Quantcast
Channel: BUKOBA WADAU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4177

WATU 4 WAUAWA KANISANI NCHINI KENYA

$
0
0

Watu wanne wameuawa baada ya watu waliojihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi ndani ya kanisa mjini Mombasa Pwani ya kenya. Watu wengine kumi na saba wamejeruhiwa vibaya. Maafisa wa polisi katika mtaa wa Likoni ambao uko kusini mwa Mombasa wamesema kuwa majambazi hao walilivamia kanisa hilo na kuanza kuwafyatulia risasi waumini hao kiholela. Usalama umeimarishwa katika eneo hilo kufuatia kutiwa mbaroni kwa watu wawili siku ya Jumatatu ambao polisi wanadai walikuwa wakimiliki mabomu yaliofichwa ndani ya gari yao. Kumekuwa na visa tofauti vya ghasia mjini Mombasa katika miezi ya hivi karibuni vinavyoshirikisha vikosi vya usalama na Waislamu wenye itikadi kali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4177

Trending Articles