Mwalimu mkuu shule ya msingi Ntanga Mwl. Sendabaye Justus akikabidhiwa kinyago baada ya shule yake kupata ufaulu wa wastani wa 16% matokeo ya darasa la saba mwaka jana
Katibu Tawala wilayani Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka akikabidhi kinyako kwa Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura
Picha zote na habari kwa hisani ya ya Shaaban Nassibu Ndyamukama kutoka Ngara.
Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura akipokea kinyago kutoka kwa katibu Tawala wilayani Ngara Vedastus Tibaijuka baada ya kata yake na tarafa kupata ufaulu duni wa 39% kwa kata & 52% kwa tarafa
Katibu Tawala wilayani Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka akikabidhi kinyako kwa Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura
Picha zote na habari kwa hisani ya ya Shaaban Nassibu Ndyamukama kutoka Ngara.
Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura akipokea kinyago kutoka kwa katibu Tawala wilayani Ngara Vedastus Tibaijuka baada ya kata yake na tarafa kupata ufaulu duni wa 39% kwa kata & 52% kwa tarafa
Pichani ni Mwalimu mkuu shule ya msingi Ntanga Mwl. Sendabaye Justus
IDARA ya elimu ya Msingi wilayani Ngara Mkoani Kagera imejiwekea mikakati ya kukutekeleza malengo ya kitaifa ya Big Results Now kwa 70% baada ya kupata walimu wapya 139 mwaka huu watakaoungana na 1543 waliokuwepo awali.
Katika utekelezaji huo wazazi , walimu na wanafunzi katika shule , na kata zilizoko tarafa ya Murusagamba wilayani humo wametakiwa kuongeza juhudi za kuinua kiwango cha taaluma katika tarafa hiyo ili kuingia katika wa malengo hayo
Ofisa elimu idara ya msingi wilayani Ngara Simon Mumbee alisema hayo juzi kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu wilayani humo na kudai tarafa hiyo iko nyuma kitaaluma katika shule zake 13 zilizoko kata ya Muganza na Mursagamba
Mumbee alisema tarafa hiyo imekuwa ya mwisho katika ufaulu wa mitihani ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata 52% ya wastani wa ushindi kitaifa ambao ni 60% na kata ya murusagamba ilikuwa ya mwisho kiwilaya kwa ufaulu wa 39%
Alisema kuwa katika wastani wa ufaulu kitaifa mwaka jana wa 60% tarafa ya Kanazi ilifaulisha kwa wastani wa 76%,Rulenge 71% na Nyamiaga 70% na kwamba wilaya hiyo ilikuwa na wategemewa wa kufanya mtihani 3913 katika shule 118.
Alifafanua kuwa mwaka jana wilaya hiyo ilikuwa na watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 3861 wavulana 1790 na wasichana 2071 sawana 99% ambao walifaulu ni 2683 wavulana 1311 wasichana 1372 sawa na wastani wa 69.5%.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na ufaulu huo bado katika shule 903 zilizoko Mkoani Kagera shule ya msingi Ntanga kata ya Murusagamba wilayani humo ilikuwa ya mwisho kimkoa kwa kuwa na wastani wa 16%
“Napenda kuwatia moyo uongozi wa tarafa kata na shule wakiwemo wazai na wanafunzi wenyewe kuoneza juhudi ili kuweza kufanya vizuri kwa matokeo ya mitihani mwaka huu”Alisema Mumbee
Aliongeza kuwa idara ya msingi wilayani humo ina jumla ya shule za msingi 118 kati ya hizo shule nne ni za binafsi na nyingine za serikali zote zinao wanafunzi wa elimu ya awali 12188 kati yao wavulana ni 5292 na wasichana ni 5356.
Pia shule hizo zinawanafunzi wa darasa la kwanza hadi la saba wapatao 73978 kati yao 36758 ni wavulana na 37220 ni wasichana ambapo wanafunzi wa elimu ya MEMKWA ni 2200 kati yao wavulana ni 1355 na wasichana 845.
Kwa upande wake afisa elimu Taaluma Fidelis Apolinari alizitaja shule zilizofanya vizuri katika mtihani na kutuzwa zawadi na vyeti vya taaluma bora kuwa ni Prince (English Medium) ya kwanza kiwilaya, kimkoa na ilikuwa ya saba kitaifa
Alitaja pia shule ya Mwanga (English Medium) ambayo ilikuwa ya pili kiwilaya ya tano kimkoa na 14 Kitaifa huku Rhec (English Medium) ilikuwa ya tatu kiwilaya na saba kimkoa ambapo kitaifa ni ya 17 kati ya shule
Alisema shule nyingine ambazo ni shule za serikali zilizofanya vema ni Murgwanza Ngara mjini , Murukukumbo, Kabalenzi , Mubinyange, Nakatunga na Ntungamo ambapo kata ya kwanza ni Ngara mjini yenye ufaulu wa wastani (98%)
“Shule zenye taaluma hafifu ni Ntanga ,Murugunga ,Rusengo Kabaheshi
Kirushya, Nyankende ,Ntobeye, Kasulo, Kanyinya na Kabulanzwili”. Alisema
Kwenye kilele cha wiki ya elimu iliyopambwa kwa kauli mbiu isemayo Elimu bora Kuboresha Mtanzania katika wilaya hiyo kata tarafa na shule ilizokuwa za mwisho zilizawadiwa vinyago na cheti chenye taaluma hafifu.
Pamoja na taarifa hiyo Katibu Tawala Vedastus Tibaijuka kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu katika hotuba yake aliwataka walimu kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kuboreshewa mazingira ya kufundishia
Tibaijuka alidai walimu katika wilaya hiyo wanahitaji kuwa na nyumba za kuishi katika shule zao kupata zana bora za kufundishia na kupata mafunzo elekezi katika kuwaongezea ujuzi na maarifa kulingana na mabadiliko ya teknolojia.
Alitaja baadhi ya changamoto katika utoaji wa taaluma kuwa ni ulevi wa walimu na kujihusisha na biashara ya bodaboda saa za kazi , mikopo mingi katika taasisi za kifedha na hatimaye kushindwa kuwajibika kiutumishi na kifamilia.
MWISHO.