupigia kura kwenye uchaguzi huo za Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, zikirudufiwa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Jimbo la Ubungo, Justine Mollel, tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati mwanachama wa chama hicho alipokwenda katika duka la vifaa vya shule na ofisini saa 8 mchana kwa lengo la kurudufu karatasi za chama hicho lakini aliambiwa arudi saa 12 jioni.
Gazeti hili lilifanikiwa kuiona moja ya nakala hizo kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ikiwa na nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ikiwa na nafasi ya kupigia kura kwa wagombea wa CCM na Chadema.
Habari zaidi zinaeleza kuwa tayari zaidi ya nakala milioni moja zilisharudufiwa, huku zikiwa zimewekwa alama ya ndiyo kwa mmoja wa wagombea wa vyama hivyo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema: “Uchunguzi bado unaendelea kwani waliokuwa wanarudufu walijitambulisha kuwa ni wasimamizi wa uchaguzi, hivyo tunaendelea na uchunguzi na hakuna mtu tunayemshikilia.”
Aliongeza: “Nimemwagiza OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya) kuwasiliana na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) ili kujua hizo karatasi ni kweli zilitakiwa kutengenezwa hapo au la... Kama ni hapo mambo yaishie palepale na kama siyo halali basi hatua zichukuliwe kwa wahusika.”
Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Khalist Luanda alisema kurudufu karatasi za kupigia kura kunatakiwa kufanyika katika wilaya au mkoa lakini siyo nje ya mkoa.
“Ni kosa kuchapa fomu za wagombea kutoka wilaya moja kwenda nyingine walipaswa kurudufu katika eneo kunapofanyika uchaguzi au wilaya husika na mchakato unaopaswa kuwa wa siri sana na siyo kila sehemu kwani haitakuwa rahisi kusafirisha kwa usalama bila kutiliwa shaka.”
Aliongeza kuwa: “Nimesikia katika vyombo vya habari na nimetuma wataalamu wangu kwenda kufuatilia jambo hilo kwani ni makosa na mkurugenzi huyo inaonyesha alikuwa na malengo au masilahi binafsi na kama ni kweli anatakiwa kuwajibika.”
Awali akisimulia tukio hilo Mollel alisema: MwanaChadema alikwenda pale kurudufu karatasi zake kwani gharama yake ni Sh25 kwa karatasi moja na aliambiwa arudi jioni kwani walikuwa na kazi maalumu, hivyo wasingeweza kumrudufia karatasi zake.”
Aliongeza: “Alipokwenda tena saa 12 aliambiwa bado hawajamaliza kazi hiyo maalumu hapo alipata hofu na kuanza kuchunguza kazi iliyokuwa ikifanyika, ndipo alipoona karatasi za kupigia kura zikirudufiwa.”
Mollel alifafanua kuwa alipoona hivyo mfuasi huyo aliwaita wanachama wengine wa Chadema waliozingira duka hilo lililopo maeneo ya Mabibo kabla ya kutoa taarifa Kituo cha Polisi Mabibo umbali wa takriban mita 100.

NECTA YATANGAZA MFUMO MPYA

$
0
0
Dodoma. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limeanza mfumo mpya wa kupanga matokeo ya kidato cha nne mwaka huu na ya kidato cha sita mwakani, ambapo sasa madaraja yatapangwa kwa wastani wa pointi (GPA) badala ya jumla ya pointi.
 Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Charles Msonde katika mkutano wa wadau wa kampeni ya elimu kwa watoto wa kike walio katika mazingira magumu (Camfed).
Dk Msonde alikuwa akitoa mada kuhusu uwekaji alama za ufaulu unaotekelezwa na Necta.
Alisema mfumo huo siyo mpya kutumiwa na Necta kwa sababu umekuwa ukitumiwa katika kupanga matokeo ya wanafunzi wa vyuo vya walimu.
“Mfumo utakaotumika kupanga madaraja ya mitihani kwa wanafunzi wa kidato cha nne wa mwaka huu na kidato cha sita mwakani na kuendelea utakuwa si ule wa kutumia jumla ya pointi badala yake utakuwa ni wastani wa pointi,” alisema na kuongeza:
“Utaratibu huu siyo kwamba ni mpya kwa baraza la mitihani, tumefanya hivyo kwa matokeo ya ualimu na hata tunapopanga shule bora tumekuwa tukitumia GPA... Hatubadilishi thamani ya madaraja.”
Alisema kuwa thamani ya madaraja itabaki kuwa ni ile ile bali sasa watakuwa na mfumo unaolingana na kupanga matokeo ya ualimu.
Dk Msonde alisema lengo la kutumia mfumo huo ni kuwezesha kuwa na mfumo unaofanana katika ngazi zote za elimu nchini.
“Lengo jingine ni kuwarahisishia wenzetu wa TCU na Necta na wadahili wengine wawe wanatumia mfumo unaofanana na wa kwetu wasianze tena kubadilisha vyeti,”alisema.
Alisema lengo lingine ni kuelimisha Watanzania kuhusu mfumo huo mpya wa upangaji wa matokeo.
ya mtihani ambapo kwa kutumia mfumo wa jumla ya pointi ilikuwa ni vigumu kuuelewa.
Dk. Msonde alisema kwa mfumo wa kutumia jumla ya pointi watanzania wengi walikuwa wanafikiri mtu akipata pointi nyingi ndio amefaulu zaidi ya wale waliopata pointi chache.
 Alisema tayari wametoa mafunzo ya uelewa juu ya mfumo huo kwa wadau mbalimbali wa elimu na kwamba wanautambua.
MWANANCHI

HII INAHUSU 'BUKOBA CORNIVAL' FUKWENI KIROYERA DEC 20,2014

$
0
0
BUKOBA;tarehe 20 ni siku ya kujiachia fukweni Kiroyera
 Burudani mbalimbali zitakuwa zikiendelea pamoja nawageni wengi maalum,Jipange  kwa shangwe mpya zenye ubunifu wa kutosha!
 Pamoja na mambo mengine yote yatakayo endelea kuna wakati, utataka mwisho wa siku uwe na kumbukumbu bora ya siku hiyo,basi Bukobawadau na timu nzima ya Nyumbani Studio wale Wataalam wenye uwezo na kipaji cha kupiga picha na kuedit watakuwepo
 Nyumbani Studio inakufanya unukie kiujana zaidi hata kama age yako imeenda
 Mc Baraka & Ally

 BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241

HADITHI YA KUSISIMUA:MKE WANGU NUSU JINI,NUSU MTU!!

$
0
0
“Niliwahi kujiuliza kama iko siku na mimi nitapata nafasi ya kusimulia popote pale mkasa uliowahi kunikumba miaka ya nyuma. Ni kuhusu mke wangu niliyefunga naye ndoa ya serikali. Nilibaini kwamba alikuwa mtu lakini pia alikuwa jini kwa sababu mbalimbali,” anasema Abigaeli, mkazi wa Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Anaendelea: “Siku ya kwanza kukutana na mke wangu ilikuwa kwenye kikao cha kupokea mahari ya mtoto wa kaka yangu aliyekuwa anataka kuolewa na Msambaa mmoja kutoka Lushoto, Tanga. Ilikuwa mwaka 2002.

Kuna kitu kilitokea kwenye kikao hicho na kama ningekuwa makini, nisingeingia kwenye matatizo makubwa yaliyowahi kunipata katika maisha yangu.Kitu hicho ni kwamba, baada ya kikao, msichana mrembo ambaye alikuja kuwa mke wangu alinifuata na kuniomba namba zangu za simu, nikamtajia, akaziingiza kwenye simu yake.

Alipoondoka, baadhi ya ndugu tuliokuwa pale tuliulizana yule msichana ni nani. Hakuna aliyekuwa na jibu. Bahati nzuri ndugu mmoja wa upande wa mwanaume aliyeleta mahari alikuwa hajaondoka, tukamuuliza kama walikuja na msichana yule, akakataa kutomtambua tena huku akisisitiza kwamba, walikuja kumi tu na yeye ndiye alibaki kumalizia mambo mengine.

Kaka aliniuliza aliponifuata kuniomba namba ya simu alisema anatokea upande gani katika tukio lile, nikamwambia kwa waleta mahari.Nilianza kuingiwa na wasiwasi tena mkubwa, niliwaza mengi. Kaka akanilaumu kwamba, siku nyingine nisikubali mawasiliano na watu ambao hawajulikani sawasawa. Lakini nilijitetea kwamba, mtu kusema kaja na watu wengine ambao kweli walikuwepo sidhani kama unaweza kumtilia shaka.

Wiki moja baada ya tukio hilo la kushangaza, nilipigiwa simu na mtu aliyedai kuwa yeye ndiye yule msichana, akasema anaitwa Munil. Alisema amenipigia simu ili kunijulisha kwamba, yule mchumba aliyekuja kutoa mahari kwa kaka amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea nusu saa iliyopita.
Nilishtuka sana kwani zilikuwa taarifa za ghafla sana kwangu.

Lakini jambo lingine sasa, niliamini yule msichana ni ndugu na wale walioleta mahari ila pengine yule mtu wa mwisho hakumjua.Nilimshukuru kwa taarifa kisha akakata simu. Nikampigia kaka kumuuliza kama analijua hilo, naye alishtuka sana akasema hajasikia, akaomba nimpe dakika tano tu ahakikishe kwa ndugu wengine halafu atanirudia. Lakini kaka hakuniuliza nilikozitoa habari zile.

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kesho usiku..........
Viewing all 4180 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>