Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all 4180 articles
Browse latest View live

ROLENE STRAUSS WA SOUTH AFRICA NDIYE MISS WORLD 2014

$
0
0
Miss South Africa Rolene Strauss mwenye umri wa miaka 22 amefanikiwa kutwa taji la Miss World 2014 ,mshindi wa pili katika shindano hilo lililofanyika usiku wa leo Dec 14,Jijijni London ni Miss Hungary, Edina Kulcsar, naye Mrembo kutoka kwa Obama ,Miss United States, Elizabeth Safrit,amefanikiwa kuwa mshindi wa tatu.
 Miss Gabon, Miss Ethiopia, Miss Curacao and Miss Chad katikati ya jukwaa.
 Mchuano ukiendelea kwa Washiriki kutoka mataifa 120 ambapo Mshiriki kutoka Thailand ndiye mshindi wa 'People Choice' nafasi pekee aliyo itegemea mshiriki kutoka Tanzania  Miss Happiness Watimanywa.
Ifuatayo ni orodha ya kumi bora  (Top 10)1st Place - INDIA ,2nd Place - SOUTH AFRICA,
3rd Place - ENGLAND,4th Place - GUYANA,5th Place - BRAZIL, 6th Place - HUNGARY,7th Place - KENYA,8th Place - UNITED STATES,9th Place - MEXICO,10th Place - AUSTRALIA

MUHIMU :BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Beauty with a Purpose Winners Pics!
 Miss Japan Hikaru Kawai (left) and Miss South Korea Song Hwa-young get their moment in the limelight
Miss Tukery and Miss Zimababwe lead contestants across the stage
 Miss Serbia Milica Vuklis (centre) parades between Miss Vietnam Loan Nguyen Thi (right) and Miss Montenegro Natasa Novakovic
Andrea Forfori Aguilera, Miss Bolivia, looks ready to fight for the crown.
 Miss Thailand Maeya Nonthawan shows off her flexibility
Contestants dance in national costumes during the grand final of the Miss World 2014 pageant at the Excel London ICC Auditorium
 LMFAO's Sky Blu croons his new single We Love Girls! as Miss United States Elizabeth Safri strides past
 The contestants enjoyed a bit of downtime during the pageant, changing into LBD's and dancing along to The Vamps
Miss Mongolia Battsetseg Turbat
 Former Blue Peter presenter Tim Vincent hosted this year's contest alongside the reigning 2013 Miss World Megan Young
Finally, after much deliberation, Rolene Strauss of South Africa was named the winner
Miss England and Miss Australia congratulate the new Miss World
 Miss World with her runners-up Miss Hungary Edina Kulcsar and Miss United States Elizabeth Safrit
 The new Miss World is a 22-year-old medical student
Rolene received the Miss World crown from 2013 winner Megan Young
 Miss World 2014 Is............. Rolene Strauss SOUTH AFRICA!!!!!!!! 
  Miss World with her runners-up Miss Hungary Edina Kulcsar and Miss United States Elizabeth Safrit
According to her Miss World biography, Rolene enjoys playing golf, netball and cycling, and reading inspirational and educational books. She is also musically minded, and can play the flute, piano and guitar
Ellie McKeating representing Scotland performed a wee Highland fling
 Miss Slovenia Julija Bizjak
 Miss France Flora Coquerel
Miss India Koyal Rana
 Following the national costume section, the women then paraded in their evening gowns. Here's Miss South Africa Rolene Strauss in a pale pink number.

Miss England Carina Tyrrell shows off her evening gown during the formal wear section of the final
Miss Venezuela Debora Menicucci parades in her gown during the grand final
 Miss South Sudan Awien Kuanyin-Agoth
 A heavily-bejewelled Miss Netherlands glides across the stage


AMBASSADOR LIBEATA MULAMULA VISITS TANZANIA COMMUNITY IN CHICAGO

$
0
0
riday December 12, 2014 The Tanzania Midwest Association was honored by the presence of The United Republic of Tanzania Ambassador to the US & Mexico Mrs. Liberata Mulamula standing in front far right.  She is accompanied by Dr. Switbert Z. Mukama Counselor/Public Affairs and her son Alvin.  Saturday evening December 13, 2014 she meets with a larger Tanzanian Community in the Midwest at Midwest Conference Center, 401 W. Lake Street. Northlake IL 60164.

BALOZI KAMALA AKIWA NA WAHITIMU WA KITUO CHA CHEKECHEA CHA FRORENCE

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa na baadhi ya Wahitimu wa Kituo cha Chekechea cha Frorence cha Kigogo Dar es salaam.

BALOZI KAMALA AANZISHA MFUKO WA ZAWADI WA DR. KAMALA "Dr. KAMALA AWARD FUND"

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (aliyevaa miwani) akizungumza katika Mahafari ya Kituo cha Chekechea cha Frorence yaliyofanyika Kigogo Dar es salaam. Watoto mia moja wamehitimu katika Kituo hicho na wote wamejifunza na kuelewa  kusoma na kuandika. Balozi Kamala amewashukuru Bwana na Bibi Mbezi kwa kuanzisha kituo hicho. Aidha, Balozi Dr. Kamala ameanzisha mfuko wa zawadi wa Dr. Kamala "Dr. Kamala Award Fund" utakaokuwa unatoa zawadi kila mwaka kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Baada ya Balozi Kamala kutoa laki moja za kuanzisha mfuko huo wazazi walimuunga mkono kwa kuchangia laki moja. Balozi Kamala amehaidi kuchangia milioni moja mfuko huo na riba itakayopatikana kila mwaka itatumika kutoa zawadi kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Vile vile Balozi Kamala alichangia shilingi laki mbili na nusu kituo hicho na amehaidi kukitafutia wafadhili wa kukisaidia.

MATOKEO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014 MANISPAA BUKOBA

$
0
0
Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 66 ndani ya Manispaa Bukoba,chama cha mapinduzi CCM wamepata mitaa 35 DHIDI ya Umoja wa UKAWA walio jinyakulia mitaa 31.
Jumla ya Wajumbe 330 walitakiwa ambapo Wapinzani wamefanya vizuri zaidi kwa kupata WAJUMBE 205 dhidi ya CCM waliopata WAJUMBE 125
  HukoWilayani Karagwe,Wilaya yenye jumla ya mitaa/vijiji 18 UKAWA wamejinyakulia Vijiji/Mitaa 12 na Chama cha Mapinduzi CCM wamepata vijiji/mitaa 6 kati ya 18.
Wakazi wa eneo la Katotorwansi-Kata kashai wakiwa tayari kuyapokea matokeo
 Pichani anaonekana Ndugu Masoud Zuberi (Kipara)  mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa ndiye Mwenyekiti wa Mtaa wa Katotorwansi-Kata kashai.
Wa pili pichani kula ni Mkurugenzi wa ulinzi na Usalama @Chademataifa Wilfred Lwakatare
Ndugu Masoud Zuberi katika furaha na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kashenye-Kashai Ndugu Nuruhudah Kabaju.
 Usikose lile Tamasha maalum la Krismas kutoka kwa Waimbaji mahiri wa muziki wa Injili, 'Kapotive Star Singers Bukoba' litakalofanyika katika ukumbi wa Linas Night Club
BUKOBAWADAU BLOG tunakutakia maandalizi mema ya sikukuu yakrismas  na heri ya mwaka mpya wa 2015
 Tupo na Nyumbani Studio, hii ni studio mpya na ya kisasa kabisa ambayo imefunguliwa Mjini Bukoba wako jirani na Ofisi za Finca mkabala na lango la Soko la Ndizi watakutendea haki na kazi yako ,Nyumbani Studio inakufanya unukie kiujana zaidi hata kama age yako imeenda.
Kwa huduma bora za kupamba katika Sherehe mbalimbali na kwa shughuli za kitaifa na kiselikali, vyama, midahalo ya kijami wasiliana na Mama matungwa Mkurugenzi wa Advents Signature Events
BUKOBAWADAU BLOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241



MIAKA 4 JELA KWA KUMTESA MTOTO MDOGO!!

$
0
0
Mahakama nchini Uganda imemhukumu kwenda jela miaka minne mfanyakazi wa ndani (House girl) Jolly Tumuhiirwe ,aliyepatikana na hatia ya kumtesa na kumpiga mtoto mwenye miezi 18. 
Katika video iliyosambaa mitandaoni hivi karibuni House girl huyu alionekana akimpiga bila huruma mtoto Aneela.
Mfanyakazi huyo alijitetea na kusema hakujua nini kilitokea hadi kufikia kufanya unyama huo.

WAHAYA JINA LA MWAKA MPYA 2015 NI "IJUKA" !!

$
0
0
Kama kawaida Wahaya tuna kawaida ya kuibatiza miaka kabla haijaanza. 
Katika muendelezo huo  tayari mwaka mpya wa 2015 umeisha pewa jina nalo ni  'IJUKA' 
Ikumbukwe kila jina huwa na maana halisi kwa kuhusishwa na matukio yaliyojili kwa  mwaka uliopo au hali halisi ya watu na maisha yao katika mchakato mzima wa kimaisha mpaka kuukamilisha mwaka uliopo.

 MWENYEZI MUNGU ATUJALIE TUWEZE KUMALIZA HUU MWAKA SALAMA 'Omukama singa atubeele tugil'emirembe'!!

--- Article Removed ---

$
0
0
***
***
*** RSSing Note: Article removed by member request. ***
***

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI FREDERICK WAREMA AJIUZURU!

$
0
0
Mwanasheria mkuu wa serikali, jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, jumanne, Desemba 16, 2014 na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Taarifa kutoka ikulu zimesema katika barua yake kwa mhe. Rais Kikwete, jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe.Rais Kikwete amemshukuru jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu

TAMKO LA CCM UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Chama cha mapinduzi CCM kimesema hakioni sababu ya suala la waliohusika kusababisha dosari zilizojitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura kuundiwa tume au kuchunguzwa wakati wanajulikana, badala yake wachukuliwe hatua, huku kikieleza kusikitishwa na mapungufu yaliyojitokeza ambayo wamedai yalitokana na uzembe wa watendaji wachache.
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Bw Nape Nnauye ameyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wakati umefika utaratibu wa kuunda tume kila jambo ufe kwani ni matumizi mabaya ya fedha na mwisho wa siku zinaleta ripoti machungungu ya jambo yakiwa yameisha hivyo haifanyiwi kazi tena huku akielezea namna CCM ilivyofanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha kwa mara ya kwanza Bw Nape amevipongeza vyama vya upinzani kwa hatua vilivyofikia lakini akadai kuwa kwa umri waliofikia tangu vianzishwe hapa nchini havikupaswa kuwa hatua vilivyopo hivi sasa bali walitakiwa kuwa mbele zaidi huku akivitaka kutekeleza yale yote waliyoahidi kwa wananchi waliowapa dhamana na kuongeza kuwa furaha ya CCM ni kuona mfumo wa ushindi unakuwa.

LIPUMBA:Walioshindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wawajibishwe.

$
0
0
Chama cha wananchi -CUF- kimemtaka rais Jakaya Kikwete kumuwajibisha waziri mkuu na waziri wa tamisemi kwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na baada ya kuibuka dosari kubwa zikiwemo kukosekana kwa wino, majina ya wananchi na karatasi za kupigia kura jambo lililote vurugu na kusababisha vituo vingi kurudiwa uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa CUF taifa Prof. Ibrahim Lipumba ametaka serikali kutekeleza makubaliano ya vyama vya siasa na tamisemi yaliyotaka uchaguzi tume ya taifa ya uchaguzi ndio iwe na dhamana ya kusimamia uchaguzi, pamoja na daftari la wapiga kura litumike katika uchaguzi wa serikali za mita pamoja na kuingizwa kwa kipengeke cha maadili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Aidha kutokana na vurugu zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika baadhi ya maeneo, Profesa Lipumba amelitahadharisha jeshi la polisi kuhacha kutumia nguvu kwa ajili ya kulinda maslahi ya baadhi ya vyama ili kuepusha vurugu zisizoza lazima katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani.

MTOTO AOKOLEWA NDANI YA SHIMO LA CHOO

$
0
0
Mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja ameokolewa na wasamaria wema toka kwenye shimo la choo akiwa bado  hai bada ya mama yake mzazi kumeza dawa kwa lengo la kutoa mimba na kumtupa ndani ya shimo hilo.
ITV imefika katika kituo ch afya cha PK  kilichopo kibaoni tegeta manisipaa ya kinondoni  jiji la Dar-es-salaam na kukutana na harakati za wahudumu wa afya wakijaribu kunasua mabaki ya kinyesi kwenye mwili wa kiumbe huo,aliyetupwa kwenye shimo la choo katika eneo la tegeta machakani.
Wakiongea na ITV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mama aliyekuw ana muhifadhi kwa muda binti anayedaiwa kutupa kichanga hicho wamesema kuwa watoto walipata taarifa ya mlio wa sauti wa mtoto ukisikika toka kwenye choo cha shimo kabla ya kuchukua hatua za kuvunja choo hicho na kutoa mwili wa kiumbe huyo.
Bi Aisha Mohamedi anayedaiwa kutupa kichanga hicho kwenye shimo la choo amesema kuwa,awali mzazi mwenzake alimlazimisha kutoa mimba hiyo bila mafanikio na hata kudiriki kumtishia kwa silaha aina ya kisu,na ndipo alipozidiwa na kupewa vidonge na mzazi mwenzake kwa minajili ya kutoa ujauzito huo na kukiri kujutia kosa lake hilo.
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya cha PK Dkt Mashaka Mwanula amethibitisha  kupokea mtoto huyo wa kiume aliyeokolewa baada ya kutupwa ndani ya choo na hivyo kumpatia huduma ya kwanza kwa kumsafisha huku wakitarajia kumpeleka katika hosip[itali ya wilya ya kinondoni mwananyamala kwa uchunguzi zaidi wa afya ya mtoto huyo,juhudi za kumpata kamnada wa polisi mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Camilius Wambura kuthibitisha tukio hilo zinaendelea.

BALOZI KAMALA AKARIBISHWA JIJINI WETTEREN UBELIGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akilisikiliza maelezo kuhusu zawadi aliyokabidhiwa kama ishara ya kumkaribisha jijini Wetteren Ubeligiji. Anayetoa maelezo ni Mhe. Live De Gelder Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii jijini Wetteren. Balozi Kamala leo atatembelea viwanda mbalimbali jijini Wetteren na atakutana na Wafanyabiashara kueleza fursa za biashara na uwekezaji Tanzania.

OFISI YA WAZIRI MKUU KUIMARISHA MIFUMO YA UTOAJI WA TAARIFA ZA TAHADHARI NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Harrison Chinyuka (Katikati) akisisitiza jinsi menejimenti ya maafa inavyotekelezwa kwa Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Taarifa za Tahadhari kuhusu Tabia nchi na Mifumo ya Tahadhari nchiniwakati wa mkutano wa wadau wa mradi huo leoJijini Dar es Salaam, (kushoto) Mwakilishi wa UNDP, Tanzania wa mradi huo,  Bw. Abbas Katogo, (kulia) Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Fanuel Kalugendo,
Baadhi ya wadau wa Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Taarifa za Tahadhari kuhusu Tabia nchi na Mifumo ya Tahadhari nchini wakifuatilia mkutano wa kujadili maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo leo Jijini Dar es Salaam, (wa kwanza ) ni Mratibu wa mradi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Bw. Alfei Daniel.
Baadhi ya washiriki wa Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Taarifa za Tahadhari kuhusu Tabia nchi na Mifumo ya Tahadhari nchini wakifuatilia mkutano wa kujadili maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Harrison Chinyuka (Katikati kwa walio kaa) akiwa na wadau wa Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Taarifa za Tahadhari kuhusu Tabia nchi na Mifumo ya Tahadhari nchini mara baada ya kufungua  mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.

DOZI YA LEO JUMATANO DEC 17,HIVI WEWE VIPI?!

$
0
0
Labda niongee na wanaume leo, najua labda uko karibu sana na mama yako mzazi, najua unampenda sana, najua labda wewe ndio wa kiume peke yako kwenu, najua jinsi mama yako alivyoteseka sana kwa ajili ya maendeleo yako hadi hapo ulipo leo na hauna budi kumheshimu na kumpenda, najua vyote hivyo na nina viheshimu sana, hata mimi pia nina mpenda mama yangu na kumheshimu, kama wengine wengi pia walivyo, ila nafasi ya mama inabaki kuwa ya mama na nafasi ya mke wangu inabaki kuwa ya mke wangu. 
Iweje leo mama yako ndio mwamuzi mkuu wa masuala ya maisha yako na familia yako?? mjenge wapi? nyumba ya aina gani? mzae watoto wangapi? mkaishi wapi na muishi vipi? muda wa kumtembelea anaamua yeye, muda wakuwaona wajukuu anaamua yeye, maisha ya mke wako mama yako pia ndio atoe maamuzi, kila unachopanga na mkeo lazima kwanza umshirikishe mama yako akipitishe au kukipinga,labda hata yeye ndio bado anakulazimisha uendelee kuishi kwa wazazi hadi leo, mama yako ndio kashika "remote control" ya familia yako na maisha yenu kwa jumla. 
 Wewe vipi??? Hivi unafahamu maana halisi ya uamuzi wa kuoa?? Kama ulikua bado hujapevuka vyakutosha siungeendelea kuishi na mama yako?? Hivi unadhani mkeo anafurahi hata kama hakwambii? Hata wewe ungekuwa mwanamke leo, ukaolewa, ukweli ni kwamba usingeweza kuvumilia hiyo hali, sasa jiulize yeye anapata wapi kifua cha kukuvumilia wewe na huyo mama yako hadi leo. Tafakari, chukua hatua, amua kubadilika - Dr. Chris Mauki

WACHEZAJI YANGA WAMLILIA MAXIMO

$
0
0
Mechi kama hiyo ilipofanyika mwaka jana, 2013, Yanga ilifungwa magoli 3-1 na kusababisha aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts kutimuliwa pamoja na benchi lake la ufundi. Mwaka huu ni zamu ya kocha Marcio Maximo kufungashiwa virago vyake baada ya kunyukwa mabao 2-0 katika mechi ya Mtani Jembe iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na huu ukiwa ni mchezo wa nane wa ushindani baada ya michezo saba tu ya ligi kuu ya Vodacom ya nchi hiyo.
KOCHA Maximo ambaye alipokelewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki na wanachama wa Yanga mwezi Juni mwaka huu baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu yao, amewaaga rasmi wachezaji wa timu hiyo kwenye mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es Salaam.
Mazoezi hayo ya Jumanne asubuhi yaligeuka simanzi baada ya Maximo kuwakusanya wachezaji wake na kuwambia kuwa kuanzia hiyo jana hakuwa kocha wa timu hiyo tena na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa klabu hiyo walielezea kutoridhishwa na uamuzi wa uongozi wa klabu hiyo kumuacha kocha wao na mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda.
Mmoja wa wachezaji hao alisema "Ni kweli kocha ametuaga asubuhi daa! ndio hivyo tumesikitika lakini hatuna jinsi."
 Naye mchezaji mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Inaumiza sana jana (juzi) tumefanya nae mazoezi vizuri kabisa tena amechangamka kama kawaida kumbe nyuma kuna mambo yanaendelea, leo asubuhi tumeenda mazoezi kama kawaida tukijua tunafanya mazoezi matokeo yake anasema acheni kila kitu kaeni hapo nataka kuzungumza na nyinyi".
Mchezaji mwingine wa timu hiyo alisema "Hakuna mchezaji kwa kweli aliyependezwa na kitendo cha uongozi, yaani kwenye mazoezi asubuhi ilikuwa kama msiba, 'mood' ya kufanya mazoezi iilisha kabisa, yaani hakuna aliyekuwa na hamu ya kuendelea na mazoezi.
"Tumefanya kidogo mazoezi tukaondoka, ukiangalia ni sawa tumefungwa cha muhimu ilikuwa ni kukaa chini na kuzungumza na kuangalia cha kufanya, kama kuna mapungufu basi yafanyiwe kazi, mimi sijaona haja ya kumfukuza kocha hasa kipindi kama hichi."
Meneja wa timu hiyo Hafidhi Saleh alikiri Maximo kuwaaga wachezaji kabla ya mazoezi ya timu hiyo kwanza akiwapa moyo wajitume kwa kuwa ni wachezaji wazuri na timu ni nzuri na kuwataka kuongeza bidii ili wafike mbali.
"Kwa kweli inasikitisha hakuna mchezaji wala mtu aliyefurahia, kama yupo labda kimoyomoyo ila dah imetuumiza, ni mazoea cha muhimu tugange yajayo hayo mengine tuwaachie viongozi."alisema Saleh
 Mchezo wa Mtani Jembe ambao ni wa kujifurahisha na kuongeza utani kati ya timu hizo, umegeuka kuwa kipimo cha ubora wa kocha hata kama kocha huyo anafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu. Hadi wakati anafukuzwa, kocha wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo, timu yake inashika nafasi ya pili baada ya Mtibwa inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na michezo saba tu iliyochezwa.
Baadhi ya mashabiki wameunga mkono uamuzi wa kumtimua Maximo wakisema timu haikuwa na uwezo wa kupambana na timu pinzani, huku wengine wakipinga uamuzi huo kuwa haukustahili kuhukumu uwezo wa kocha huyo katika mchezo mmoja wa kirafiki na kusahau nafasi inayoshikiliwa na timu katika msimamo wa ligi kuu.

DK MASSABURI AFUNGUKA SAKATA LA ESCROW KWA MARA YA KWANZA

$
0
0

 SEHEMU YA VIDEO HAPO JUU DK MASSABURI AKIONGELEA  SAKATA LA ESCROW
 Dk. Massaburi:

Tusimtwishe Rais Kikwete mizigo mizito
WATANZANIA wameombwa kumuonea huruma na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuiletea Tanzania maendeleo katika kipindi cha miaka 9 ya uongozi wake, na si kumkatisha tamaa kwa kumtwisha mizigo mizito.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT), Dk Didas Massaburi aliyasema hayo wakati alipokuwa anazungumzia mzigo mkubwa aliokabidhiwa Rais Kikwete wa kutekeleza maazimio manane ya Bunge kuhusu sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha zinazodaiwa kuwa ni za umma katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
 

Dk Massaburi alisema hivi sasa suala la Escrow limeleta mtafaruku na madhara makubwa ndani ya nchi kutokana na kupotoshwa na kikundi cha watu wachache wenye maslahi binafsi, hatua ambayo sasa inamfanya Rais kuacha kushughulikia maendeleo ya nchi na kulishughulikia suala hilo.
“Tufike mahala tuache kumbebesha Rais wetu mizigo mizito na isiyo na sababu kwani amefanya mambo mengi na makubwa na yanayogharimu matrilioni ya shilingi katika ujenzi wa barababara, umeme, maji na elimu.

“Leo hii kutokana na sakata la Escrow ambalo fedha zinazodaiwa kuwa ni za serikali haziwezi hata kujenga barabara mbili za lami, nchi inapita katika wakati mgumu sana,” alisema Dk Massaburi.
Alisema ALAT kama mdau mkubwa wa maendeleo katika serikali za mitaa na hasa vijijini inaguswa na sakata hilo kwa vile sasa serikali inaendelea na kazi kubwa ya kupeleka umeme vijijini na hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa vijijini bila nishati ya umeme.
Alisema suala la Akaunti ya Tegeta Escrow limepotoshwa na watu wenye maslahi binafsi yakiwemo ya kutaka kukubalika kwenye nafasi za Ubunge, Umeya na hata Urais na kwa bahati mbaya wananchi wameingiwa na imani kali kuhusu upotoshaji huo na kujenga chuki kubwa kwa serikali yao.

 “Hali imekuwa mbaya sana bila sababu ya msingi, watu wanashindwa kufanya shughuli muhimu za maendeleo kwa suala la Escrow. Imefika mahala tunaweka shinikizo la kutaka kuwajibishwa kwa viongozi wachapa kazi na walioliletea maendeleo makubwa Taifa letu kwa masuala yanayopotoshwa tu, jambo ambalo ni la hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu,” alisema Dk Massaburi. 
Alisema mbali ya wanasiasa, taasisi za kifedha za kigeni pia zinalishabikia suala hilo kutokana na ulafi wa kutaka kuzichukua fedha hizo na wala si kuwapa wananchi na pia kampuni za kigeni za umeme ambazo zinaathirika na bei ndogo ya umeme inayouzwa na IPTL ukilinganisha na wao, zinahusika.
“Kwa bahati nzuri mimi nimeisoma vizuri sana taarifa ya CAG, hakuna mahala anaposema fedha ni za umma. Fedha ya umma inajitokeza katika ulipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na ambayo kwa kawaida kodi hii hulipwa na aliyelipwa.
“Mimi nikilipwa fedha leo, napokea kwanza hundi yangu halafu baada ya kuchukua fedha na kuwa mikononi mwangu ndio mwisho wa mwezi nakwenda kulipa kodi ya VAT, hawakati fedha hiyo moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yangu. TRA wanapaswa kuifuatilia kodi yao maana hapa ni suala la sheria ya Kodi kukiukwa hakuna Sheria ya Escrow,” alisema Dk Massaburi. 

Alisema kwa namna taarifa ya CAG ilivyofafanua hakuna ubishi kwamba IPTL sasa inamilikiwa kihalali na Kampuni ya PAP, na hivyo ni lazima kama Taifa kuipa ushirikiano kampuni hiyo kuendelea kuzalisha umeme na kuuza kwa bei nafuu na si kushinikiza kutaifishwa kwa mitambo hatua ambayo italiingiza Taifa kwenye matatizo makubwa ikiwemo kurejea kwenye bei kubwa ya umeme.
“Mazungumzo kuhusu Escrow ni ya miaka mingi sana, yalianza tangu enzi za Ngeleja (William- aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini. Watu hawa wamezungumza suala hili kwa zaidi ya miaka minane.Leo hii mtu anapotosha kwamba makubaliano ya kuondoa fedha kwenye akaunti ya Escrow yalifanywa siku moja tu pale Kunduchi Beach.
“Tuwasaidie viongozi wetu wanaofanya kazi nzuri ili kulikoa Taifa letu. Rais anafanya kazi nzuri, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda ) anafanya kazi nzuri, Waziri Muhongo anafanya kazi kubwa na nzuri. Hawa ni watu muhimu sana kwetu,” alisema Dk Massaburi ambaye alitangaza kutokuwa na mgongano wa kimaslahi kwa sakata hilo. 

NANI WA KULAUMIWA
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kutokana na uzoefu wake katika masuala ya hisa za kampuni, amegundua kuwa sakata ta escrow linachochewa na makundi mawili.
“Kundi la kwanza ni wapotoshaji wakiwamo wabunge, wachumi ambao walikuwa wakisambaza upotoshaji huo kwa masilahi yao binafsi...mtu mwingine anaweza kusema ninatetea labda nimepata mgao, hapana...ila ukweli unatakiwa uelezwe wazi.”
Dk Massaburi alitaja kundi lingine aliloliita la fisi ambalo lina idadi kubwa ya wapambe waliokuwa na njaa ya kupata mgao huo.
Alisema hakuna kiongozi anayetakiwa kuwajibishwa kutokana na ukweli kwamba, Kampuni ya Mechmar ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa tatizo hilo.
Mwaka 2010, kampuni ilikabidhi umiliki wake wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda kwa Kampuni ya Piper Link

NENDA AISHA MADINDA

$
0
0

Na Happiness Katabazi
MNENGUAJI wa Muziki wa Dansi nchini ambaye aliwahi kujizolea Umaarufu mkubwa Katika medani za muziki wa dansi Kipindi kile wakati akiwa mcheza show wa Bendi ya African Stars' Twanga Pepeta, Extra Bongo, amefariki Dunia mchana huu.
Nikiwa Kama mwanahabari na Mpenzi wa muziki wa dansi nchini,nilikuwa nikiudhuria maonyesho ya bendi ya Twanga Pepeta Kwani imekuwa ni bendi inayotoa burudani nzuri na Marehemu Aisha alilitumikia kwa muda mrefu.
Hakuna ubishi Kuwa Aisha alikuwa na mvuto wa aina yake awapo stagini na ataakiwepo nje ya kazi yake hiyo ya unenguaji.Aliweza kuifanya kazi yake ya unenguaji vizuri.Nilikuwa napenda kazi yake.
Kuna Msemo usemao Kuchunga Umaarufu wako usipotee ni kazi sana.Naweza Kusema Aisha Hilo lilimshinda la Kuchunga Umaarufu wake Kwani akiwa Twanga na hata alipoama Twanga, marehemu alikuwa akituhumiwa kufanya matendo ambayo yaliporomosha Umaarufu wake kwa kasi Hali liyosababisha mashabiki wake Wengi kupoteza mapenzi kwake na kuanza kupotea Katika majukwaa ya muziki wa dansi.
Hakika Aisha umetutoka ila familia yake itambue Kuwa umeacha alama ya kukumbukwa Katika tasnia ya unenguaji hapa Tanzania.
Wananguaji chipukizi jifunzeni Mema yaliyofanywa na dada yenu Aisha na Manaa yake msiyaige.Naamini mkifuata moyo wake wa kujituma na kuipenda kazi yake ya unenguaji ,Matafika Mbali.
Ukitazama Video ya Wimbo wa Mtu pesa, msinijadili, Famili Confrict ,Nyimbo zote hizo mali ya bendi ya Twanga Pepeta,tu akubaliana na Mimi Kuwa marehemu Aisha Madinda alikuwa ni mnenguaji mzuri.
Wapenzi wa muziki wa dansi nikiwemo Mimi nimesikitishwa sana na kifo Chako.Pole Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka maana ni miongoni mwa watu waliomlea Aisha Kimziki hadi hapo alipofikia.Pole familia ya marehemu.
Aisha sisi tulikulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi. Mungu ailaze roho yako mahali panapo Stahili.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Disemba 17 Mwaka 2014.

MDH KUTOA BURE HUDUMA YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI-MJINI BUKOBA

$
0
0
Shirika la Usimamizi na Maendeleo ya Afya (MDH) ,shirika la JHPiego na Wizara ya afya wameanza kutoa huduma za Dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi ,Mkoani Kagera,huduma hii tayari imeanza  toka Jana tarehe 17  hadi 20 desemba 2014 katika hospitali ya Mkoa iliyopo Mjini Bukoba. 
Wanawake wanashauriwa kujitokeza kwa wingi,huduma ni bure!!

BALOZI KAMALA AITANGAZA TANZANIA WETTEREN UBELIGIJI

$
0
0
 Picha zinaonesha Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akibainisha fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana Tanzania katika Kongamano la kuitangaza Tanzania lililofanyika Wetteren Ubeligiji.
Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji umeandaa Kongamano hilo kwa kushirikiana na kampuni za Recticel, SGS, Zonpunt na Chuo Kukuu cha Ghent.
Matukio ya picha wakati Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akibainisha fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana Tanzania katika Kongamano la kuitangaza Tanzania lililofanyika Wetteren Ubeligiji.
 Picha zinamuonesha Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea maua kutoka kwa mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Wetteren Ubeligiji baada ya kuelezea fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania. Wafanyabiashara hao wamemshukuru Balozi Kamala kuwatembelea na kuwaeleza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania.
 WAFANYABIASHARA WA WETTEREN UBELIGIJI WAMSHUKURU BALOZI KAMALA
 Picha zinaonesha Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa na Washiriki mbalimbali wa Kongamano la Kuitangaza Tanzania lililofanyika Wettrern Ubeligiji.
Viewing all 4180 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>